OR TAMISEMI
Ministry
- Jul 3, 2024
- 20
- 93
- Thread starter
- #81
Tumepokea na tunafanyia kazi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aaaah aaah. Kweli nyinyi TAMISEMI hamjitambui kabisa. Sasa hapo umepokea nini? Acheni ubabaishaji, rushwa, upendeleo, dharau, majivuno na kujiona nyinyi ni mungu watu ili nchi ipige hatua ya kwenda mbele.Tumepokea na tunafanyia kazi
Hilo la huyo Mtumishi wa Manispaa ya Sumbawanga mmelipokea?Tumepokea na tunafanyia kazi
Tamisemi tunaomba mfanye vitu kama wasomi unasema umepokea na unafanyia kazi …unafanyia kazi kitu gani na changamoto gani? Hivi mmekosa cha kuwajibu wadau hapo juu yaani ofisi yote imekosa hata muda wa kujibu? Sasa kama hamjibu maswali ya wadau mnafanya nini ofisini? Kwanini tusiseme ninyi ndio mnahujumu Mh Rais? Sasa hao watu ambao hamjawajibu kwanini wasimlamikie Rais?Tumepokea na tunafanyia kazi
Mwalimu mkuuNaona ajira za ualimu zimetoka, kuna kijana amekuwa akijitolea kwenye kituo chetu kwa miaka takribani mitano na anafanya kazi kwa uadilifu mkubwa na anaipenda kazi yake.
Tatizo amekuwa kila akiomba hapati kwa miaka yote hiyo. Naomba kama itawezekana akumbukwe kipindi hiki, kama utaruhusu nitakutumia majina yake na mawasiliano yake PM. Nasubiri mrejesho mkuu.
Mwimu mkuu naomba umwambie aombe kama wenzie na umuwekee recomendation letter kwenye mfumo ajaze kila kitu! Sasa hivi ni mwendo wa interview….kuna watu huwa wanakosa pakujitolea je hao wafanyweje? Hapa uzuri ni usahili aoneshe uwezo wake atapata kazi!Naona ajira za ualimu zimetoka, kuna kijana amekuwa akijitolea kwenye kituo chetu kwa miaka takribani mitano na anafanya kazi kwa uadilifu mkubwa na anaipenda kazi yake.
Tatizo amekuwa kila akiomba hapati kwa miaka yote hiyo. Naomba kama itawezekana akumbukwe kipindi hiki, kama utaruhusu nitakutumia majina yake na mawasiliano yake PM. Nasubiri mrejesho mkuu.
OR TAMISEMIMtumishi mwenye Mkataba namba Na. SMC/CW/PF.113/3 amefika Ofisini kwetu na ameomba tupaze sauti kwa niaba yake. Hii hapa historia fupi ya malalamiko yake.
Wakati wa zoezi la uhakiki wa Watumishi wa Umma 2016/2017 mwajiri wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga alizuia, kusitisha na Hatimaye kumwondoa kwenye malipo ya mshahara akiwa masomoni kwa Shahada ya kwanza katika moja ya vyuo vikuu hapa nchini. (Zingatia kuwa alikuwa na sifa zote kwenda masomoni na kwa ufadhili wa Mwajiri wake). Huyu Mtumishi alilalamikia hatua hiyo na baada ya uhakiki mwajiri alijiridhisha pasi na shaka kwamba;
1. Si Mtumishi hewa.
2. Alikuwa na Ruhusa Rasmi ya kwenda Masomoni.
CHANGAMOTO
Kwa kuwa mwajiri alishazuia, kusitisha na kumwondoa kwenye malipo ya mshahara tangu Januari 2017, imekuwa ni vigumu kumrejesha Kazini licha ya juhudi kubwa za ufuatiliaji wa mara kwa mara na kwa muda wote anazoendelea kuchukua kwa Muda wa miaka 7.
sasa! Ikumbukwe kwamba kati ya Julai na Disemba 2021, Ndugu, Jamaa na Marafiki walilazimika kumchangia Fedha za kuweka kambi Ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ili kukwamua shauri lake.
Kwa ujumla alifanikiwa kwa hatua kadhaa maana kamati ya nidhamu ilimuita kwa barua yenye Kumb. Na.SMC/CW/PF.118/6 na kumhoji kwa maneno na kwa Maandishi. Kamati hiyo iliahidi kutoa taarifa yake kwa Mkurugenzi ili nae atoe uamuzi wake kulingana na Taratibu.
OMBI LAKE KWA MAMLAKA HIZI
Anaomba Mamlaka zimsaidie kujua.
A) Mchakato uliotumika kuzuia, kusimamisha na Hatimaye kumwondoa kwenye malipo ya Mshahara January 2017.
B) Majibu ya Kamati ya Nidhamu chini ya Ofisi Mwajiri wake iliyomuita na kumhoji tarehe 11.11.2021 kwa Barua yenye Kumb.Na SMC/CW/PF.118/6
C) Endapo hatua A na B hapo juu hazikuzingatia Kanuni za Utumishi wa Umma, basi aruhusiwe kuendelea kutumikia mkataba wake wa Ajira kama ulivyo na Marekebisho yake.
D) Na iwapo alishaondolewa Kazini, ni haki ajulishwe kwa Barua Rasmi kulingana na Sheria, Taratibu na Kanuni za Kiutumishi.
IKUMBUKWE KUWA
Mheshimiwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo kwa waliokuwa watumishi hewa kurejeshewa sehemu ya iliyokuwa michango yao. Lakini kwa kesi ya Mtumishi huyu imekuwa ni vigumu maana si Mtumishi hewa na hana Barua yoyote inayoelezea hatima ya Mkataba wake vs Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Amejaribu kudai mafao yake PSSSF, Jambo hili nalo limekuwa gumu na kwa ufupi limeshindikana maana hana fao analoweza kuangukia.
TETESI ZILIZOPO KUHUSU UGUMU WA JAMBO HILI
Inasadikika kwamba Afisa Utumishi katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa wakati huo Bwana Shaphat Samuel Kaponela, alificha Jalada (Kama siyo kulipoteza kabisa) la Mtumishi huyu na hivyo kwa sasa inakuwa vigumu kwa Watendaji waliopo kufanya Uamuzi Sahihi.
Afisa huyo alichukua Uamuzi huo wa ajabu baada ya kubaini kuwa aliipotosha Mamlaka kufikia maamuzi ya kufaa. Kwa sasa Afisa huyo amehamishwa. Tunazo nyaraka nyingi kuhusiana na shauri hili na tunapanga namna ya kumsaidia huyu mwenzetu ili haki yake ipatikane maana Jambo hili limekuwa ni mateso kwake yeye na familia yake. Amerudi kwao kijijini na anajitafuta kutokea huko. Mamlaka na wadau mbalimbali mvusheni mwenzetu.
Naomba swali langu hili lijibiwe.Watumishi wa umma ambao tumeomba UHAMISHO kwa kutumia mfumo wa ESS na maombi yanaonesha yapo TAMISEMI ni lini mtayashughulikia na kutoa majina ya UHAMISHO?
Msalimie mkwe wa mama yuleNdugu wana JamiiForums,
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), kupitia thread hii, tutapokea Maoni, Ushauri, Malalamiko, Mapendekezo yako Mwananchi. Tunakuhakikishia kuchukua hatua stahiki kwa haraka zaidi kwa kile utakachokiwasilisha kwetu.
Ikumbukwe kuwa tangu Mwaka 1961 hadi sasa Ofisi ya Rais –TAMISEMI imekuwa ni Wizara inayojitegemea na madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka Madaraka kwa Wananchi ambapo chimbuko lake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 Sura ya 8, Ibara ya 145 na 146.
Hadi sasa Nchi ina Mikoa 26, Wilaya 139, Halmashauri 184, Tarafa 570, Kata 3,956, Vijiji 12,319, Vitongoji 64,361 pamoja na Mitaa 4,263.
Majukumu ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI
yanatekelezwa katika ngazi ya Makao Makuu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia Hati ya Rais ya Mgawanyo wa Majukumu (Presidential Instrument) iliyotolewa na Rais Mei 2021, majukumu ya OR-TAMISEMI ni pamoja na:-
i) Kuratibu utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Mijini na Vijijini na Upelekaji wa Madaraka kwa Umma (D by D);
ii) Kuratibu huduma mijini kama vile usafirishaji, maji na usafi wa mazingira;
iii) Kusimamia Tume ya Utumishi wa Walimu;
iv) Kuratibu na Kusimamia Tawala za Mikoa ili ziweze kuziwezesha Halmashauri kutekeleza wajibu wake;
v) Kuratibu Usimamizi na Uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM);
vi) kusimamia na kuratibu shughuli za utolewaji wa huduma za Afya ya Msingi, Ustawi wa Jamii na Lishe
vii) Kuratibu na kusimamia mifumo na miundombinu ya TEHAMA katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi
viii) Kujenga uwezo wa watumishi wa OR-TAMISEMI ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi
ix) Kuratibu shughuli za wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo
x) Kusimamia utendaji wa Mashirika, Taasisi, Programu na miradi iliyo chini ya OR-TAMISEMI
Kupitia JamiiForums.com unaweza kuwasiliana nasi (OR-TAMISEMI) kwa kutuma ujumbe wako kwenye sehemu ya kuweka maoni hapo chini au tutumie kupitia Private Message (PM).
Pia, tunapatikana kupitia:
Instagram @ortamisemi
Twitter @ortamisemitz
Facebook Ofisi ya Rais-Tamisemi
Website www.tamisemi.go.tz
YouTube @ortamisemi
Watssap channel: Ofisi ya Rais - TAMISEMI
Anuani
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
S.l.P 1923 Dodoma - Tanzania,
Telephone: +255 262 321 234
Fax: +255 262 322 116
Email: ps@tamisemi.go.tz
Complain: ps@tamisemi.go.tz
Kituo cha Huduma kwa Mteja
+255 735 160 210 au +255 26 216 0210
Kuanzia saa 1:30 asubuhi mpaka saa 10:30 jioni