Nyumba nyingi hutumia mlango wa jikoni kuingia ndani badala ya mlango wa sebuleni, ni uchawi au ni nini?

Nyumba nyingi hutumia mlango wa jikoni kuingia ndani badala ya mlango wa sebuleni, ni uchawi au ni nini?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Kuna nyumba nyingi sana nilizowahi kutembelea, unakuta unakaribishwa ndani kwa kupitia mlango wa jikoni, na ule wa sebuleni unakuta haujawahi kutumika tangu nyumba ijengwe.

Hii husababishwa na nini, chanzo au lengo la tabia hii, ni nini?
 
Sifahamu aisee [emoji23]
 
Urithi wa kikoloni. Watu weusi hasa watumishi wa ndani kwa wazungu huko ulaya hawakuruhusiwa kupitia mlango mkubwa bali wa jikoni. Mkubwa ulikuwa ni wa wazungu pekee. Inaanzia hapo
 
Ni mazoea tu kutokana na muundo wa nyumba. Mara nyingi kutokana na shughuli nyingi kutendeka jikoni basi mlango wake huwa wazi mara zote na ili kuzuia ingia toka za watoto tunadhibiti mlango wa sebuleni na kuacha wa jikoni....

Pia kiusalama ni vyema kutumia mlango mmoja wa jikoni kuliko wa mbele sebuleni.

Naweza kuweka sababu hizi.
1. Kiusalama.
2. Udhibiti wa nyumba kwa watoto.
3. Mazoea.
 
Issue ni msosi na umbea tu.
Jikoni ndio kila kitu, huko ndiko kuna chakula na watu hutulia kupiga story za reja reja. Na kwa jinsi waafrika tunavyooendekeza tumbo na umbea basi ni muhimu kutumia mlango wake kuingia au kutokea.
 
Mlango mkubwa huwa hatumiki kwasababu
1. Usafi,
2. Unasumbua kufunga na kufungua
3. Ukifunguliwa unaonesha uwazi wa sebule na kushawishi michezo ya watoto kukimbilia nje
4. Kiusalama ni vigumu kumonitor mlango wa mbele ...
5. Zawadi na vikalagos ni rahisi kuvidrop jikon
6. Ni rahisi kuwazoom wagen uliowakuta kwa kupitia jikon
 
Niliwahi kupiga marufuku wanangu kutumia mlango wa jikoni wakiwa wanatoka shule. Maana nimekua napenda kuwaona kila wanapo ondoka na kurejea kutoka shuleni, hivyo maranyingi mlango wa mbele hutumika kuliko wa jikoni.
 
Tena umenikumbusha keshokutwa nikirudi nikauchomelee ule mlango mmoja wa mbele, maana huyu kijana wangu wa 7 kuzaliwa ashauvunja bawaba kwasababu ya kuning'inia kama konda wa daladala za tandale...🤨
 
Kwanza mlango wa jikoni ukitumika sana watoto wanafichaga viatu nyuma ya mlango, sasa wazazu ni ngumu kung'amua wapi pa kurekebisha ama hata kama wanapiga kiwi kila siku au pengine mtoto alinipigia mawe hadi kiatu kikafumuka..😎
 
Kuna nyumba nyingi sana nilizowahi kutembelea, unakuta unakaribishwa ndani kwa kupitia mlango wa jikoni, na ule wa sebuleni unakuta haujawahi kutumika tangu nyumba ijengwe.
Hii husababishwa na nini, chanzo au lengo la tabia hii, ni nini?
Kwa uzoefu wangu... Mlango wa sebule ulikuwa ukitumika wakija home wageni wa heshima tu!
Kwa hiyo inawezekana mleta uzi sio mgeni wa heshima kabisa
 
Kuna nyumba nyingi sana nilizowahi kutembelea, unakuta unakaribishwa ndani kwa kupitia mlango wa jikoni, na ule wa sebuleni unakuta haujawahi kutumika tangu nyumba ijengwe.

Hii husababishwa na nini, chanzo au lengo la tabia hii, ni nini?
Hii hutokana na kwamba mara nyingi shughuli nyingi hufanyika upande wa nyuma au upande wa jikoni wa nyumba na hivyo kufanya upande huo kua salama zaidi kuliko upande wa mbele au upande wa sebuleni. Na hivyo kufungua mlango wa mbele au sebuleni ni hatari zaidi kwani ni mara chache watu kuwepo sebuleni au upande wa mbele wa nyumba. Na hasa ukisaulika kufungwa wakati watu hawapo sebuleni au upande wa mbele wa nyumba.
 
Tena umenikumbusha keshokutwa nikirudi nikauchomelee ule mlango mmoja wa mbele, maana huyu kijana wangu wa 7 kuzaliwa ashauvunja bawaba kwasababu ya kuning'inia kama konda wa daladala za tandale...[emoji2955]
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji848]
 
Hii ipo ninapokaa, ninaishi nyumba ya upande wa nyuma kwenye geti dogo ila mbele kuna nyumba kubwa wanayoishi walionipangisha.
Lakin cha ajabu hawatumii mlango wao wa mbele ili watumie geti kubwa matokeo yake wanatumia mlango wa jikon so wote tunajikuta tunatumia geti dogo...
Sometime unakuja na babe wako ile unafungua tu geti unawakuta wamekaa kwenye kibalaza cha kuingia ndani kupitia jikoni.
Inaniboa sana..[emoji1785]

Sent from my SM-N960U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom