Nyumba nyingi zinatelekezwa na wababa kisa akina mama. Hii ni baada kumsikiliza baba yake kijana Majaliwa, baba Dimpozi n.k

Nyumba nyingi zinatelekezwa na wababa kisa akina mama. Hii ni baada kumsikiliza baba yake kijana Majaliwa, baba Dimpozi n.k

ommytk

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
520
Reaction score
1,143
Nyumba nyingi wazazi wa kiume ama kina baba wanazikimbia na kuwaacha watoto kisa kikubwa inaonesha ni kina mama, hii ni baada kujitokeza mara nyingi wazazi wa kiume baada vijana wao kupata maendeleo flani mifano michache ni kama huyu kijana shujaa Majaliwa na watu maarufu kama Dimpoz na Diamond.

Kuna kitu kina mama huwa wanasababisha ambacho wazee wanaona Bora kukaa pembeni na kuwaacha watoto na mama yao ila bado anaondoka anawapenda watoto hali tu ya yule mama ndio inamkwaza.
 
Mwanamke akiwezeshwa anaweza.

Kampeni ya usawa wa kijinsia imefanikiwa asilimia 200%+.

Wanawake sasa wanashika usukani na hatimaye, wanashika na sharubu za wanaume.

Wamama sasa wanahisi wanaweza kuishi peke yao, ila baba akiondoka, wanagundua alooh! Kumbe bado mwanaume ana nafasi yake.

Kupanga ni kuchagua. Tumechagua kumwinua mwanamke, na ameinuka haswa!

Alamsiki!
 
Tusidanganye

Wewe na mimi tumeoana alafu tukashindwana kwa sababu zetu personal,haijalishi nani mkosefu!

Wewe ukaamua kuondoka,hivi kinachokuzuia kuhudumia watoto ni kipi adi usubiri afanikiwe ndo ujitokeze useme eti ni mwanao na unampenda?

Biblia inasema upendo hufadhili,wewe unajiita baba umeacha kumfadhili mwanao miaka 10+ alafu eti unasema unampenda ila mama yake ndo alikufanya usimsaidie?

Mtupumzishe jamani,mkiachana na wake zenu regardless of what lea watoto wako achana na visingizio visivyo na maana!

Mbona ulaya wanaachana ila bado baba analea watoto?au kwasababu sheria zao ni kali kuliko za kwetu?
Yani baba dizaini ya majaliwa ni wa kuchapwa viboko tu!
 
Tusidanganye
Wewe na mimi tumeoana alafu tukashindwana kwa sababu zetu personal,haijalishi nani mkosefu!
Wewe ukaamua kuondoka,hivi kinachokuzuia kuhudumia watoto ni kipi adi usubiri afanikiwe ndo ujitokeze useme eti ni mwanao na unampenda?
Hivi hata kama unahudumia mama anaweza kukubali unahudumia?

Lakini pia wanaume inatupasa kuwa karibu na watoto ingawaje wanajazwa sumu sana.
 
Wanawake ni tatizo sana tena sana , slogan ni Ile Ile tu, mwanamke akikuzingua mpak kiwango cha mwisho cha uvumilivu mwache, vinginevyo utafanya mauaji, mwachie kila kitu sepa, wanaume tumeumbiwa kupambana, popote kambi, cha msingi hao watoto endelea kuwahudumia, wakifanikiwa wakakutelekeza fresh tuu we umetimiza majukumu.

Mambo ya kumnyenyekea mtoto kisa kafanikiwa Kwa mwanaume mwenye akili timamu ni Ujinga wa Hali ya juu, yeye anatakiwa na ni wajibu kumkumbuka mzazi wake, kama hawezi leave him/her alone.
 
Daaàah hivi unajua watoto wengi waliotelekezwa na baba zao ni watoto wa mpango kando, yaaaan wengi wao ni baba kamuongopea mwanamke. Ommy dimpoz baba alikua ana familia teyari, diamond baba yake teyari alikua ana familia tena baba wote wawili, same to Majaliwa.

Mmejaa lawama kwa wanawake eti ndo sababu. Hamjiskii vibaya,hamuoni aibu kuwanyooshea vidole mama zenu kila siku. Kuna mwanamke hapendi kuona watoto wake hawalelewi na wazaz wote? Acheni utoto na kujitoa faham. Sikia story za pande zote mbili ndo muanze kubwabwaja.
 
Siku zote mbaya anaonekana ni mwanamke. Umetolea mfano wa baba majaliwa. Umemsikia aliposema aliondoka akaja dar kutafuta lakini hakuwa na ugomvi na mama majaliwa. Alipokua dar akaanzisha familia nyingine. Ila we umeona wa kupoint hapo ni mama majaliwa.

Umemtaja pia na baba yake ommy, ommy kazaliwa nje ya ndoa kama niliskia vizuri interview lakini baba yake alimtelekeza mazima, na hata msibani kwa mama ommy huyo mzee hakukanyaga, leo mzee analalamika vipi ommy kamkosea, wanaume hamuonagi shida zenu ila ni wanawake tu.

Nyie mnpoenda kuzaa nje mnataka mkirudi mwanamke aufyate akupigie magoti akulambe nyayo, makosa yenu huwa hamuyaoni ama ni kujitoa ufahamu?

Kama uliona kumuacha mama wa mwanao ni kumkomoa basi usirudi pindi mtoto atakapofanikiwa
 
Daaàah hivi unajua watoto wengi waliotelekezwa na baba zao ni watoto wa mpango kando, yaaaan wengi wao ni baba kamuongopea mwanamke.ommy dimpoz baba alikua ana familia teyari, diamond baba yake teyari alikua ana familia tena baba wote wawili,same to majaliwa.
Mmejaa lawama kwa wanawake eti ndo sababu.hamjiskii vibaya,hamuoni aibu kuwanyooshea vidole mama zenu kila siku.kuna mwanamke hapendi kuona watoto wake hawalelewi na wazaz wote??acheni utoto na kujitoa faham.sikia story za pande zote mbili ndo muanze kubwabwaja.
Kunywa soda crate zima ntalipa. Wanajitia ufahamu. Kwahiyo mwanaume akiwa mzinifu, akiwa anamtesa mwanamke huyo hana shida ila shida ni mwanamke. What is wrong with humans
 
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu
 
Nyumba nyingi wazazi wa kiume ama kina baba wanazikimbia na kuwaacha watoto kisa kikubwa inaonesha ni kina mama, hii ni baada kujitokeza mara nyingi wazazi wa kiume baada vijana wao kupata maendeleo flani mifano michache ni kama huyu kijana shujaa Majaliwa na watu maarufu kama dimpoz na diamond.

Kuna kitu kina mama huwa wanasababisha ambacho wazee wanaona Bora kukaa pembeni na kuwaacha watoto na mama yao ila bado anaondoka anawapenda watoto hali tu ya yule mama ndio inamkwaza.
Hufahamu Sisi Akina Baba baada ya kutimiza miaka 55 hutakiwi kukaa na mwanamke?, endapo kama unataka kuishi zaidi, endapo huyapendi maisha yako komaa kuishi naye!,
Wanawake wema ni 2/10.
#NOTE THIS KEENLY
 
Yani imefika hatua hadi wanaume tunatafuta sympathy. Hii ni aibu kubwa sana.

Ujana wako hujafanikiwa, uzeeni unakuja kusumbua jamii ikuonee huruma mwanao akusaidie!!

Hii ya kusema eti wanawake wanazingua sana hivyo unamwachia kila kitu hadi watoto kweeelii.??
Mfano huyo mzee wake majaliwa alimwachia kila kitu, kila kitu gani??, hao watoto kibao au kitu gani?

Aliezingua sio mtoto ni mama. Sasa kwanini umtelekeze mtoto sehemu usiyojua damu yako itaishije??

Ni mwanaume mpumbavu anaetelekeza damu yake kisa mwanamke.
 
Daaàah hivi unajua watoto wengi waliotelekezwa na baba zao ni watoto wa mpango kando, yaaaan wengi wao ni baba kamuongopea mwanamke.ommy dimpoz baba alikua ana familia teyari, diamond baba yake teyari alikua ana familia tena baba wote wawili,same to majaliwa.
Mmejaa lawama kwa wanawake eti ndo sababu.hamjiskii vibaya,hamuoni aibu kuwanyooshea vidole mama zenu kila siku.kuna mwanamke hapendi kuona watoto wake hawalelewi na wazaz wote??acheni utoto na kujitoa faham.sikia story za pande zote mbili ndo muanze kubwabwaja.
Siyo kila anayeandika hapa amesimuliwa
 
Yani imefika hatua hadi wanaume tunatafuta sympathy. Hii ni aibu kubwa sana.

Ujana wako hujafanikiwa, uzeeni unakuja kusumbua jamii ikuonee huruma mwanao akusaidie!!

Hii ya kusema eti wanawake wanazingua sana hivyo unamwachia kila kitu hadi watoto kweeelii.??
Mfano huyo mzee wake majaliwa alimwachia kila kitu, kila kitu gani??, hao watoto kibao au kitu gani?

Aliezingua sio mtoto ni mama. Sasa kwanini umtelekeze mtoto sehemu usiyojua damu yako itaishije??

Ni mwanaume mpumbavu anaetelekeza damu yake kisa mwanamke.
You seem less informed! Kitendo cha mwanaume kuacha mji wake ni kigumu mno. Hivyo ukiona mwanaume kaacha mji ujue limefika shingoni na busara ni kuondoka.

Vinginevyo ni kumdhuru mke au familia
 
Yani imefika hatua hadi wanaume tunatafuta sympathy. Hii ni aibu kubwa sana.

Ujana wako hujafanikiwa, uzeeni unakuja kusumbua jamii ikuonee huruma mwanao akusaidie!!

Hii ya kusema eti wanawake wanazingua sana hivyo unamwachia kila kitu hadi watoto kweeelii.??
Mfano huyo mzee wake majaliwa alimwachia kila kitu, kila kitu gani??, hao watoto kibao au kitu gani?

Aliezingua sio mtoto ni mama. Sasa kwanini umtelekeze mtoto sehemu usiyojua damu yako itaishije??

Ni mwanaume mpumbavu anaetelekeza damu yake kisa mwanamke.
Umezungumza ukweli "Tusitelekeze watoto kwa visa vya kina mama" Tuwalee watoto wetu kwa ukamilifu mpaka pale watakapoweza kujitegemea binafsi.,concentrates kwa watoto na si kwa mwanamke mkorofi na mzinzi.
 
Back
Top Bottom