Ofisi ya Waendesha Mashtaka kugeuka kuwa ofisi ya wafuta mashtaka kunatia doa mfumo wa haki nchini

Wigo upi?

Unaelewa hata gaidi au tapeli ukimfunga bila kufuata due process unajiwekea mazingira ya kujitetea kaonewa yanayoweza kupelekea kesi kufutwa?
Due process maana yake nini?

Kuna sheria inayotoa mwongozo kuhusu muda wa kufanya upelelezi?
 
Usikute wewe ulikua katibu muhtasi kwenye kundi la mauaji la wasiojulikana,,zama zenu zimepita,,kiongozi mwenye hekima hawezi kukaa anawinda winda kuwaumiza raia wake na kuwafirisi ili yeye na ukoo wake ndo wabakie matajiri
 

Penseli Ina ufuto kwa juu, Ina mamlaka ya kufuta na kuandika, sasa Kama hujaelewa muulize pili Yule mtoto wako wa la 2 au Mwanasha wa la 4
 
Naamini labda DPP hakuelewa vyema maelekezo maana anaachia Kila mtu,

Yaani mpaka matapeli maarufu.
Tapeli yupi?,kama unamuongelea papa msofe ,huyo si alihukumiwa na wakamtoa pesa kisha wakamkamata tena ,wakamtoa upepo,kusha wakamkamata tena..
Huo ulikua uhasama,sijui labda kuna mtu walinyang'anyana mwanamke,😁😁,sio kwa kukomoana vile asee
 
Hivi unayajua madaraka na mamlaka ya DPP kikatiba?Sheria zilizopo,au unacjojua ni kufunga watu tu,shame !!!!
 
Mtapata tabu sana, kubambika kesi kisa mnatofautiana siasa au itikadi no.Imeisha hiyo
 
.kwa nn Askari hakupeleka uthibitisho?
 
Kama unadhania DPP anawaachia watuhumiwa wanaosahili kuhukumiwa, peleka huo ushahidi ambao mpaka leo Mahakama haijapokea.

Uzuri mmoja jinai haifi wala kufutika
 
Kama haipo Ni uhuni, unaanzaje kumkamata mtu na kumweka ndani miaka 9 Kisha unasema upelelezi haujakamilika?
Hata makaburu walikuwa na sheria ya ubaguzi wa rangi. Ilikuwa ndiyo sheria ya nchi, lakini ni sheria dhalimu.

Hata sheria zipo dhalimu zinazotakiwa kupingwa na kufutwa.

Hizi sheria za "indefinite detention" ni sheria ambazo zilisemwa vibaya kama sheria 40 kandamizi na marehemu Jaji Nyalali katika ripoti ya tume aliyoiongoza.

Ni sheria za kikoloni zilizotumika kuwadhibiti wapigania uhuru.

Cha ajabu, wazalendo wamechukua nchi zao, watu walewale waliopinga ukoloni, walipochukua madaraka wao wakaona sheria hizi za kikoloni ni tamu, hawakuziondoa.

Tangu ukoloni mpaka tume ya Nyalali sheria hizi kandamizi hazijaondolewa.

Tangu Jaji Nyalali akemee ubaya wa sheria hizi kandamizi, mpaka leo hazijaondolewa.
 
DPP aendelee kukomaa na kesi ambazo hazina mshiko? Kesi za kutengeneza na kukomoa ambazo hawezi kuzithibitisha mahakamani? Bora ameamua kuchukua njia tofauti na ya mr Biswalo.
 
Laana kama hii alitengeneza mwendazake
 
Wigo uliowekwa na Katiba. Kautizame — umeelezwa vyema.

Hiyo "due process" unayoitaka wewe ni ipi?
Due process inayoondokana na letter na spirit ya sheria kandamizi za kikoloni 40 kama zilivyotajwa katika ripoti ya tume ya Jaji Nyalali.

Sheria hizi na zinazofanana nazo zinaipa nguvu serikali kuwafunga watu kizuizini bila mashitaka, au kuwaweka mahabusu kwa muda mrefu kwa kisingizio cha "uchunguzi unaendelea".

Hiyo katiba unayoisema pia inampa mtu haki ya kujitetea mahakamani.

Kwenye sheria kuna msemo " justice delayed is justice denied".

Unapomfunga mtu mahabusu miaka sita au zaidi, bila kukamilisha uchunguzi wala kumpa nafasi ya kujitetea, umemuondolea uhuru wake kwa miaka sita kabla hata hujamuhukumu kwenye kesi.

Hicho tayari ni kifungo cha miaka sita kabla hata ya hukumu.
 
Kiranga kongole, well put and professionally with living examples
 
Unataka muda wa kufanya upelelezi uwe kiasi gani?

Hii sio hisabati, kwamba moja jumlisha moja ni mbili.

It depends on case to case basis, available resources, technology and national security.

Kuna makesi ya mauaji yanachukua mpaka miaka kumi. Washtakiwa wamekimbia, mashahidi wameuwawa ama kujificha.

Wakati mwingine mpaka ufanye extradition, usubiri correspondences kutoka nchi jirani, ama uombe uchunguzi ufanyike kwenye foreign soil nk...

Ni rahisi sana kwa wanaharakati wa mitandaoni kupiga mayowe na kubwata...... ooh tunaonewa!!!

But when it comes to the reality on ground, mambo yanahitaji utimamu.

Mahakama haiendeshwi kwa harakati za kisiasa. Kuna michakato.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…