Nguva Jike
JF-Expert Member
- Jan 22, 2018
- 1,292
- 1,867
Hivi ni benki ndo wanaondoa Makato?
Ticha alienda kwa mahesabu kuanzia siku anajaza ombi la mkopo.Lakini,nao hao benki,kwa nini wanampuuzia mtu amewafuata mara saba/kwa zaidi ya miezi miwili hawashughulikii changamoto moja tu?Na wenyewe wamekuwa kama vijitaasisi vya Beipongo,Fanikwama na vicoba vingine?Hivi ni benki ndo wanaondoa Makato?
Ni ngumuDaa mwalimu ndo basi tena kazi itaota nyasi
Source imeelezwa ndugu sio mahusianoMambo ya pesa ama mahusiano.... si kingine
Yeah ,wanastopisha ila unapewa clearance kutoka bank kwenda kwa mwajiri wao...Wana mtindo wa kuendelea kukata kama hutowaambia ,na ukienda watakuambia wanarudisha ,hapo subiria miezi na mwezi unaofuata wanakata tena ..Mfumo hauko automatic.Hivi ni benki ndo wanaondoa Makato?
Tumuombee dua njema asiharibikiwe.Shida hazina huruma.Shida k......o!Daa mwalimu ndo basi tena kazi itaota nyasi
Hukigazabika kina nyakati unafanya maamuzi magumu👊 bila kuwaza after😎Ofisa mmoja wa benki inayoanzia na herufi A avunjwa mkono wa kulia na mtumishi wa kada ya ualimu.Tukio hilo limetokea jana asubuhi wilayani Kilindi ndani ya ofisi ya benki hiyo jina linahifadhiwa.
Vurugu hiyo ilitokana na mwalimu huyo kuwalalamikia benki hiyo kushindwa kuondoa makato ya mkopo ambao tayari mwalimu huyo ameshalipa na hana deni tena katika benki hiyo.
"Ni mwezi wa pili huu Sina deni kwao na makato bado yanaonekana kwenye mfumo wa ESS na Leo hii nimefika kwenye ofisi zao Kwa mara ya Saba na huyu ofisa hanipi maelezo ya kuridhisha na akadhihaki kada yangu nikaghadhibika nikamvunja mkono wa kulia bahati mbaya katika majibizano".Aliongea mwalimu huyo akiwa chini ya ulinzi.
Ofisa huyo anapatiwa huduma ya kwanza huku wakimuandaa Kwa rufaa hospitali ya mkoa kwakuwa mkono umevunjika juu ya bega unaning'inia kabisa.
Mwalimu amehojiwa na amesema anajutia kitendo alichofanya lakini anasema ameghadhibika sana kitendo kilichopelekea afanye tukio hilo BAYA.