Pre GE2025 Nzega, Tabora: Mtaani kwetu kuna watu wanapita Kila kaya wanagawa mitungi ya gesi, Sharti lao uwape namba yako ya NIDA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hapo na mim ndio sijaelewa.. wataalam watueleweshe ukishagawa taarifa zako Nini kitatokea?
Wanaenda kufyatua kitambulisho cha kupigia kura na kura yako itapigwa tu sehemu. Wakuu mnakuwa kama hamjasoma shule ?. Ukimpa mtu namba zako za nida si unakuwa umempa detail zako zote..kaeni kitaalam
 
Labda hao Wahusika wangetoa elimu ya kwa nini wanahitaji hiyo namba.
 
Ukishaonq rushwa inatolewa kwa uwazi namna hii ujue taifa lipo hoi kabisa
 
Wewe na wao ni wale wale unachokitetea unakijua
Hivi hata kusoma unajua ?!!! Moja kama issue ni namba ya NIDA tu unaweza ukazipata namba za NIDA bila muhusika kukupa.., Issue ya kugawa Mitungi ya Gesi nimekuwa nikilaumu tangia enzi na enzi..., Kwanini Serikali ihangaike kugawa mitungi ya gesi ili watu wapikie gesi kijijini wakati ni gharama na gesi hio wala sio yetu tunaagiza ?

Now huenda ni kweli ninachokisema ninakijua (sio kukitetea) ila wewe unacholaumu haujui impact yake ukubwa wake na impact yake sio uchaguzi bali ni kududumiza maisha ya raia na upuuzi huo haujaanza leo wala juzi sababu kuna kipindi hata waziri wa Nishati aligeuka dalali wa gesi...
 
Mi waniletee
 
Sawa boss
 
Labda hao Wahusika wangetoa elimu ya kwa nini wanahitaji hiyo namba.
Wanakwambia ukiwapa namba ya nida tayari umewapgia kura, Mimi sijui inawezekanaje hiyo
 
Kuna watu wanakula pesa za Samia bila huruma.
 
Wanaenda kufyatua kitambulisho cha kupigia kura na kura yako itapigwa tu sehemu. Wakuu mnakuwa kama hamjasoma shule ?. Ukimpa mtu namba zako za nida si unakuwa umempa detail zako zote..kaeni kitaalam
Pia na Mimi najua hivyo ss Kuna member hapo juu wanapayuka payuka wanadhani watanzania wote wajinga
 
sio kura bro bali ni uthibitisho wa takwimu kuwa gesi imewafikia watu na haikutapeliwa
 
Kumekucha😅😅😅
 
Pia na Mimi najua hivyo ss Kuna member hapo juu wanapayuka payuka wanadhani watanzania wote wajinga
Hii nchi sababu ya umasikini watu wanaamua kuuza utu wao na vitu kama hivyo...mfano kugawiwa mitungi ni dhahiri kabisa kwamba Sisi ni masikini ila sisi hawa hawa nakuja kiongozi na akasema sisi ni matajiri sisi hawa hawa tunapiga vigeregere...Watu wa Ajabu sana
 
Wanaenda kufyatua kitambulisho cha kupigia kura na kura yako itapigwa tu sehemu. Wakuu mnakuwa kama hamjasoma shule ?. Ukimpa mtu namba zako za nida si unakuwa umempa detail zako zote..kaeni kitaalam
Hao wagawa mitungi ili wapate Namba za NIDA (kama ni namba Pekee) Ndio hawajasoma sababu kupata namba tu rahisi sana wewe nenda kwa wasajili simu au stationary wanaofanyia watu Loss Reports let alone namba za NIDA hadi kuna wakati mtu anampa kitambulisho ili achukue information za kuzinfanyia Kazi..., Namba yako is not meant to be a Secret bali ni kama Utambulisho katika Sehemu tofauti tofauti...

Sasa kama Namba pekee ndio inapiga Kura; Issue sio kwa wanaochukua au kutoa pekee bali mfumo mzima ni mundelezo wa Maigizo... Na kama nilivyosema huko Awali...

Duh, mkuu we chukua tu, Bora ni halali. Maana kura hautapiga Kwa kutumia NIDA, kura si Kuna kitambulisho Cha kupigia kura. Kura ni Siri Yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…