Ujamaa ni sera ngumu sana kuipandikiza kwa watu wakaielewa. Ujamaa unahitaji kiongozi awe dikteta atumie nguvu kulazimisha watu wafanye vile anavyotaka yeye.
Mjomba wangu aliuawa na wanamgambo wa kijamaa baada ya kukataa kuhama katika eneo lake alilokuwa akiishi na familia yake ~kajijenga ana ng'ombe ,mbuzi ,kondoo, kuku ,Bata na kadhalika. Sheria ikamtaka akaungane na wanakijiji wenzie ili wauende Kijiji cha ujamaa, akakataa ,matokeo yake wale mgambo wakachoma nyumba zake na mabanda ya mifugo ili kumshinikiza ahamie kwenye Kijiji cha ujamaa, ukatokea ugomvi mkubwa sana ambao ulipelekea kifo chake.
Mnakwenda kulima mashamba ya ujamaa, matokeo yake Kuna majamaa miongoni mwenu ni mvivu ~ badala ya kuweka bidii kwenye kulima shambani yeye kazi yake kubwa ni kwenda kujisaidia Kila wakati. Katika hali kama hiyo ni nani atakuwa na Ari ya kujituma? Kumbuka mvuno yanakuwa Mali ya Kijiji.
Darasani; wewe unakesha unajisomea kiasi cha kuloweka miguu kwenye beseni la maji ili upate alama nzuri na matokeo mazuri, wakati huo huo roommate na classmate wako anakesha disko na night club. Mnafanya mtihani wewe unafaulu classmate wako anafeli ,kwakuwa ni ujamaa inabidi wewe umgawie alama zako ili walau muwe sawa. Ni nani njinga kiasi hiko kuwa ataendelea kukesha darasani ilhali anajua wazi fulani hajitumi halafu atagawana alama na anayejituma?
Hata kwa Mungu si kweli kwamba binadamu wote ni sawa. Ndio sababu Kuna waafrika, wazungu, wahindi, waarabu, warefu, wafupi, walemavu na kadhalika.
Ujamaa ni upuuzi ambao hautekelezeki. Hao wachina tumekaa nao Dar visa zao zilishaisha muda wa kuendelea kukaa hapa nchini lakini wanakuambia Tanzania ni nchi nzuri sana kuishi ukilinganisha na kwao simply kwasababu ya uhuru wa mtu binafsi