Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,914
- 168,320
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linaendelea na uchunguzi wa tukio la moto lililotokea Julai 29, 2026 majira ya saa 7:35 mchana katika nyumba za Polisi Msambweni zilizopo eneo la Mapinduzi “A”, Kata ya Ngamiani Kusini, Wilaya ya Tanga.
Moto huo umeteketeza baadhi ya mali zilizokuwa ndani ya nyumba hizo, huku thamani ya mali zilizoharibika ikiwa bado haijafahamika. Juhudi za kuuzima zilifanyika kwa ushirikiano kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Polisi pamoja na wananchi.
Jeshi la Polisi limesema hakuna madhara yoyote kwa binadamu yaliyoripotiwa kutokana na tukio hilo, huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha moto huo.