Nyumba za Polisi zateketea kwa moto Tanga

Nyumba za Polisi zateketea kwa moto Tanga

Hao wananchi walioenda kuzima moto ilitakiwa wachapwe viboko 6 asubuhi mchana na jioni siku nyengine waache kuingilia kazi za kipuuzi
 
Polisi sio binadamu wa kawaida..
hapo kuna mtu watamwangushia kesi ya ugaidi ya kuchoma vibanda vyao!
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linaendelea na uchunguzi wa tukio la moto lililotokea Julai 29, 2026 majira ya saa 7:35 mchana katika nyumba za Polisi Msambweni zilizopo eneo la Mapinduzi “A”, Kata ya Ngamiani Kusini, Wilaya ya Tanga.

Moto huo umeteketeza baadhi ya mali zilizokuwa ndani ya nyumba hizo, huku thamani ya mali zilizoharibika ikiwa bado haijafahamika. Juhudi za kuuzima zilifanyika kwa ushirikiano kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Polisi pamoja na wananchi.

Jeshi la Polisi limesema hakuna madhara yoyote kwa binadamu yaliyoripotiwa kutokana na tukio hilo, huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha moto huo.
Miaka ya nyuma polisi wakienda likizo walikuwa wanaacha taa za nyumba zao zinawaka(hazizimwi).Baadaye wakafungiwa mita.pia kulikuwa na tabia baadhi yao walikuwa hawachomoi majiko yao kwenye swichi za umeme.inawrzekana ikawa ndo chanzo cha tukio hili.
Pameshauzwa ukiona hivyo
 
Mungu ni mwema wakati wote. Amen 🙏
Kazi ni kipimo cha utu
 
Itabidi wahamishiwe mbweni Kwa muda.
 
Back
Top Bottom