Ofisi ya Rais – TAMISEMI Special Thread: Karibu tukuhudumie, tupe Maoni, Maswali, Mapendekezo na Malalamiko

Ofisi ya Rais – TAMISEMI Special Thread: Karibu tukuhudumie, tupe Maoni, Maswali, Mapendekezo na Malalamiko

Wanyooshe,wanyooshe wakati naleta malalamiko humu watu walikuwa wanapita kama hawaoni,sasa hivi wameanza kujitokeza wenyewe,kwanza mwaka huu tuko bize na uchaguzi
 
Uhamisho lini @Tamisemi ya Wananchi???? Mnatuma vibali kimyakimya...hawa wakurugenzi wanavikalia chini ya siti zao. Hapa toeni mkeka ili tukapasuane nao.
 
Subiri angalau mwaka upite,make mlitoa oktoba tena mwishoni,si vyema watu kuhama kila mara
 
Tamisemi please toeni vibali vyetu tuhame maana wengine ndoa zitakufa na pia morali kazini hatuna maana kisaikolojia akili haijatulia nawaza matatizo ya familia ilioko huko niliko omba hamia ,aya majibu yenu ya kuwa mda wowote kuanzia sasa vibali vitatoka sio fair,maana kuanzia mwaka jana mwezi wa saba hadi leo ...tuoneeni huruma jamanii .
TUNAOMBA MAJIBU KWENYE HILI LA WALIOMBA UHAMISHO TOKA MWAKA JANA,JULAI 2023..BARUA ZA KUOMBA VIBALI ZILIWASILISHWA KUPITIA maRAS..mfano mkoa wa Arusha, barua zilifika hapo TAMISRMI Dodomq,Julai 30, 2023
 
Mbona ajira ya 2020 December hatujapanda daraja? Hebu tufanyie wepesi na sisi, mjue na sisi ni wakongwe kazini.
Kweli kabisa watufanyie namna. Ujue ni miaka minne kasoro miezi minne tu. Tumeongeza watoto hivyo majukumu yameongezeka😂
 
Ushauri wangu muache kujinunulia magari ya kifahari hadi kufikia kununua gari moja kwa Tsh.milioni 600 wakati nchi yetu ni masikini na wananchi wengi wanaishi kwenye lindi kubwa la umasikini lakini nyinyi hamjali! Muache ufahari na pesa nyingi zielekezwe kwenye kuhudumia wananchi masikini hivi hamjisikii vibaya kumuuzia mwananchi panadol au mseto kwenye zahanati na vituo vya afya mkidai serikali haina uwezo lakini nyinyi viongozi mkiumwa mnaenda kutibiwa India na Ulaya kwa gharama kubwa? Kesho mtaenda kumueleza nini muumba wenu? Kumbukeni duniani hapa tunaishi kwa muda mfupi sana ni vyema nyie wenzetu mliopewa dhamana ya kuhudumia binadamu wenzenu muwatendee vyema.
Ni ushauri tu kuuchukua ama kuuwacha ni uamuzi wenu.
 
Hivi huu mfumo wenu wa kuhama mliuweka kimkakati sio? maana mliweka aina tano za sababu za kuhama, kuumwa,kukaa kituoni zaidi ya miaka.3,kwenda kuuguza wazazi,kushindwa kuendana na mazingira, sasa watu wana hadi vyeti vya hospital na ni seriously issue wameshapitisha maombi yao kwa wakuu wa idara na kadhalika ikifika sehemu ya kusubmitt kwenda mbele mfumo unasema umekaa kituoni chini ya miaka 3 sasa kulikuwa na sababu gani ya kuweka kigezo cha kuumwa kama sifa ya kuomba uhamisho?
 
OR TAMISEMI mmefungua Uzi wenu humu kuonesha nyie ni mabingwa wa dharau au vipi?

Watu wanauliza maswali nyie mko kimya. Jifunzeni toka kwa Dkt. Gwajima D ambaye yeye mwenyewe hujibu maswali mbali mbali anayoulizwa.

Kama hamna majibu Kwa maswali mnayoulizwa, kwa nini mlifungua Uzi hapa JF.

Acheni dharau Kwa watanzania wenzenu nyie watu.
 
Poleni sana wadau,kama kuna ishu yote ya uhamisho niulize nitakujibu info zote ninazo
 
Back
Top Bottom