Nyumba za Polisi zateketea kwa moto Tanga

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linaendelea na uchunguzi wa tukio la moto lililotokea Julai 29, 2026 majira ya saa 7:35 mchana katika nyumba za Polisi Msambweni zilizopo eneo la Mapinduzi “A”, Kata ya Ngamiani Kusini, Wilaya ya Tanga.

Moto huo umeteketeza baadhi ya mali zilizokuwa ndani ya nyumba hizo, huku thamani ya mali zilizoharibika ikiwa bado haijafahamika. Juhudi za kuuzima zilifanyika kwa ushirikiano kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Polisi pamoja na wananchi.

Jeshi la Polisi limesema hakuna madhara yoyote kwa binadamu yaliyoripotiwa kutokana na tukio hilo, huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha moto huo.
Kuna polisi mwenzao amewafanyia ugaidi
 
Ngoja ninyamaze tuu ,maana hapo njee imepita hardtop yenye namba za caterpillar...
 
Huu uzi ni misleading hizo sio nyumba za Polisi hayo ni Mabanda, Nyumba za Polisi i believe zipo barabara ya Mwai Kibaki karibu na Tanesco Kinondoni.
 
Back
Top Bottom