Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi mna mpango gani wa kulipa mapunjo ya mishahara kwa watumishi waliopanda vyeo 2015 , Mimi binafsi ni muathirika wa hiyo kadhia, ulienda halmashauri maafisa utumishi wanakuonesha kwenye mfumo kuwa walishashughulikia imebaki Tamisemi, miaka 10 sasa!Pole sana kwa changamoto hii tafadhali naomba utume raarifa za kutosha ili tuweze kufuatilia suala hili
Kipi kitakachonijuza Kuwa ametuma au la taarifa zangu?.na ziliwasilishwa na Katibu Tawala Mkoa wako
Habar za leo ,nikuulizen kuhusu vyeo vya mserereko lakin hamjibu kabisa,Sasa changamoto ni nini?Ndugu wana JamiiForums,
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), kupitia thread hii, tutapokea Maoni, Ushauri, Malalamiko, Mapendekezo yako Mwananchi. Tunakuhakikishia kuchukua hatua stahiki kwa haraka zaidi kwa kile utakachokiwasilisha kwetu.
Ikumbukwe kuwa tangu Mwaka 1961 hadi sasa Ofisi ya Rais –TAMISEMI imekuwa ni Wizara inayojitegemea na madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka Madaraka kwa Wananchi ambapo chimbuko lake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 Sura ya 8, Ibara ya 145 na 146.
Hadi sasa Nchi ina Mikoa 26, Wilaya 139, Halmashauri 184, Tarafa 570, Kata 3,956, Vijiji 12,319, Vitongoji 64,361 pamoja na Mitaa 4,263.
Majukumu ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI
yanatekelezwa katika ngazi ya Makao Makuu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia Hati ya Rais ya Mgawanyo wa Majukumu (Presidential Instrument) iliyotolewa na Rais Mei 2021, majukumu ya OR-TAMISEMI ni pamoja na:-
i) Kuratibu utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Mijini na Vijijini na Upelekaji wa Madaraka kwa Umma (D by D);
ii) Kuratibu huduma mijini kama vile usafirishaji, maji na usafi wa mazingira;
iii) Kusimamia Tume ya Utumishi wa Walimu;
iv) Kuratibu na Kusimamia Tawala za Mikoa ili ziweze kuziwezesha Halmashauri kutekeleza wajibu wake;
v) Kuratibu Usimamizi na Uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM);
vi) kusimamia na kuratibu shughuli za utolewaji wa huduma za Afya ya Msingi, Ustawi wa Jamii na Lishe
vii) Kuratibu na kusimamia mifumo na miundombinu ya TEHAMA katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi
viii) Kujenga uwezo wa watumishi wa OR-TAMISEMI ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi
ix) Kuratibu shughuli za wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo
x) Kusimamia utendaji wa Mashirika, Taasisi, Programu na miradi iliyo chini ya OR-TAMISEMI
Kupitia JamiiForums.com unaweza kuwasiliana nasi (OR-TAMISEMI) kwa kutuma ujumbe wako kwenye sehemu ya kuweka maoni hapo chini au tutumie kupitia Private Message (PM).
Pia, tunapatikana kupitia:
Instagram @ortamisemi
Twitter @ortamisemitz
Facebook Ofisi ya Rais-Tamisemi
Website www.tamisemi.go.tz
YouTube @ortamisemi
Watssap channel: Ofisi ya Rais - TAMISEMI
Anuani
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
S.l.P 1923 Dodoma - Tanzania,
Telephone: +255 262 321 234
Fax: +255 262 322 116
Email: ps@tamisemi.go.tz
Complain: ps@tamisemi.go.tz
Kituo cha Huduma kwa Mteja
+255 735 160 210 au +255 26 216 0210
Kuanzia saa 1:30 asubuhi mpaka saa 10:30 jioni
Asante.Uhamisho unatoka na Barua zimeshaanza kutumwa kwenye Halmashauri zenu! Tafadhali hakikisha kuwa Taarifa zako zilikamilika na ziliwasilishwa na Katibu Tawala Mkoa wako kama hilo lilikamilika utapokea barua yako hivi karibuni!
Utaandika barua hadi uchakae, serikali kumejaa wala rushwa na wala sio haki.Mwaka wa nane huu mke wangu anahangaikia uhamisho, amekuja dodoma zaidi ya mara tano, ameandika barua zikiwa na viambatanisho vyote muhimu lakini kupo,
Kwanini mnakua hivyo? Seriously miaka nane kuwa mbali na familia inauma sana, naombeni fanyeni kitu muiunganishe familia yangu
Kuna hawa watu wanaitwa maafisa afya ni hovyo kabisaMajukumu ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI
yanatekelezwa katika ngazi ya Makao Makuu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia Hati ya Rais ya Mgawanyo wa Majukumu (Presidential Instrument) iliyotolewa na Rais Mei 2021, majukumu ya OR-TAMISEMI ni pamoja na:-
i) Kuratibu utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Mijini na Vijijini na Upelekaji wa Madaraka kwa Umma (D by D);
ii) Kuratibu huduma mijini kama vile usafirishaji, maji na usafi wa mazingira;
iii) Kusimamia Tume ya Utumishi wa Walimu;
iv) Kuratibu na Kusimamia Tawala za Mikoa ili ziweze kuziwezesha Halmashauri kutekeleza wajibu wake;
v) Kuratibu Usimamizi na Uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM);
vi) kusimamia na kuratibu shughuli za utolewaji wa huduma za Afya ya Msingi, Ustawi wa Jamii na Lishe
vii) Kuratibu na kusimamia mifumo na miundombinu ya TEHAMA katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi
viii) Kujenga uwezo wa watumishi wa OR-TAMISEMI ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi
ix) Kuratibu shughuli za wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo
x) Kusimamia utendaji wa Mashirika, Taasisi, Programu na miradi iliyo chini ya OR-TAMISEMI
Kupitia JamiiForums.com unaweza kuwasiliana nasi (OR-TAMISEMI) kwa kutuma ujumbe wako kwenye sehemu ya kuweka maoni hapo chini au tutumie kupitia Private Message (PM).
Kila la KheriNatamani sana kuja kudeal na wala RUSHWA. Hawa watu ndio wanafanya nchi isiendelee...