Ofisi ya Rais – TAMISEMI Special Thread: Karibu tukuhudumie, tupe Maoni, Maswali, Mapendekezo na Malalamiko

Ofisi ya Rais – TAMISEMI Special Thread: Karibu tukuhudumie, tupe Maoni, Maswali, Mapendekezo na Malalamiko

Hawa waliofungua uzi halafu hawa replay hii inaonesha jinsi wananchi wanavoteseka bila kero kushughulikiwa katika maisha halisi ya mtanzania
Hao mbona ndivyo walivyo hadi maofisini kwao. Yaani hii sura waliyoionyesha hapa ndiyo sura yao halisi kabisa hata ukiwakuta ofisini kwao. Wao na ofisi ya Utumishi (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) kitabia ni mtu na pacha wake.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), kupitia thread hii, tutapokea Maoni, Ushauri, Malalamiko, Mapendekezo yako Mwananchi. Tunakuhakikishia kuchukua hatua stahiki kwa haraka zaidi kwa kile utakachokiwasilisha kwetu.

Ikumbukwe kuwa tangu Mwaka 1961 hadi sasa Ofisi ya Rais –TAMISEMI imekuwa ni Wizara inayojitegemea na madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka Madaraka kwa Wananchi ambapo chimbuko lake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 Sura ya 8, Ibara ya 145 na 146.

Hadi sasa Nchi ina Mikoa 26, Wilaya 139, Halmashauri 184, Tarafa 570, Kata 3,956, Vijiji 12,319, Vitongoji 64,361 pamoja na Mitaa 4,263.

Majukumu ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI
yanatekelezwa katika ngazi ya Makao Makuu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia Hati ya Rais ya Mgawanyo wa Majukumu (Presidential Instrument) iliyotolewa na Rais Mei 2021, majukumu ya OR-TAMISEMI ni pamoja na:-

i) Kuratibu utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Mijini na Vijijini na Upelekaji wa Madaraka kwa Umma (D by D);
ii) Kuratibu huduma mijini kama vile usafirishaji, maji na usafi wa mazingira;
iii) Kusimamia Tume ya Utumishi wa Walimu;
iv) Kuratibu na Kusimamia Tawala za Mikoa ili ziweze kuziwezesha Halmashauri kutekeleza wajibu wake;
v) Kuratibu Usimamizi na Uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM);
vi) kusimamia na kuratibu shughuli za utolewaji wa huduma za Afya ya Msingi, Ustawi wa Jamii na Lishe
vii) Kuratibu na kusimamia mifumo na miundombinu ya TEHAMA katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi
viii) Kujenga uwezo wa watumishi wa OR-TAMISEMI ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi
ix) Kuratibu shughuli za wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo
x) Kusimamia utendaji wa Mashirika, Taasisi, Programu na miradi iliyo chini ya OR-TAMISEMI

Kupitia JamiiForums.com unaweza kuwasiliana nasi (OR-TAMISEMI) kwa kutuma ujumbe wako kwenye sehemu ya kuweka maoni hapo chini au tutumie kupitia Private Message (PM).

Pia, tunapatikana kupitia:

Instagram @ortamisemi
Twitter @ortamisemitz
Facebook Ofisi ya Rais-Tamisemi
Website www.tamisemi.go.tz
YouTube @ortamisemi
Watssap channel: Ofisi ya Rais - TAMISEMI

Anuani
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
S.l.P 1923 Dodoma - Tanzania,
Telephone: +255 262 321 234
Fax: +255 262 322 116
Email: ps@tamisemi.go.tz
Complain: ps@tamisemi.go.tz

Kituo cha Huduma kwa Mteja
+255 735 160 210 au +255 26 216 0210
Kuanzia saa 1:30 asubuhi mpaka saa 10:30 jioni
Ivi mnayatatua vipi matatizo ya MaDED kuwadhulumu wazabuni waliotoa huduma kwenye halmashauri hasa katika kipindi ambacho hao maDED hawakuwepo?
 
Utaratibu wa kutoa mikopo kwa makundi maalum kuanzia mwezi huu kwa kushirikisha taasisi za kifedha(mabenki) umekaaje?
 
Poleni,changamoto zinazohusiana na uhamisho uliza utajibiwa hapa,na nina uhakika na majibu nnayo kupa
Kwenye ess wanasema kuhama ni mpka miaka 3, jee ule wa kusubiri kuthibitishwa upo ndani ya hio mi tatu, au ni mitatu baada ya kuthibitishwa?
 
Kwenye ess wanasema kuhama ni mpka miaka 3, jee ule wa kusubiri kuthibitishwa upo ndani ya hio mi tatu, au ni mitatu baada ya kuthibitishwa?
Hiyo ya kuhama baada ya miaka mitatu ni kwa wale wasio na connection pale TAMISEMI au UTUMISHI. Kama una connection utahama hata kama umekaa sehemu miezi mitatu tu.
 
Kwenye ess wanasema kuhama ni mpka miaka 3, jee ule wa kusubiri kuthibitishwa upo ndani ya hio mi tatu, au ni mitatu baada ya kuthibitishwa?
Iwe wa kubadilishana,iwe wa kuhama lazima ufikishe miaka mitatu
 
Hiyo ya kuhama baada ya miaka mitatu ni kwa wale wasio na connection pale TAMISEMI au UTUMISHI. Kama una connection utahama hata kama umekaa sehemu miezi mitatu tu.
Uko sahihi mkuu,connection itakutoa mahali ulipo kwenda unapotaka,kuwa makini kuna matapeli pia
 
Ushauri wangu;
Nafikiri ni wakati sasa wa kuachana na ile dhana ya kufikiri kuwa, Kila Mwalimu hata asiyekuwa na UFAULU WOWOTE kwenye somo la Hesabu anaweza kufundisha Hisabati shule za msingi kwani IMEPITWA NA WAKATI

Na hii inajidhihisha wazi wazi kwani kila mwaka takribani asilimia 80% ya wanafunzi wa shule za msingi za Umma hupata Alama 0% kwenye mtihani wa Hisabati na kuna uwezekano mkubwa kuwa; huo uwiano unaendana sambamba na Asilimia ya waalimu ambao hawana sifa ya kufundisha somo la Hisabati katika shule hizo (naamini mnatakwimu za kuonesha idadi ya waalimu wa Hisabati wenye angalau alama D ya Hesabu kidato cha nne; unaweza kuta hawafiki 15% ya mahataji, utategemea nini? kama sio sifuri) Kwa hiyo sioni haja kabisa ya kupoteza fedha za kufanya utafiti eti kwa nini wanafunzi wanafeli hesabu ambayo ndio msingi wa kila kitu, kwani sababu ipo wazi wazi kuwa, hakuna Waalimu wenye sifa ya kufundisha hesabu!

Nyongeza;
Hesabu ndio Muoarobaini wa HAYA MATATIZO YA VIKOBA/ MIKOPO UMIZA/ KUKWEPA KODI nk nk , Ukifuatilia vizuri utagundua kuwa, haya matatizo kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na watu kutokuwa na uelewa wa Hesabu. Namaanisha wengi wao walipata alama Sifuri hivyo; hukimbilia tu kukopa bila kupiga hesabu ya marejesho na hivyo kuanza kulilia Serikali mwishoni wakidaiwa pesa nyingi.
Mfano mwingine: Kodi ya VAT ni hesabu rahisi sana ila kwa mtu aliyepata alama sifuri hawezi kuelewa na kama biashara haitoshi kuajiri mtu wa kumsaidia hesabu, anaishia kulalamika na kukwepa.....nk nk nk
MADEREVA na ajali za barabarani;
Kuendesha gari ni Hesabu (Fikiria unavyo calculate umbali wa kuovertake, unavyofanya maamuzi ya kuovertake, break nk nk) hesabu tupu.
Kama kigezo cha leseni kingekuwa na hesabu walau D, ungeshangaa ajali zikapungua hadi mkashangaa.

Kwa mtazano wangu, Ili hii Nchi iweze kuvuka hapa ilipo kwa kupata maendeleo ya haraka ya saiyansi na Technologia, Inahitaji MAPINDUZI YA HESABU (Mfano kuajiri waalimu 30,000 wa hesabu tu); hata waliopita sekondari za Umma wanajua kuwa, huko pia kuna upungufu mkubwa, nafuu yake ni kuwa, waliopo huko japo wachache Ila wana sifa ya kufundisha Hesabu.
MAENDELEO YA HARAKA HAYAWEZI KUPATIKANA BILA KUWEKA MSINGI WA HESABU!
 
Hawa waliofungua uzi halafu hawa replay hii inaonesha jinsi wananchi wanavoteseka bila kero kushughulikiwa katika maisha halisi ya mtanzania
Zamani nilikuwaga nasikia watu wakiiponda sana Tamisemi nikafiri labda majungu tu ila kupitia Hawa walioanzisha huu uzi nimegundua Tamisemi Ina wafanyakazi Vimeo balaa
 
Wale wa uhamisho admin niko hapa
Hivi kwa walimu wa shule ya msingi ili kuhamia mkoa mwingine bado ni muhimu kuhakikishiwa kimaandishi kuhusu upatikanaji wa nafasi katika halmashauri unayotaka kuhamia kwanza na kisha unatumia taarifa hiyo kama moja ya viambatanisho kwenye mfumo? Au njia nyingine yenye uhakika na nyepesi zaidi ni ipi katika haya mazingira ambapo mfumo umekuwa ni kizungumkuti?
 
Hivi kwa walimu wa shule ya msingi ili kuhamia mkoa mwingine bado ni muhimu kuhakikishiwa kimaandishi kuhusu upatikanaji wa nafasi katika halmashauri unayotaka kuhamia kwanza na kisha unatumia taarifa hiyo kama moja ya viambatanisho kwenye mfumo? Au njia nyingine yenye uhakika na nyepesi zaidi ni ipi katika haya mazingira ambapo mfumo umekuwa ni kizungumkuti?
Nje ya mfumo ni connection my dear
 
Back
Top Bottom