Ofisi ya Rais – TAMISEMI Special Thread: Karibu tukuhudumie, tupe Maoni, Maswali, Mapendekezo na Malalamiko

Ofisi ya Rais – TAMISEMI Special Thread: Karibu tukuhudumie, tupe Maoni, Maswali, Mapendekezo na Malalamiko

Ndugu wana JamiiForums,

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), kupitia thread hii, tutapokea Maoni, Ushauri, Malalamiko, Mapendekezo yako Mwananchi. Tunakuhakikishia kuchukua hatua stahiki kwa haraka zaidi kwa kile utakachokiwasilisha kwetu.

Ikumbukwe kuwa tangu Mwaka 1961 hadi sasa Ofisi ya Rais –TAMISEMI imekuwa ni Wizara inayojitegemea na madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka Madaraka kwa Wananchi ambapo chimbuko lake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 Sura ya 8, Ibara ya 145 na 146.

Hadi sasa Nchi ina Mikoa 26, Wilaya 139, Halmashauri 184, Tarafa 570, Kata 3,956, Vijiji 12,319, Vitongoji 64,361 pamoja na Mitaa 4,263.

Majukumu ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI
yanatekelezwa katika ngazi ya Makao Makuu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia Hati ya Rais ya Mgawanyo wa Majukumu (Presidential Instrument) iliyotolewa na Rais Mei 2021, majukumu ya OR-TAMISEMI ni pamoja na:-

i) Kuratibu utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Mijini na Vijijini na Upelekaji wa Madaraka kwa Umma (D by D);
ii) Kuratibu huduma mijini kama vile usafirishaji, maji na usafi wa mazingira;
iii) Kusimamia Tume ya Utumishi wa Walimu;
iv) Kuratibu na Kusimamia Tawala za Mikoa ili ziweze kuziwezesha Halmashauri kutekeleza wajibu wake;
v) Kuratibu Usimamizi na Uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM);
vi) kusimamia na kuratibu shughuli za utolewaji wa huduma za Afya ya Msingi, Ustawi wa Jamii na Lishe
vii) Kuratibu na kusimamia mifumo na miundombinu ya TEHAMA katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi
viii) Kujenga uwezo wa watumishi wa OR-TAMISEMI ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi
ix) Kuratibu shughuli za wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo
x) Kusimamia utendaji wa Mashirika, Taasisi, Programu na miradi iliyo chini ya OR-TAMISEMI

Kupitia JamiiForums.com unaweza kuwasiliana nasi (OR-TAMISEMI) kwa kutuma ujumbe wako kwenye sehemu ya kuweka maoni hapo chini au tutumie kupitia Private Message (PM).

Pia, tunapatikana kupitia:

Instagram @ortamisemi
Twitter @ortamisemitz
Facebook Ofisi ya Rais-Tamisemi
Website www.tamisemi.go.tz
YouTube @ortamisemi
Watssap channel: Ofisi ya Rais - TAMISEMI

Anuani
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
S.l.P 1923 Dodoma - Tanzania,
Telephone: +255 262 321 234
Fax: +255 262 322 116
Email: ps@tamisemi.go.tz
Complain: ps@tamisemi.go.tz

Kituo cha Huduma kwa Mteja
+255 735 160 210 au +255 26 216 0210
Kuanzia saa 1:30 asubuhi mpaka saa 10:30 jioni
Shida yangu ni uhamisho status inasoma TAMISEMI muda mrefu naomba kujua nitapata barua lini, sababu nipo stressed Sana miaka 15 naishi mbali na familia tafadhali naomba mnisaidie nashindwa Hadi kufanya kazi kwa Sasa
 
Maoni, ushauri kwa Mama yetu kipenzi Rais wa JMT ambaye ndio mwenye serikali na mwenye mamlaka ya kutoa agizo lolote : kilio walioajiriwa 2014 kudai kupandishwa vyeo kama ilivyostahiki hakijasikilizwa, ni hivi 👉kufikia 2018 walipaswa kupanda vyeo kwa mara ya kwanza, kufikia 2021 walipaswa kuwa kwenye cheo cha pili, kufikia 2024 walipaswa kuwa kwenye cheo cha tatu, lakini ilivyo ni kuwa wapo kwenye cheo cha pili badala ya cheo cha tatu.
 
Shida yangu ni uhamisho status inasoma TAMISEMI muda mrefu naomba kujua nitapata barua lini, sababu nipo stressed Sana miaka 15 naishi mbali na familia tafadhali naomba mnisaidie nashindwa Hadi kufanya kazi kwa Sasa
TAMISEMI kuna mtandao wa rushwa. Ukiuliza wengi waliohama wametoa rushwa. Hivi mtu hawezi kuhama kwa utaratibu wa kawaida hadi azungushwezungushwe?
 
Mawasiliano hovyo.

Namba za simu zote za halmashauri,, wilaya, namaanisha zote zilizowekwa kwenye tovuti (websites) zao. Mpaka za wizara yenu. Hazijibiwi au hazifanyi kazi.

Na email sdress zote mlizoweka, tukiandika emails hazijibiwi.

Huo ndiyo utawala bora?
 
Pale kuna mkwe mtu. Makelele na mbwembwe nyiiingi lakini hata kusimamia ipasavyo uwajibikaji wa pale makao makuu tu ya wizara yake pamemshinda.
 
Napenda kuwapongeza TAMISEMI pamoja na UTUMISHI wa UMMA kwa kutoa fursa za uhamisho kwa watumishi.

Hii mmezingatia, ustawi wa familia za watumishi, kupunguza migogoro ya ndoa na ndoa kuvunjika, watoto kupata malezi bora, hali kadhalika ustawi wa maendeleo ya kiuchumi kwa familia husika, kwani wenza wakiwa pamoja ni rahisi kufanya mipango ya maendeleo, pia kupunguza gharama za maisha kwa wata share nyumba, chakula, utilities n.k.

Hii pia ni kuzingatia sheria mbali mbali, ikiwemo katiba ya nchi, sheria ya mtoto pamoja na sheria ya ndoa.

Pamoja na pongezi hizo, kuna mambo machache yamejitokeza.

1. Muda kuwa finyu, tokea tarehe ya tangazo mpaka tarehe 5 October 24 ambayo nayo haikuzingatiwa na wakurugenzi wengi, kuna baadhi ya watumishi hawakuweza kuwasilisha taarifa zao kutokana na mazingira ya vituo vyao vya kazi kuwa mbali na mahali walipoziacha taarifa, mfano cheti cha ndoa.

2. Wakurugenzi kupunguza muda wa "deadline" mpaka tarehe 3 october, badala ya tar 5 kwa sababu zao binafsi.

3. Wakurugenzi wengi wameweka mazingira magumu ya utekelezaji wa agizo hilo. Mf. Kuchelewa kutoa taarifa hiyo (tangazo) kwa watumishi, pia kuwakwepa watumishi wanaoleta taarifa zao kwa ajili ya uhamisho na kufunga zoezi kabla ya muda.

Wanafanya hivyo kwa madai kuwa, kukiwa na watumishi wengi wanaohama, basi itapelekea upungufu wa watumishi kwenye eneo lake, wakati ukweli ni kwamba uwiano wa wanaohama unaratibiwa na utumishi wa umma kwa kuzingatia mahitaji.

Baada ya kusema hayo, ombi langu kwenu, Ninaomba muda uongezwe, angalau mpaka 30 October 2024.

Bado kuna idadi kubwa ya watumishi tunahitaji nafasi hii, kwani tumeacha familia zetu mbali, tunapata mfadhaiko wa akili kiasi hata kupunguza kasi ya utendaji.

Naomba kuwasilisha.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), kupitia thread hii, tutapokea Maoni, Ushauri, Malalamiko, Mapendekezo yako Mwananchi. Tunakuhakikishia kuchukua hatua stahiki kwa haraka zaidi kwa kile utakachokiwasilisha kwetu.

Ikumbukwe kuwa tangu Mwaka 1961 hadi sasa Ofisi ya Rais –TAMISEMI imekuwa ni Wizara inayojitegemea na madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka Madaraka kwa Wananchi ambapo chimbuko lake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 Sura ya 8, Ibara ya 145 na 146.

Hadi sasa Nchi ina Mikoa 26, Wilaya 139, Halmashauri 184, Tarafa 570, Kata 3,956, Vijiji 12,319, Vitongoji 64,361 pamoja na Mitaa 4,263.

Majukumu ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI
yanatekelezwa katika ngazi ya Makao Makuu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia Hati ya Rais ya Mgawanyo wa Majukumu (Presidential Instrument) iliyotolewa na Rais Mei 2021, majukumu ya OR-TAMISEMI ni pamoja na:-

i) Kuratibu utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Mijini na Vijijini na Upelekaji wa Madaraka kwa Umma (D by D);
ii) Kuratibu huduma mijini kama vile usafirishaji, maji na usafi wa mazingira;
iii) Kusimamia Tume ya Utumishi wa Walimu;
iv) Kuratibu na Kusimamia Tawala za Mikoa ili ziweze kuziwezesha Halmashauri kutekeleza wajibu wake;
v) Kuratibu Usimamizi na Uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM);
vi) kusimamia na kuratibu shughuli za utolewaji wa huduma za Afya ya Msingi, Ustawi wa Jamii na Lishe
vii) Kuratibu na kusimamia mifumo na miundombinu ya TEHAMA katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi
viii) Kujenga uwezo wa watumishi wa OR-TAMISEMI ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi
ix) Kuratibu shughuli za wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo
x) Kusimamia utendaji wa Mashirika, Taasisi, Programu na miradi iliyo chini ya OR-TAMISEMI

Kupitia JamiiForums.com unaweza kuwasiliana nasi (OR-TAMISEMI) kwa kutuma ujumbe wako kwenye sehemu ya kuweka maoni hapo chini au tutumie kupitia Private Message (PM).

Pia, tunapatikana kupitia:

Instagram @ortamisemi
Twitter @ortamisemitz
Facebook Ofisi ya Rais-Tamisemi
Website www.tamisemi.go.tz
YouTube @ortamisemi
Watssap channel: Ofisi ya Rais - TAMISEMI

Anuani
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
S.l.P 1923 Dodoma - Tanzania,
Telephone: +255 262 321 234
Fax: +255 262 322 116
Email: ps@tamisemi.go.tz
Complain: ps@tamisemi.go.tz

Kituo cha Huduma kwa Mteja
+255 735 160 210 au +255 26 216 0210
Kuanzia saa 1:30 asubuhi mpaka saa 10:30 jioni
Nyie tamisemi why ajira zenu ni za mchongo na za kupeana kwa connection na kwa wale wasio na connection si rahisi kupata??
 
RUDISHENI AJIRA ZENU ZOTE KWA MAMLAKA ZENU UTUMISHI MIYAYUSHO SANA
 
Ni miaka 4 sasa nasubirii fidia yangu, nimewaandikia barua zaidi ya 5 hakuna jibu la maana ninalopata toka Wilayani kwangu Kinondoni. Si Mkurugenzi wala her subordinates wanatoa msaada na si mimi tu ninaowalalamikia, Wilaya ya Kinondoni mna shida na huduma zenu.
 
Kweli kabisa yaani ubovu wa halmashauri nyingi zinatokana na TAMISEMI yenyewe
 
Ni miaka 4 sasa nasubirii fidia yangu, nimewaandikia barua zaidi ya 5 hakuna jibu la maana ninalopata toka Wilayani kwangu Kinondoni. Si Mkurugenzi wala her subordinates wanatoa msaada na si mimi tu ninaowalalamikia, Wilaya ya Kinondoni mna shida na huduma zenu.
Utalipwa sasa sababu ya hizi chaguzi!
 
Habari Viongozi TAMISEMI naomba kujua kuhusu Nafasi za Ukufunzi wa vyuo vya Kati mbona Huwa hazitangazwi ni dhahiri watumishi hustaafu katika vyuo mbalimbali nchini, je hizo Nafasi zinajazwaje? naomba ufafanuzi kidogo.
 
TAMISEMI,ni kwanini serikali inatumia madaftari ya karatasi na pen kuborehsa daftari la wapiga kura ilihali zoezi hili kunakila sababu yakufanyika kidigitali?
 
Naomba email/namba ya simu ya kamishna wa elimu(anayehusika na kusajili shule mpya za msingi Tanzania)
Asante.
 
Sijui kama hawa NSSF - wapo chini yenu
Ukweli hili shirika bado kuna mambo hayako sawa kwa sababu wanafanya kazi kwa taratibu zile zile za miaka ya 1980 ambapo hapakuwa na reliable digital data base, Kitambulisho cha taifa na Internet.

Badala ya kushinda maofisini kwa nini wasitembelee taasisi/mashirika waliko wafanyakazi (wanaowalipa) wakaweka kila kitu wanachohitaji kwa data base, siku mtu akistaafu anakwenda tu na barua ya utambulisho ya mwajiri na kitambulisho chake cha taifa anapata mafao yake?

Kuzunguka huko ni faida marambili kwani pamoja na kukusanya taarifa za wanachama wao, kutawasaidia kuelimisha, kupanua uigo na kukutana na wanachama na kupata maoni yao nk
HAI INGII AKILINI KWA KARNE HII, MFANYAKAZI ACHANGIE PENGINE KWA MIAKA 25, HALAFU SIKU ANASTAAF NDIO ANATAKIWA ALETE UTAMBULISHO WA AJIRA n.k/HATAMBULIKI ? Fikiria huko Private ambapo mtu anaweza kufanya kazi tofauti tofauti (mpya) kabla ya kustaafu?
Kuna kitu hakipo sawa !

Kinachoendelea kwa sasa kuna mwanya mkubwa wa kuchelewesha kwa kizingizio hajakamisha, taratibu..... Naamini mnajua matokeo yake......
 
Back
Top Bottom