Nakumbuka kipindi kile Magufuli ndio ameingia madarakani akafuta sitting allowances, akaziba Ziba na mianya yote ya upigaji hasa ile ya mishaara hewa.Lakini pia nyakati hizi wizi na ubadhilifu vimekuwa jambo kijanja na ushindi kwa mtumishi wa umma......kiasi kwamba mtu akipata teuzi anaonekana ameula.......na akitumikia taifa kwa weledi na uaminifu mpaka akastaafu akiwa masikini anaoenekana bwege na kuchekwa.......
Lakini pia serikali yetu ina usimamizi na utaratibu mbovu kwa wastaafu waliowahi kumwaga jasho lao wakilipigania taifa hili........
Jasho lao la damu na la kizalendo wanakuja kulipwa matusi, kejeli na dharau na serikali yao waliyoipigania.....
Yote haya yanachochea wizi na ubadhilifu kwa watumishi waliopo kwenye nafasi nyeti na hata zisizo nyeti kwani hata wao wanayaona mateso, dhiki na dharau wanazofanyiwa wastaafu hivyo wanajilipa kabisa kwa kuiba na kuwekeza ili kuziepuka aibu za uzeeni ya kuomba kilichokuwa chako.....
Kuna watumishi baadhi waliachaga kazi na sababu waliyokuwa wanatoa eti serikalini Sasa Hivi hakuna maisha...
Yaani mbongo sehemu anayoajiriwa kama hakuna mianya ya wizi na ubadhirifu haijalishi analipwa mshaara kiasi gani yeye anakwambia sehemu hiyo Haina maisha... Na bahati mbaya sana hii imekuwa ni culture iliyokomaa