Nywele zinavyohusishwa na roho na mapepo

Nywele zinavyohusishwa na roho na mapepo

Mimi ninacho shauri mabint mnaotaka kupendeza na hizo human hair; muwe mnaziombea; mnazitakasa; wale christian wananielewa zaidi; lakin neno linasema; huwez kuuteka mji au ufalme had umfunge yule mwenye nguvu; swali langu lipo hapa; je wewe una nguvu ndani yako ya kumfunga huyo mwenye nguvu? Sababu ufalme wa Mugu unapatikana kwa nguvu na wenye nguvu ndio wanao uteka; hivyo bas tutafute nguvu kwa Mungu ili tuweze kumfunga huyo ibilisi na nguvu zake ili sisi tuweze kumiliki. Tuna Damu ya Yesu iliyo pamoja nasi; ( narud baadaye)
 
Jambo gani jipya? Hujasikia mcheza mpira anajitayarishakwa mazoezi anakaa kambi?
 
Hivi dhamira kuu haswa ya wachawi kuchukua nywele, wanaroga nini hasa, ili uwe zezeta kwa kuchukua akili ama ni nini hasa nifungue nielewe mshana jr
 
Mshana Jr, kuna ukweli mtupu kwenye mada hii wachawi wengi huanza kuroga kichwa ambacho hubeba nywele kisha anafumua viungo vingine
 
Hivi dhamira kuu haswa ya wachawi kuchukua nywele, wanaroga nini hasa, ili uwe zezeta kwa kuchukua akili ama ni nini hasa nifungue nielewe mshana jr
Mchawi kamwe hana dhamira njema chochote atakachokifanya kwako ni kibaya na chenye nia na matokeo mabaya
 
Kuna mambo ya kushangaza ambayo kwasababu ileile ya kimapokeo na mazoea huwa hatuyahoji au hatuna muda wa kufuatilia na pengine tunaridhika tu na hivyo yalivyo.

Nywele hizi zetu za kichwani zinabeba siri kubwa ambayo ina mawasiliano ya moja kwa moja na kuzimu au na roho zinazotangatanga.

Hebu tujihoji haya;

- Kwanini baadhi ya imani ni marufuku na hairuhusiwi kwa mwanamke kuonyesha nywele zake hadharani?
- Kwanini mchawi/mwanga anapokamatwa hukatwa nywele zote ili kummaliza nguvu zake?
- Kwanini chizi kichaa au mwendawazimu hunyolewa nywele kama sehemu ya tiba?
- Kwanini wachawi na waganga wengi hutumia nywele kama sehemu ya uchawi/ulozi wao?

Historia ya nywele kuhusiana na roho na nguvu za kiza inaanzia mbali sana miaka elfu nyingi iliyopita kwenye habari za Biblia takatifu kisa cha Samsoni na Delilah pale Mwenyezi Mungu alipoweka nguvu isiyomithilika kwenye nywele za Samsoni lakini shetani kupitia Delilah alimrubuni Samsoni na Samsoni akatoa siri ya nguvu zake.

Ni kutoka hapo ile nguvu ya kimungu iliyowekwa kwenye nywele za Samsoni iligeuka na kuwa nguvu ya kishetani na kufanya maangamizi makubwa, tangu hapo nywele imekuwa ni kitu kinachohusishwa na roho chafu na mapepo.

Mkuu kipindi cha nyuma niliwahi kuamka asubuhi nimenyolewa nywele kidogo, na wengi tu walikuwa wanaamka asubuhi na kukuta wamenyolewa kiduara, na wengine zilikuwa zikichukua muda sana kuota! Inamaanisha nn hiyo?
 
Mkuu kipindi cha nyuma niliwahi kuamka asubuhi nimenyolewa nywele kidogo, na wengi tu walikuwa wanaamka asubuhi na kukuta wamenyolewa kiduara, na wengine zilikuwa zikichukua muda sana kuota! Inamaanisha nn hiyo?
Ukinyolewa na hakuna madhara yanayotokea ujue nywele zako zimechukuliwa kama malighafi ya kwenda kuumiza wengine
Kuchelewa kuota Inategemea mnyoaji alitumia nini kukunyoa kwakuwa wengine hukwangua mpaka ngozi kulingana na mahitaji na pia hutumia madawa ya kishirikina
 
1466622259096.jpg
 
Chuo nilichosoma mimi hatukuruhusiwa kufuga nywele na tulikuwa tunanyoa kwa mwezi mara mbili na ilikuwa imo kwenye ratiba ya chuo na haikuwezekana usinyoe unaweza hata kufukuzwa chuo ukikaidi

Mnanyoa nywele za wapi?fafanuwa
 
Back
Top Bottom