Haya nayo ni mawazo fulani ya ajabu sana mkuu,wakati najenga nyumba yangu kipindi sijaoa nilitaka room nne but aliyenipa ramani akaniyumbisha kwa kauli kama hii akaniambia room tatu zinatosha leo nina familia siifurahii nyumba yangu.
Sasa hivi nina watoto watatu wamechanganya jinsia,chumba kimoja wa kiume kingine wa kike so nikipata mgeni labda mama yangu inabidi alale chumba cha mtoto wa kike kuna mdogo anakojoa kitandani so inabidi asubuhi bi mkubwa nae alalamike halafu bado ninazaa,mwanangu wa kiume yupo 13 so nikipata mwengine leo akija kufika 5 kaka yake yupo 18 ningekuwa na chumba cha nne ningewagawa hawa kila mmoja na chumba chake but siwezi so inabidi niingie gharama upya nijenge servant quarter.
Nadhani hii kauli inawafaa wenye kikomo cha watoto labda wawili au mmoja kama mpenzi wa watoto haifai.