Asalam Aleykum wapenzi wana JF,
Wakati nafuatilia mchakato wa kumpigia chapuo Raila Odinga ili awe Mwenyekiti wa umoja wa Afrika, Mh. Ruto alifanya hafla na kuwaalika viongozi mbali wa Kiafrika pamoja na viongozi wastaafu.
Mmoja wao alikuwa Rais mstaafu wa Nigeria, Mh. Obasanjo ambaye alipoalikwa kutoa salamu alinishangaza kwa mambo mawili;
Kwanza ni kitendo chake cha kutoa "kirefushaji" na kuwananga waliomwekea kwa kusema, "I am not as short as you think I am."
Pili ni pale alipomtupia "kijembe" Mh. Kikwete kwa kusema, wakati anaingia alitaka akae kwenye "Bendera". Lakini yeye (Mh. Obasanjo), akamwambia " You are now a man without flag"!
Hili kwa kweli binafsi limeniacha na maswali mengi sana.
Mh. Obasanjo hapa alitaka kufikisha ujumbe gani kwa Mh. Rais msitaafu?