Ofisa wa benki avunjwa mkono na mtumishi ndani ya benki wilayani Kilindi

Daa mwalimu ndo basi tena kazi itaota nyasi
Sio rahisi kiasi hivyo ,kuna vyama vya walimu hapo ndipo utaona umuhimu wake ...Bank pale Ngamiani nilishawahi kuzinguana na jamaa ,mwaka jana ,kipind kile watu wanaenda pesa unakuta wameramba ...Yule mother pale ni meneja ,nilimuwakia mpaka wlinzi walijaa pale. sababu nilikuta mil 2 haipo na nikiomba statement inaishia nusu.
 
Ofisa mmoja wa benki inayoanzia na herufi A avunjwa mkono wa kulia na mtumishi wa kada ya ualimu.Tukio hilo limetokea jana asubuhi wilayani Kilindi ndani ya ofisi ya benki hiyo jina linahifadhiwa.

Vurugu hiyo ilitokana na mwalimu huyo kuwalalamikia benki hiyo kushindwa kuondoa makato ya mkopo ambao tayari mwalimu huyo ameshalipa na hana deni tena katika benki hiyo.

"Ni mwezi wa pili huu Sina deni kwao na makato bado yanaonekana kwenye mfumo wa ESS na Leo hii nimefika kwenye ofisi zao Kwa mara ya Saba na huyu ofisa hanipi maelezo ya kuridhisha na akadhihaki kada yangu nikaghadhibika nikamvunja mkono wa kulia bahati mbaya katika majibizano".Aliongea mwalimu huyo akiwa chini ya ulinzi.

Ofisa huyo anapatiwa huduma ya kwanza huku wakimuandaa Kwa rufaa hospitali ya mkoa kwakuwa mkono umevunjika juu ya bega unaning'inia kabisa.

Mwalimu amehojiwa na amesema anajutia kitendo alichofanya lakini anasema ameghadhibika sana kitendo kilichopelekea afanye tukio hilo BAYA.
Anafanya fujo ofisini kwa watu then anasingizia kada yake ili kuonewa huruma. Ualimu umekuwa kama ulemavu kutafuta sympathy ya jamii. Wampeleke mahakani tu.
 
Ofisa mmoja wa benki inayoanzia na herufi A avunjwa mkono wa kulia na mtumishi wa kada ya ualimu.Tukio hilo limetokea jana asubuhi wilayani Kilindi ndani ya ofisi ya benki hiyo jina linahifadhiwa.

Vurugu hiyo ilitokana na mwalimu huyo kuwalalamikia benki hiyo kushindwa kuondoa makato ya mkopo ambao tayari mwalimu huyo ameshalipa na hana deni tena katika benki hiyo.

"Ni mwezi wa pili huu Sina deni kwao na makato bado yanaonekana kwenye mfumo wa ESS na Leo hii nimefika kwenye ofisi zao Kwa mara ya Saba na huyu ofisa hanipi maelezo ya kuridhisha na akadhihaki kada yangu nikaghadhibika nikamvunja mkono wa kulia bahati mbaya katika majibizano".Aliongea mwalimu huyo akiwa chini ya ulinzi.

Ofisa huyo anapatiwa huduma ya kwanza huku wakimuandaa Kwa rufaa hospitali ya mkoa kwakuwa mkono umevunjika juu ya bega unaning'inia kabisa.

Mwalimu amehojiwa na amesema anajutia kitendo alichofanya lakini anasema ameghadhibika sana kitendo kilichopelekea afanye tukio hilo BAYA.
Hata angeuwa kesi yake ingekuwa kuuwa bila kukusudia " Waalimu wanapuuzwa sana ikabidi aondoke na mkono wa mtu.
 
Kesi ngumu hii, kwa kuwa ni nje ya kituo chake cha kazi, labda malalamiko ya kimaandishi yaanzie bank, yaende kwa muajiri, na muajiri aangalie kama kuna kifungu cha kutoa adhabu, vinginevyo mahakama itabidi iingilie.​
Suluhu ni ofisa wa benki kusamehe.Watu wamevurugwa mbaya-mbovu sababu ya uchumi duni.Mola amuepushe na kikombe hicho ndugu mwalimu.
 
Ilitakiwa iwe automatic maana si kiasi kinaonekana kilichobaki. Mi nilidhani mwajiri na hazina ndio wanastopisha!

Kwa hiyo nisipolalamika watakata mpaka wakati mkataba umeisha. Hiyo ingeishia tu kwa mwajiri kustopisha makato
 
Back
Top Bottom