Hata makaburu walikuwa na sheria ya ubaguzi wa rangi. Ilikuwa ndiyo sheria ya nchi, lakini ni sheria dhalimu.
Hata sheria zipo dhalimu zinazotakiwa kuping3a na kufutwa.
Hizi sheria za "indefinite detention" ni sheria ambazo zilisemwa vibaya kama sheria 40 kandamizi na marehemu Jaji Nyalali katika ripoti ya tume aliyoiongoza.
Ni sheria za kikoloni zilizotumika kuwadhibiti wapigania uhuru.
Cha ajabu, wazalendo wamechukua nchi zao, watu walewale waliopinga ukoloni, walipochukua madaraka wao wakaona sheria hizi za kikoloni ni tamu, hawakuziondoa.
Tangu ukoloni mpaka tume ya Nyalali sheria hizi kandamizi za hazijaondolewa.
Tangu Jaji Nyalali akemee ubaya wa sheria hizi kandamizi, moaka leo hazijaondolewa.