Ofa: Kesho nitaombea wote wenye uhitaji wa kuombewa. Kama wewe ni mmoja wapo jiunge nami

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Anaandika; Robert Heriel
Kuhani Katika Hekalu Jeusi.

Kesho ni mwisho wa Mwaka. Kuanzia majira ya 12:00 - 4:00 Usiku nitautumia muda huo kuombea watu wote wenye kuhitaji msaada wa KUOMBEWA.

Nafahamu sio Watu wote wanaoamini kwenye mambo ya maombi. Nawaelewa Watu wa Aina hiyo. Maombi haya ni Kwa wale wanahitaji msaada wa nguvu zisizoonekana, wanaohitaji Mvuto na bahati, wanaohitaji connection kwani Hawana connection.

Maombi haya yatawahusu wale wote wanaohitaji MUDA WAO WA SIKU ZIJAZO KUHIFADHIWA NA KULINDWA VYEMA.

Maombi haya yatahusu, wale wote wanaohitaji Mahusiano yenye furaha, na hapa nazungumzia mahusiano ya familia na yakindugu, pamoja na mahusiano kazini.

Maombi haya yatahusu, wale wote wanaohitaji kutumikia muda wao hapa duniani, wasio na kazi wapate kazi.

Maombi haya yatahusu wale wote waliopo katika mikondo mibaya ya Maisha na walioharibiwa njia zao za Maisha, au wamejiharibu wao wenyewe.

Maombi haya yatahusu kwale wote wanaotamani kuwa Wakweli, wenye Haki na wenye Upendo. Maombi haya yatafanya kazi Kwa kuzingatia Ukweli, Haki na Upendo.

Ikiwa wewe ni mmoja wapo, hutokuwa na haja ya kunitajia majina yako. Utasema tuu nipo tayari kuwa mkweli, mwenye upendo na HAKI.

Ni KESHO jioni.
Taikon atakuwa katika Hekalu kuombea Watu.
Hakuna cha sadaka wala dhabihu.

Sadaka na dhabihu utaitoa BAADA ya kufanikisha ombi na haja zako kujibiwa.
Kuwatumikia Watu Kwa Ukweli, Haki na Upendo hiyo ndio Sadaka na dhabihu.

Maombi yataelekezwa Kwa Mungu Mkuu muumba WA mbingu na Nchi. Kupitia majina yake matakatifu ambayo hatuyajui kama tusivyomjua yeye.

Maombi yatajibiwa na mamlaka zote za Mungu bila kujali ni njema au Mbaya kulingana na mtazamo wetu. Hivyo BAADA YA maombi itatupasa kuishi na kila MTU anayetuzunguka Kwa upendo, Haki na kweli.

Nawakaribisha!

Nawatakia maandalizo Mema ya SABATO
 
Duh kumbe kesho ndo mwisho wa mwaka..mungu atuepushe tukae salama wengi walishindwa kumaliza mwaka kawawa alikufa siku kama ya leo
 
Kesho kanisani nitakesha pia nitasali na wewe Robert nikimaliza ibada kanisani naendelea na maombi na wewe robert
 
Maombi ni upuuzi tu kama upuuzi mwingine, hakunaga kitu kama kuombewa.
 
Anaandika; Robert Heriel
Kuhani Katika Hekalu Jeusi.

Kesho ni mwisho wa Mwaka. Kuanzia majira ya 12:00 - 4:00 Usiku nitautumia muda huo kuombea watu wote wenye kuhitaji msaada wa KUOMBEWA.

Nafahamu sio Watu wote wanaoamini kwenye mambo ya maombi. Nawaelewa Watu wa Aina hiyo. Maombi haya ni Kwa wale wanahitaji msaada wa nguvu zisizoonekana, wanaohitaji Mvuto na bahati, wanaohitaji connection kwani Hawana connection.

Maombi haya yatawahusu wale wote wanaohitaji MUDA WAO WA SIKU ZIJAZO KUHIFADHIWA NA KULINDWA VYEMA.

Maombi haya yatahusu, wale wote wanaohitaji Mahusiano yenye furaha, na hapa nazungumzia mahusiano ya familia na yakindugu, pamoja na mahusiano kazini.

Maombi haya yatahusu, wale wote wanaohitaji kutumikia muda wao hapa duniani, wasio na kazi wapate kazi.

Maombi haya yatahusu wale wote waliopo katika mikondo mibaya ya Maisha na walioharibiwa njia zao za Maisha, au wamejiharibu wao wenyewe.

Maombi haya yatahusu kwale wote wanaotamani kuwa Wakweli, wenye Haki na wenye Upendo. Maombi haya yatafanya kazi Kwa kuzingatia Ukweli, Haki na Upendo.

Ikiwa wewe ni mmoja wapo, hutokuwa na haja ya kunitajia majina yako. Utasema tuu nipo tayari kuwa mkweli, mwenye upendo na HAKI.

Ni KESHO jioni.
Taikon atakuwa katika Hekalu kuombea Watu.
Hakuna cha sadaka wala dhabihu.

Sadaka na dhabihu utaitoa BAADA ya kufanikisha ombi na haja zako kujibiwa.
Kuwatumikia Watu Kwa Ukweli, Haki na Upendo hiyo ndio Sadaka na dhabihu.

Maombi yataelekezwa Kwa Mungu Mkuu muumba WA mbingu na Nchi. Kupitia majina yake matakatifu ambayo hatuyajui kama tusivyomjua yeye.

Maombi yatajibiwa na mamlaka zote za Mungu bila kujali ni njema au Mbaya kulingana na mtazamo wetu. Hivyo BAADA YA maombi itatupasa kuishi na kila MTU anayetuzunguka Kwa upendo, Haki na kweli.

Nawakaribisha!

Nawatakia maandalizo Mema ya SABATO
Kuhani Katika hekalu jeusi!!

Hapo tu!

Kwanini sio jeupe!!?
 
Back
Top Bottom