Kwa watu waliobobea kwenye mambo ya matangazo na uhamasishaji, utengenezaji wa tangazo la kiuhamasishaji kila kitu huzingatiwa kwa makini Sana
CCM wametoa bango lao la kuhamasisha watu wapige kura kwenye uchaguzi wa Oktoba 2025 wenye kila dalili kuwa watanzania wenye akili timamu hawatashiriki.
Kwenye bango hilo kuna picha ya mwanamke kwenye herufi "O" ambayo bila ya shaka inaashiria ilikusudiwa iwe ya mgombea wa CCM kwenye uchaguzi huo usioaminika unaopigiwa chapuo na CCM, Samia Suluhu Hassan.
Lakini nimewaza ni kwa nini CCM wameweka picha ya mgombea wao kwenye herufi "O" badala ya labda kuitanguliza au kuiweka mbele ya kauli mbiu yao?
Wanaojua historia ya uandishi labda wanaweza kutuambia ni kwa nini herufi "O" inafanana kimaumbile na tarakimu sifuri "0".
👇
View attachment 3361037