Ogopa kufanya jambo ambalo Nyerere hakufanya

Agree
 
Hakika mkuu Saudi Arabia ama quatar isingekua hivyo leo
 
Tangu lini zezeta anayejiita chura kiziwi akawa na akili kuliko the legendary J.K Nyerere?
 
Nyerere ndio kaharibu nchi, hakupenda mawazo pinzani, alizani yeye pekee ndio mwerevu, siku za mwishoni nchi ilimshinda
Kwa unavyoona wewe kati ya hawa viongozi wako wa leo na Nyerere ni nani anakubali mawazo pinzani?

Watu wengi wanamtafsiri Nyerere kivingine kwamba hakupenda mawazo pinzani lakini wanasahau kwamba Nyerere kama kiongozi mwingine yoyote yule wa juu ni lazima uwe na vision ya unapotaka kuipeleka nchi (taasisi) unayoiongoza

Ilikuwa ni lazima nyakati za Nyerere awe mkali kwa mawazo kinzani hasa ukizingatia dunia yenyewe ilikuwa imagawanyika pande mbili; Ujamaa au ubapari

Yeye kama kiongozi wa juu alitamani nchi yake aipeleke kwenye Ujamaa kwasababu alizoziamini yeye

Kwa vyovyote vile isingewezekana wasaidizi wake woooooote wamuunge mkono na kukubaliana naye. Labda wangekuwa maroboti ingewezekana, lakini kwa vila nao walikuwa watu, wenye fikra, wenye matamanio, wenye malengo, na waliotamani kuwa na mali ilikuwa lazima watokee watu wa kumpinga na wengine wakukubaliana naye

Wewe ni kiongozi mkuu, mwenye dira na ramani kamili ya namna unavyotaka nchi iwe, ungefanyaje?
 
Muundo wa Muungano wetu hautofautiani sana na United Kingdom wao wana Acts of Union sisi pia tuna hizo hizo.

Lisu ni msomi wa sheria ila kwa hapo alitulisha matango.

Akubali tu kuwa hawezi akajua kila kitu.
 
Ukweli ni kwamba kuna viwanja kadhaa vya ndege (ndogo) ndani ya hifadhi ya Serengeti.
Lakini uwanja mkubwa zaidi unatarajiwa kujengwa kilomita kadhaa nje ya hifadhi.
Kifupi ni kwamba uwanja huo utakuwa na faida kubwa kwa mji wa Mugumu, Mkoa wa Mara, Kanda ya Ziwa na Taifa kwa ujumla!

NB: Nyerere aliwaza na kufanya kwa wakati wake! Nyakati zinabadilika!
 
Muundo wa Muungano wetu hautofautiani sana na United Kingdom wao wana Acts of Union sisi pia tuna hizo hizo.

Lisu ni msomi wa sheria ila kwa hapo alitulisha matango.

Akubali tu kuwa hawezi akajua kila kitu.
Kwahiyo muungano wetu ni mzuri kuliko wa UK?
 
Ndio maana nikasema kama hakuna tija kama ilivyo sasa uvunjike tu maana mimi sioi tija ya muungano kwa sasa .
 
Kwahiyo muungano wetu ni mzuri kuliko wa UK?
Ni halali kabisa.

Kulikuwa na mchakato kabla ya Muungano.

Makubaliano ya Muungano yalisainiwa na serikali ya Tanganyika na Zanzibar tarehe 22, April, 1964.

Baada ya makubaliano hayo,

Bunge lilipitisha muswada na kubariki makubaliano hayo tarehe 25, April, 1964, ambayo yalisainiwa na Nyerere.
 
Ndio maana nikasema kama hakuna tija kama ilivyo sasa uvunjike tu maana mimi sioi tija ya muungano kwa sasa .
Ni kweli kabisa , tungalikaa kila mmoja na nchi yake . Si tuko majirani Wazuri tu na Kenya, Uganda , Msumbiji nk maisha yanakwenda. Kwanini tuvutane siku zote
 
Kwa mujibu wa makubaliano muungano si halali kwani haukusainiwa na bunge la a Zanzibar ambalo ni Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa makubaliano


View: https://youtu.be/x5pYPbYHkVc?is=BYKpW8aarzc7dFMM
 
Hiyo hati ya muungano kwanini huwa inafichwa?

Na ni kwanini kila anayeupinga huu muungano huwa anatishiwa wengine walipotezwa kabisa na Jumbe aliwekwa house arrest.
 
Kwa mujibu wa makubaliano muungano si halali kwani haukusainiwa na bunge la a Zanzibar ambalo ni Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa makubaliano


View: https://youtu.be/x5pYPbYHkVc?is=BYKpW8aarzc7dFMM
Bunge lililopitisha hayo makubaliano lilikuwa Bunge la JMT na katiba iliyotumika ya mpito ni ya Tanganyika mpaka ilipopatikana ya JMT 1977.

Nyerere ndiye alisaini muswada huo kama Rais wa JMT.
 
Sasa wewe si ni chawa wa Wanamtandao, Ni wapi Nyerere aliua watanganyika elfu 17 ndani ya siku 3?
 
Bunge lililopitisha hayo makubaliano lilikuwa Bunge la JMT na katiba iliyotumika ya mpito ni ya Tanganyika mpaka ilipopatikana ya JMT 1977.

Nyerere ndiye alisaini muswada huo kama Rais wa JMT.
Kwa mujibu wa makubaliano ya muungano ili hiyo hati iwe halali ni mpaka mabunge yote yaridhie. Zanzibar Hakuna kikao kilichokaa kuzungumzia hiyo hati , wala hamna säini ya kukubali. Nilikuwekea clip hapo jussa ameongea yote na kutoa ushahidi . Labda hujapata wakati wa kuisikiliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…