Nyumba ya Serikali yenye thamani ya Sh 1.2 bilioni yauzwa kwa mfanyabiashara kwa Milioni 130. Waziri Lukuvi alia na watendaji, amkabidhi DCI

Nyumba ya Serikali yenye thamani ya Sh 1.2 bilioni yauzwa kwa mfanyabiashara kwa Milioni 130. Waziri Lukuvi alia na watendaji, amkabidhi DCI

..Wizara ya ujenzi ndiyo waliopanga bei za hasara.

..Na Magufuli ndiyo alikuwa waziri wakati huo.
Kwanza kabisa muelewa wadau, ulikuwa ni uamuzi wa baraza la mawaziri. Alafu kila nyumba iliuzwa kulingana na thamani yake na eneo ilipo. Hizi nyumba mfano kule Mwanza Isamilo nyingi zilikuwa zimechakaa na hata zilikuwa zinavuja maana zilikuwa zimeezekwa kwa vigae. Alafu walipita wataalamu kufanya valuation ya kila nyumba ili kupanga bei. Kumhusisha mkuu na hili suala ni kumuonea tu. Wa kulaumiwa ni Sumaye ambae alikuwa waziri mkuu
 
Kuuza nyumba za serikali ulikuwa ni uamuzi wa Baraza la mawaziri!

..lakini ulitekelezwa na kusimamiwa na Magufuli.

..huwezi kuwa na kesi ya mauaji halafu ukasema the person who PULLED THE TRIGGER is not guilty because he is not the one who directed the killing.
 
..lakini ulitekelezwa na kusimamiwa na Magufuli.

..huwezi kuwa na kesi ya mauaji halafu ukasema the person who PULLED THE TRIGGER is not guilty because he is not the one who directed the killing.
Msimamizi mkuu alikuwa Lumbanga na mzee Sumaye!
 
Kwanza kabisa muelewa wadau.ulikuwa ni uamuzi wa baraza la mawaziri. Alafu kila nyumba iliuzwa kulingana na thamani yake na eneo ilipo. Hizi nyumba mfano kule mwanza isamilo nyingi zilikuwa zimechakaa na hata zilikuwa zinavuja maana zilikuwa zimeezekwa kwa vigae. Alafu walipita wataalamu kufanya valuation ya kila nyumba ili kupanga bei. Kumhusisha mkuu na hili suala ni kumuonea tu. Wa kulaumiwa ni Sumae ambae alikuwa waziri mkuu

..baraza la mawaziri hufikia uamuzi baada ya waziri anayehusika kuwasilisha pendekezo na kulijengea hoja.

..kama pendekezo halijatokea wizarani kwake, waziri anaweza kulipinga. Na akishindwa anatakiwa kujiuzulu.

..Waziri akienda kutekeleza maamuzi ya baraza maana yake anayaunga mkono. Na anakuwa amejifunga ikiwa utekelezaji wa maamuzi hayo utakuwa na madhara.

..Kwa hiyo Magufuli hawezi kukwepa lawama kwa ufisadi uliotokea ktk zoezi hili.

..Ukizingatia thamani ya nyumba + kiwanja utakubaliana na mimi kuwa Magufuli alifanya ufisadi.
 
Waziri wa ardhi mh Lukuvi amemtaka mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai kuwashughulikia watendaji wa NHC na NIC waliouza kifisadi nyumba mbili za Serikali kinyume cha utaratibu.

Naye DCI amemuhakikishia Waziri Lukuvi kuwa atalishughulikia swala hilo kwa haraka na kuhakikisha nyumba hizo mbilu zinarudi serikalini.

Source ITV habari!
Bado Waziri wa ujenzi awamu ya Mkapa ashitakiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..baraza la mawaziri hufikia uamuzi baada ya waziri anayehusika kuwasilisha pendekezo na kulijengea hoja.

..kama pendekezo halijatokea wizarani kwake, waziri anaweza kulipinga. Na akishindwa anatakiwa kujiuzulu.

..Waziri akienda kutekeleza maamuzi ya baraza maana yake anayaunga mkono. Na anakuwa amejifunga ikiwa utekelezaji wa maamuzi hayo utakuwa na madhara.

..Kwa hiyo Magufuli hawezi kukwepa lawama kwa ufisadi uliotokea ktk zoezi hili.

..Ukizingatia thamani ya nyumba + kiwanja utakubaliana na mimi kuwa Magufuli alifanya ufisadi.
Agizo la Rais ni sheria bwashee!
 
Safi Sana,huyu lukuvi anajitahidi Sana kwskweli

Huyu akigombea URAIS Nampa kura yangu.

Moja ya mawaziri makini na hodari sana.

Nimwelevu, anahekima pia busara...
Yaani anaelewa kutenda kwa haki.
 
Mada ni nyumba za serikali zilizouzwa kifisadi. Nadhani yupo mule mule! , ,[emoji56][emoji56][emoji56]

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaa. Jamaa anafikiri wadau wanajadili nje ya box kumbe wapo mlemle ilhali yeye alizungushia wigo wa makuti na jamaa wamechana nyavu mpaka kufukua makaburi. Sometimes tuwe tunaangalia na mada za kuleta otherwise upepo utatubadilikia. Na tukiwanyooshea vidole wenzetu tujiulize vile vinavyobaki vinamwelekea nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli aliuza nyumba zingine kwa laki mbili moja alimkabidhi mdogo wake.

Acheni kunyanyasa watumishi wakati mwizi yuko ikulu.

Tupeni maelezo na mapato ya nyumba zote mlizogawana na kuzigawa kwa bei ya kutupa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom