Nyumba nyingi hutumia mlango wa jikoni kuingia ndani badala ya mlango wa sebuleni, ni uchawi au ni nini?

Mkuu kwel hata mimi natumia mlango wa jikoni sijui shida ni nini lakin kuna wakat nakasirika kuzunguka kufuata kitu ndan wakati ningepita chap kwa haraka mlango wa mbele
 
Sembuleni ni dabo door na jikoni ni singo door pia jiografia ya nyumba ulazimika wa jikoni kutumika mara kwa mara
 
Kuna nyumba nyingi sana nilizowahi kutembelea, unakuta unakaribishwa ndani kwa kupitia mlango wa jikoni, na ule wa sebuleni unakuta haujawahi kutumika tangu nyumba ijengwe.

Hii husababishwa na nini, chanzo au lengo la tabia hii, ni nini?
Kuepuka uchafu /sebule kuchafuka .
 
Umesahau kuwa haufunguliwi ovyo ili kuwazuia wapiga chabo kuona vilivyopo sebuleni ili usiku waje kuvishughulikia
 
Kuna nyumba nyingi sana nilizowahi kutembelea, unakuta unakaribishwa ndani kwa kupitia mlango wa jikoni, na ule wa sebuleni unakuta haujawahi kutumika tangu nyumba ijengwe.

Hii husababishwa na nini, chanzo au lengo la tabia hii, ni nini?
mazoea
 
Inategemea jinsi nyumba ilivyo jiposition. Nyumba nyingi upande wa jikoni ndio kuna space na shughuli nyingi hufanyikia huko ikiwemo za kiusafi. Kwa sababu ya shughuli nyingi kufanyika huko ndio maana mlango huo unakuwa wazi muda wote. Ndio maana anapokuja mgeni wa aina yeyote inabidi umfungulie mlango wa mbele. Kama hukufunguliwa mlango wa mbele basi mwenyeji wako alikuchukulia kama mwenyeji
 
Kuna nyumba nyingi sana nilizowahi kutembelea, unakuta unakaribishwa ndani kwa kupitia mlango wa jikoni, na ule wa sebuleni unakuta haujawahi kutumika tangu nyumba ijengwe.

Hii husababishwa na nini, chanzo au lengo la tabia hii, ni nini?
Pamoja na sababu zingine lakini pia hata nyumba ikishajengwa tayari kama kunatokea uhaba wa milango basi utaanza kuwekwa wa nyuma then wa mbele, hivyo basi kutokana na hali hiyo kunajengeka mazoea ya kutumia mlango wa jikoni.
 
Jenga yako ufanye unavyotaka
 
Kuna nyumba nyingi sana nilizowahi kutembelea, unakuta unakaribishwa ndani kwa kupitia mlango wa jikoni, na ule wa sebuleni unakuta haujawahi kutumika tangu nyumba ijengwe.

Hii husababishwa na nini, chanzo au lengo la tabia hii, ni nini?
We hujui mlango wa mbele ni wa baba tu?
 
Sababu kubwa ni hizi
1. Kiusalama.
2. Udhibiti wa nyumba kwa watoto.
Nyumba ikiwa na watu wengi na milango yote ikawa inatumika upo uwezekano mlango mmoja kusauliwa kufungwa hivyo kuatarisha usalama

2.michezo ya watoto kama unaishi eneo ambalo Lina watoto wenzi mfano uswahilini basi tegemea mji wako kuwa sebule yako kuwa Banda la video watoto mtaani wote watajaa sebuleni kekao wakifuata watoto wenzao kucheza na kwakua si watoto wako jiandae kwa maumivu kuvunja remote ya tv au radio nk
 
Tatizo ni mlango wa mbele kutokea moja kwa moja sebuleni. Ungekuwa unatokea kwenye kaspace(foyer) ingekuwa haina tatizo.
 
Kuna nyumba nyingi sana nilizowahi kutembelea, unakuta unakaribishwa ndani kwa kupitia mlango wa jikoni, na ule wa sebuleni unakuta haujawahi kutumika tangu nyumba ijengwe.

Hii husababishwa na nini, chanzo au lengo la tabia hii, ni nini?
Mzee hio itakuwa ni coincidence yako tu
 
Ni ishu ya usalama kidogo,jografia kidogo, usafi kidogo,ila mazoea zaidi kwakua shughuli nyingi hufanyika kwenye eneo kubwa la mbele ya nyumba ambako mara nyingi ndio kunakua na mlango wa kutokea jikoni!!!ila mgeni mpya au ambae hana mazoea sana na nyumba akija ni lazima atafunguliwa mlango huo ila wageni wenyeji wao hawana shida wanapitia huo huo wa jikoni.

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…