Nguva Jike
JF-Expert Member
- Jan 22, 2018
- 1,292
- 1,867
Ofisa mmoja wa benki inayoanzia na herufi A avunjwa mkono wa kulia na mtumishi wa kada ya ualimu.Tukio hilo limetokea jana asubuhi wilayani Kilindi ndani ya ofisi ya benki hiyo jina linahifadhiwa.
Vurugu hiyo ilitokana na mwalimu huyo kuwalalamikia benki hiyo kushindwa kuondoa makato ya mkopo ambao tayari mwalimu huyo ameshalipa na hana deni tena katika benki hiyo.
"Ni mwezi wa pili huu Sina deni kwao na makato bado yanaonekana kwenye mfumo wa ESS na Leo hii nimefika kwenye ofisi zao Kwa mara ya Saba na huyu ofisa hanipi maelezo ya kuridhisha na akadhihaki kada yangu nikaghadhibika nikamvunja mkono wa kulia bahati mbaya katika majibizano".Aliongea mwalimu huyo akiwa chini ya ulinzi.
Ofisa huyo anapatiwa huduma ya kwanza huku wakimuandaa Kwa rufaa hospitali ya mkoa kwakuwa mkono umevunjika juu ya bega unaning'inia kabisa.
Mwalimu amehojiwa na amesema anajutia kitendo alichofanya lakini anasema ameghadhibika sana kitendo kilichopelekea afanye tukio hilo BAYA.