Nyumba ipi naweza kuikamilisha kwa 7M nikahamia kati ya hizi?

Nyumba ya kwanza hujengwa kwa hatua, mil saba inaweza kukukufanya uhamie kwenye gofu , then utaendeleza ukiwa uko ndani
Kusema mil 7 ukamilishe kila kitu kwa ramani ulizotoa hapo ni uongo,
Dirisha tu la alluminium linakamilika kwa 300,000 hapo naona unayo matatu upande mmoja
 
Shukran sana mkuu
 
Shukran mkuu, me lengo langu nipate jengo nipige plasta, niweke floor ya kawaida tu, niweke grill, Umeme na ikiwezekana nifunge gypsum board basi, je NITAWEZA???
 
Huu ndio ushauri murua ukishupaza shinga utajutia
 
Haitoshi mkuu
Inategemea na eneo ulilopo
Ukibana saaana
Kwa haraka haraka kusimamisha boma
Msingi utakula mil. 2
Tofali ni kama 1800pcs=mil. 1.8
Cement mifuko 70pcs= mil. 1.4
Mbao na bati mil. 3
Na hapo bado sana make kuna
Slab
Brandaling za gypsum
Gypsum board
Plasta
Wearing ya maji na umeme
Vigae
Na vitu vingne vingi inategemea decoration zako unazotaka
 
Shukran mkuu, me lengo langu nipate jengo nipige plasta, niweke floor ya kawaida tu, niweke grill, Umeme na ikiwezekana nifunge gypsum board basi, je NITAWEZA???
hiyo pesa haiwezi tosha makorokoro yote hayo!
Kama lengo ni kukimbia kadhia za wenye nyumba jenga boma tu ikiwezekana hata room moja , grills ,umeme, floor plasta .nk utafanya ukiwa ndani kwako, kuna watu wanahamia hata choo hajachimba na maisha yanaendelea
 
Una milioni saba na bado unafikiria ramani zenye choo na jiko??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…