Ofisi ya DED kuchunguza madai ya Walimu kukwepa majukumu ya kufundisha katika Shule ya Msingi Kishangazi (Tanga)

Ofisi ya DED kuchunguza madai ya Walimu kukwepa majukumu ya kufundisha katika Shule ya Msingi Kishangazi (Tanga)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Lushoto.jpg

TAARIFA KWA UMMA​
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuari ya Wilaya ya Lushoto imeona taarifa iliyotolewa katika Mtandao wa kijamii wa JamiiForums ikieleza kwamba katika Shule ya Msingi Kishangazi, iliyopo Kijiji cha Kishangazi, Kata ya Shagayu ni Mwalimu Mmoja tu ndiyo anafika shuleni kufundisha huku wengine wakionekana mitaani wakizunguka.

Hoja ilianzia hapa ~ Shule ya Msingi Kishangazi (Tanga) ina Mwalimu mmoja, wengine wanashinda tu mtaani

Kufuatia taarifa hiyo Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kupitia Idara ya Elimu Awali na Msingi imeanza kufanya ufuatiliaji ili kutambua kiini cha tatizo. Iwapo itabainika kuna mtumishi yoyote ambaye hatekelezi wajibu wake hatua za kinidhamu na kisheria zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria na miongozo ya utumishi wa umma.

Aidha, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji inatoa wito kwa wananchi wa Lushoto kuwasilisha kero kupitia Ofisi za Vijiji na Kata zao, ikiwa watakosa ushirikiano wafike Halmashauri kwa msaada zaidi au wanaweza kuwasiliana kwa mawasiliano yafuatayo; Simu namba: 027-2977216/ 027-297721, Barua pepe: [email protected], au barua ya kawaida kwa sanduku la Posta 32, Lushoto, au kuwasiliana moja kwa moja na Mkurugenzi Mtendaji kwa namba ya simu 0755-723 374.

Ili kuendelea kuwafikia wananchi na kutatua kero zao, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuari ya Wilaya ya Lushoto imeitenga siku ya Jumatano ya kila wiki kama siku maalum ya kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi ambapo kupitia ratiba maalum Timu ya Wataalam itapita Kata hadi Kata kwa lengo la kusikikiliza na kutatua kero za wananchi.

Imetolewa na:
Selemani S. Selemani
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
 
Back
Top Bottom