Nyumba za 60m zinaweza kuleta 2m kila mwezi kama kodi?

factor kubwa ya kupanga nyumba kwa kodi kubwa ni location.

milioni 60 ukijenga vyumba master maeneo ya kurasini, sinza, ubungo, mwenge, kinondoni una uwezo wa kupata kodi zaidi ya milioni 3 kwa mwezi.

sababu kuu ni location ina wateja wengi
Sasa hayo maeneo kiwanja unakipataje bila kuwa na million 300?
 
Anachukulia simple sana😂 kijana anawaza apate 20k akagonge malaya na kunywa visungura. Mtaumizana vichwa tu. Bajaji mpe mtu mzima mwenye majukumu utaipenda.
 
Sasa hapo kuvunja maana yake si lazma uwalipishe uharibifu. Bila hivyo utafanya biashara kichaa tu
 
Hardware ya 60M ikupe 100k as profit kwa siku na kwa mwenzi jumla M3 hamna hamna M2 ......utani huu.
Kwenye hardware faida ya 100k inawezekana hasa ukiiiweka kwenye maeneo ya saiti watu wanapojenga.
Bidhaa za kwenye hardware faida yake ni kubwa sana ukipata sehemu yenye mzunguko mzuri laki 1 kwa siku ni hela ndogo sana
 
Sasa hapo kuvunja maana yake si lazma uwalipishe uharibifu. Bila hivyo utafanya biashara kichaa tu
Kwahiyo uko zako Mbezi kila aliyekodi Airbnb yako akiondoka Bunju unaenda kagua sinki na vyoo kama havijaziba. Kifaa kikiharibika hata huoni kirahisi, au aki-abuse vifaa mfano umeweka maji anafungulia mpaka mwisho au kaja amelewa anaacha yanamwagika.

Ni sawa na kugawa gari lako hovyo kwa mikono tofauti ukiamini kila atakayerudisha utakagua. Subiri majibu kwenye maintenance cost
 
Ritani ya real estate bongo ipo chini sana labda kama upo kwenye "prime area" au uwe eneo la biashara kama hizi frames barabarani tofauti na hapo pesa huwa inarudi kuanzia miaka 10 huko yaani 10% kwa mwaka, (Duniani kote average return on investment kwenye real estate is 8 to 10%).

Maana yake nyumba ya 60m utapata maximum ya 6m kwa mwaka ambayo ni 500k kwa mwezi. Haina tofauti na UTT.

Ila kama una mtaji mkubwa na unazo nyingi sio tatizo maana ni low risk investment isiyo na usumbufu ila sio ya kukupa faida kubwa Inasaidia pia kukuza mtaji unaweza kukopea ukaongeza nyingine.
 
Jenga danguro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…