Ogopa kufanya jambo ambalo Nyerere hakufanya

Jinga

So watu zaidi ya milion 60 tuwe tunategemea fikira za mtu mmoja ambaye Tayari ni mfu !?

Hata kama angelikuwa hai bado hazitoshi kusema kwamba Akili zake pekee ndio Akili sahihi kuliko Akili za watu wa Taifa Zima
 
Wewe ulikuwa unaishi pangoni kutojuwa kwamba Kenya walikula sana huo unga wa njano, wakati huo; na hata baadhi ya watu kufa kwa njaa kwenye maeneo kama Turkana na kwingineko?
Ya Turkarna yalikuja baadaye lakini sisi tukinunua sembe la chapa Bibi kutoka Kenya , sukari, unga ngano chapa Atta. Yote kwa magendo na wauzaji wakati mwengine wakiwemo haohao polisi wa Nyerere. Wote njaa tupu. Nchi alianza kuiharibu Nyerere zamani , Sasa ni Cancer.
 
Amka UTAJINYEA.
Hapa hujajijibu hoja zangu, labda nirudie kuuliza maswali yangu kwa lugha nyepesi zaidi.

Nieleweke hivi, kitu kilichokua na faida 1960, 1970 , sio lazima kiwe na faida sasa.

Kwanini nasema hivi, nimeuliza huu muungano kama hauoni una shida na kama ambavyo mleta mada anasema watu wasijaribu kuubadili sababu Nyerere aliona kitu fulani mwaka 1964 ni lazima hicho kitu kiwe hadi sasa kina faida?

Mfano , tunasemaje tuna muungano ilhali muungano ulimeza na kuipoteza identity ya Tanganyika ila ya Zanzibar ikabaki?

Leo hii ukikutana na mzanzibar nje ya nchi atajitambulisha kama ni mzanzibar kuliko kujitambulisha kama mtanzania , sasa je huyu mtanzania halisi ni wa wapi?

Mzanzibar anaweza kushika nafasi za udiwani, ubunge, uwaziri, makamu wa rais na hata rais ila mtanganyika huyu aliyepotezwa identity yake hawezi kuwa hata sheha [diwani] pale Zanzibar.

Tunavyoongea sasa mtu wa kutoka bara[Tanganyika iliyopotezwa kihuni na kuitwa bara] hawezi kumiliki kiwanja kule Zanzibar ila mzanzibar anaweza kwenda Tangayika akajizolea maelfu ya hekari.

Ajira zinazotoka katika taasisi za Zanzibar hazimpi nafasi mtanganyika wa kiwango kile kile cha elimu kuweza kushindana na mzanzibar bali zile ajira zinaenda kwa wazanzibar 100% huku ajira za watangayika[wanaoitwa wa bara] zikitolewa wazanzibar wanaweza kuja kushindana na watanganyika kujipatia ajira zile zile kule Zanzibar ila zimewekwa tu kwa wazanzibar.

Alichokiongea Saada Mkuya juzi kwamba mtanganyika akiugua Zanzibar hawezi kupewa matibabu kama mzanzibar ina tofauti gani na mtanganyika aliyeugua akiwa Kenya matembezi ambapo hawezi kupewa huduma kama mkenya bali kama mgeni hii haina tofauti na atakachofanyiwa kule Zanzibar ambapo tunasema tumeungana

Mtu akinunua bidhaa Zanzibar akiwa matembezini ili aivushe kwenda Tanganyika[mnayoita bara] atabidi kuilipia ushuru tena!

Nimetoa mifano kadhaa kuonyesha kwa uchache muungano huu nikimaanisha Nyerere hakua mkamilifu na alichokiwaza 1960's pengine kilikua na manufaa kwa zama hizo ila sio lazima kiwe nayo sasa hivyo kwenye makosa atakosolewa na dawa ya kosa ni kujisahihisha sio kupiga propaganda.

Hivyo tusijikite kwenye kila alichoanzisha Nyerere basi tukaamini na kusema hatuwezi kukibadili sababu tu alianzisha Nyerere, sote ni mashahidi tulivyoona sera ya ujamaa ilivyofeli katika utawala wake hivyo kuna mengi alikua sahihi na kuna mengine alichemka pakubwa tu likiwemo hili la muungano uliowaachia wazanzibari identity yao na ukapoteza identity ya watanganyika.

Miaka ile ya 1970, 1980, 1990 na 2000 mwanzoni simu ya aina hii iikua nyenzo kubwa ya mawasiliano ila kwa sasa unaweza kuzunguka katika eneo lako uitafute hii simu unaweza usiipate, jibu ni kwamba njia zilzotumika miaka hiyo zilifaa kwa wakati huo ila kwa sasa njia zipo nyingi hata unaweza kufanya mawasiliano sio tu kwa kuongea kama ilivyokua kwa aina hii ya simu bali kwa teknolojia ya sasa unaweza kuongea na hata kuonana na mtu maelfu ya maili kutoka ulipo.
depositphotos_152199626-stock-photo-retro-black-telephone.webp
 
Ktk Africa sijaona rais aliye hai au aliyekufa ambaye alikuwa na Nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo wenzake wakati yeye akibakia vilevile akiridhika na vichache alivyonavyo.
Yeyite anayemponda Nyerere au atakayekuja kumponda Nyerere kwa makosa mengi ambayo ni irrelevant ni mvivu wa kufikiri au ni opportunist ambaye anaamini akifanya hivyo itamsaidia kwa mazingira yake ya kipato kama baadhi ya watu ktk huu uzi
Kagame ni tofauti
 
Hapa hujajijibu hoja zangu, labda nirudie kuuliza maswali yangu kwa lugha nyepesi zaidi.

Nieleweke hivi, kitu kilichokua na faida 1960, 1970 , sio lazima kiwe na faida sasa.

Kwanini nasema hivi, nimeuliza huu muungano kama hauoni una shida na kama ambavyo mleta mada anasema watu wasijaribu kuubadili sababu Nyerere aliona kitu fulani mwaka 1964 ni lazima hicho kitu kiwe hadi sasa kina faida?

Mfano , tunasemaje tuna muungano ilhali muungano ulimeza na kuipoteza identity ya Tanganyika ila ya Zanzibar ikabaki?

Leo hii ukikutana na mzanzibar nje ya nchi atajitambulisha kama ni mzanzibar kuliko kujitambulisha kama mtanzania , sasa je huyu mtanzania halisi ni wa wapi?

Mzanzibar anaweza kushika nafasi za udiwani, ubunge, uwaziri, makamu wa rais na hata rais ila mtanganyika huyu aliyepotezwa identity yake hawezi kuwa hata sheha [diwani] pale Zanzibar.

Tunavyoongea sasa mtu wa kutoka bara[Tanganyika iliyopotezwa kihuni na kuitwa bara] hawezi kumiliki kiwanja kule Zanzibar ila mzanzibar anaweza kwenda Tangayika akajizolea maelfu ya hekari.

Ajira zinazotoka katika taasisi za Zanzibar hazimpi nafasi mtanganyika wa kiwango kile kile cha elimu kuweza kushindana na mzanzibar bali zile ajira zinaenda kwa wazanzibar 100% huku ajira za watangayika[wanaoitwa wa bara] zikitolewa wazanzibar wanaweza kuja kushindana na watanganyika kujipatia ajira zile zile kule Zanzibar ila zimewekwa tu kwa wazanzibar.

Alichokiongea Saada Mkuya juzi kwamba mtanganyika akiugua Zanzibar hawezi kupewa matibabu kama mzanzibar ina tofauti gani na mtanganyika aliyeugua akiwa Kenya matembezi ambapo hawezi kupewa huduma kama mkenya bali kama mgeni hii haina tofauti na atakachofanyiwa kule Zanzibar ambapo tunasema tumeungana

Mtu akinunua bidhaa Zanzibar akiwa matembezini ili aivushe kwenda Tanganyika[mnayoita bara] atabidi kuilipia ushuru tena!

Nimetoa mifano kadhaa kuonyesha kwa uchache muungano huu nikimaanisha Nyerere hakua mkamilifu na alichokiwaza 1960's pengine kilikua na manufaa kwa zama hizo ila sio lazima kiwe nayo sasa hivyo kwenye makosa atakosolewa na dawa ya kosa ni kujisahihisha sio kupiga propaganda.

Hivyo tusijikite kwenye kila alichoanzisha Nyerere basi tukaamini na kusema hatuwezi kukibadili sababu tu alianzisha Nyerere, sote ni mashahidi tulivyoona sera ya ujamaa ilivyofeli katika utawala wake hivyo kuna mengi alikua sahihi na kuna mengine alichemka pakubwa tu likiwemo hili la muungano uliowaachia wazanzibari identity yao na ukapoteza identity ya watanganyika.

Miaka ile ya 1970, 1980, 1990 na 2000 mwanzoni simu ya aina hii iikua nyenzo kubwa ya mawasiliano ila kwa sasa unaweza kuzunguka katika eneo lako uitafute hii simu unaweza usiipate, jibu ni kwamba njia zilzotumika miaka hiyo zilifaa kwa wakati huo ila kwa sasa njia zipo nyingi hata unaweza kufanya mawasiliano sio tu kwa kuongea kama ilivyokua kwa aina hii ya simu bali kwa teknolojia ya sasa unaweza kuongea na hata kuonana na mtu maelfu ya maili kutoka ulipo.
View attachment 3613239
Kama hoja yako ni Muungano.

Kwanza kuungana halijawahi kuwa jambo baya.

Pili, kwasasa tuna leadership crisis kiasi kwamba hata matatiO kidogo tumeshindwa kutatua, bara na Unguja.

Na huo upumbavu wa kushindwa kutatua hizo changamoto ndio kutavunja huo Muungano wenyewe.
 
Ya Turkarna yalikuja baadaye lakini sisi tukinunua sembe la chapa Bibi kutoka Kenya , sukari, unga ngano chapa Atta. Yote kwa magendo na wauzaji wakati mwengine wakiwemo haohao polisi wa Nyerere. Wote njaa tupu. Nchi alianza kuiharibu Nyerere zamani , Sasa ni Cancer.
Wewe umekwishaeleza matatizo yako ni kuhusu nini na Nyerere; haya yote unayoeleza hapa ni gfheresha tu ya kusukuma ajenda ileile moja.

Sasa unataka nipoteze muda na maswala ya pembeni zaidi kuliko hayo yanayokuhusu mwenyewe.
Unafikiri huo muda wa kupoteza ninao?

Ajenda yako inajulikana, ni ya kipumbavu.
 
Kama hoja yako ni Muungano.

Kwanza kuungana halijawahi kuwa jambo baya.
Kwa wakati huo pengine lilikua ni zuri ila matatizo yake nayaona ni mengi kwa sasa.
Pili, kwasasa tuna leadership crisis kiasi kwamba hata matatiO kidogo tumeshindwa kutatua, bara na Unguja.
Na chanzo chake sio muungano ni sheria mama [katiba]
Na huo upumbavu wa kushindwa kutatua hizo changamoto ndio kutavunja huo Muungano wenyewe.
Mimi naona uvunjike maana matatizo yake ni mengi na kwa muda mrefu yameshindwa kutatulika suluhu waliyobaki nayo ni "tutaulinda kwa gharama yoyote" kauli hiyo ya gharama yoyote ni mtutu wa bunduki uliopambwa tu kwa maneno mepesi.

Sasa kama kitu kinalindwa na mtutu wa bunduki kina faida gani?
 
Kama hoja yako ni Muungano.

Kwanza kuungana halijawahi kuwa jambo baya.

Pili, kwasasa tuna leadership crisis kiasi kwamba hata matatiO kidogo tumeshindwa kutatua, bara na Unguja.

Na huo upumbavu wa kushindwa kutatua hizo changamoto ndio kutavunja huo Muungano wenyewe.
Mimi nitakwenda kumuuliza 'mkuu 'Matrix' moja kwa moja swali; kwa sababu ninamwelewa kiasi cha kutosha.
Swali lenyewe ni hilo hilo la Muungano.
Hivi Muungano uliopo leo, lengo lake ni lile lile kama lilivyokuwa linategemewa wakati muungano unaasisiwa?

Nyerere angerudi leo, angesemaje kuhusu muungano huu ulivyo sasa; kwamba ulisimamiwa vyema na kuelekea katika maono yaliyokuwepo wakati ule?

Mkuu 'Matrix' kaandika mengi hapo; ngoja nikamsome vizuri huko alikoanzia.
 
Nyerere aliacha NCHI MOJA, SERIKALI MBILI.

Leo tuna NCHI MBILI, SERIKALI MBILI kwasababu ya akili ndogo, tunatafuta kuwafurahisha wanasiasa kutoka Zanzibar.
 
Nieleweke hivi, kitu kilichokua na faida 1960, 1970 , sio lazima kiwe na faida sasa.
Unaweza kusema Tanganyika kuwa huru 1961", kwa sasa uhuru huo hauna manufaa? Hii ni kukupa tahadhari tu kwamba usijumuishe mambo kwa sababu tu uongozi uliofuata ulivuruga lengo lililokusudiwa toka mwanzo.

Kuweka juhudi katika kukuza umoja wa kitaifa wa waTanzania (waTanganyika ukipenda); badala ya kushikilia makabila au dini hiyo miaka ya mwanzo; tunaweza leo kusema kwenye mambo ya kileo swala hilo halikuwa na faida?

Labda niishie tu hapo katika kujibu hicho kipande kidogo kabla sijaendelea na hayo mengine uliyoandika huko chini ili kuepuka mikanganyiko.
 
Nyerere aliacha NCHI MOJA, SERIKALI MBILI.

Leo tuna NCHI MBILI, SERIKALI MBILI kwasababu ya akili ndogo, tunatafuta kuwafurahisha wanasiasa kutoka Zanzibar.
Mwambie, mkuu 'Matrix'; hata sijui kwa nini leo kashikilia maswala ya aina hii?
 
Kagame ni tofauti
Kagame is involved in killing spree of his own people up to this century!
Kagame is operative who cares not for his feelow Africans ndo ulimnganishe na mtu aliyejitoa kwa ajili ya uhuru wa wengine. Aisee hizi ni dharau kwa mwalimu.
 
Kwanini nasema hivi, nimeuliza huu muungano kama hauoni una shida na kama ambavyo mleta mada anasema watu wasijaribu kuubadili sababu Nyerere aliona kitu fulani mwaka 1964 ni lazima hicho kitu kiwe hadi sasa kina faida
Unachozungumzia wqewe kinaeleweka.
Unazungumzia muungano mbovu walioutengeneza waliofuata baada ya Nyerere.
Nyerere hakutengeneza huu muungano mbovu tulionao leo; hii ndiyo hoja muhimu ya kuizingatia hapa.

Lengo la muungano lilikuwa ni kuwaleta watu pamoja, siyo kuwatenganisha.

Muundo ulioassisiwa ulikuwa na lengo hilo la kuwaleta pamoja; lakini baada ya Nyerere, ajenda kuu ikawa ni kutumia njia hizo za kutuunganisha na kuzibadili kuwa za kututenganisha.
 
Nyerere mwanzilishi wa Taifa huru la Tanzania toka Tanganyika na Zanzibar.

Kama kuna jambo hakulifanya tukaja kulifanya sisi.

Tufikiri mara mbili.

Pamoja na kuwa mzaliwa wa Mkoa wa Mara, hakufikiri hata kujenga Airport Mbuga ya Serengeti.

Ila sasa sisi wajanja kumzidi tunataka kujenga.

Kitatulamba.
Kizazi kinajenga barabara hata kwenye mikondo ya maji
 
Wewe umekwishaeleza matatizo yako ni kuhusu nini na Nyerere; haya yote unayoeleza hapa ni gfheresha tu ya kusukuma ajenda ileile moja.

Sasa unataka nipoteze muda na maswala ya pembeni zaidi kuliko hayo yanayokuhusu mwenyewe.
Unafikiri huo muda wa kupoteza ninao?

Ajenda yako inajulikana, ni ya kipumbavu.
Mbona nakujibu kile ulichokiandika au umesahau uliandika nini ? Uliandika hivi :-

Wewe ulikuwa unaishi pangoni kutojuwa kwamba Kenya walikula sana huo unga wa njano, wakati huo; na hata baadhi ya watu kufa kwa njaa kwenye maeneo kama Turkana na kwingineko?
 
Alichokiongea Saada Mkuya juzi kwamba mtanganyika akiugua Zanzibar hawezi kupewa matibabu kama mzanzibar ina tofauti gani na mtanganyika aliyeugua akiwa Kenya matembezi ambapo hawezi kupewa huduma kama mkenya bali kama mgeni hii haina tofauti na atakachofanyiwa kule Zanzibar ambapo tunasema tumeungana
Sasa niambie mkuu 'Matrix', kwa heshima kubwa niliyonayo; kweli huu ndio Muungano aliotegemea Nyerere wakati kunakuwepo na Muungano? Tuseme tu ukweli, leo hii akirudi atasema muungano umefana sana kama lilivyokuwa lengo la mwanzo?

Tumulaumu Nyerere kwa matokeo haya?
 
Unachozungumzia wqewe kinaeleweka.
Unazungumzia muungano mbovu walioutengeneza waliofuata baada ya Nyerere.
Nyerere hakutengeneza huu muungano mbovu tulionao leo; hii ndiyo hoja muhimu ya kuizingatia hapa.

Lengo la muungano lilikuwa ni kuwaleta watu pamoja, siyo kuwatenganisha.

Muundo ulioassisiwa ulikuwa na lengo hilo la kuwaleta pamoja; lakini baada ya Nyerere, ajenda kuu ikawa ni kutumia njia hizo za kutuunganisha na kuzibadili kuwa za kututenganisha.
Hilo halikuwa Katu ajenda ya Nyerere , ajenda ya Nyerere Kama unatafuta ukweli soma hapa:-..

Mbona nakujibu kile ulichokiandika au umesahau uliandika nini ? Uliandika hivi :-

Wewe ulikuwa unaishi pangoni kutojuwa kwamba Kenya walikula sana huo unga wa njano, wakati huo; na hata baadhi ya watu kufa kwa njaa kwenye maeneo kama Turkana na kwingineko?
Sasa umenijibu nini; kwamba Kenya hawakuwa na matatizo wakati huo?

nilikuuliza kama uliishi pangoni, kwa sababu inaonyesha unajisahaulisha tu kutojuwa kwamba matatizo yalikuwa ni ya mtikisiko wa hali ya uchumi wa kidunia ukichangiwa na hali mbovu ya hali ya hewa, kupanda kwa mafuta na vita Mashariki ya Kati.
Yote haya wewe hukuyaona kwa vile ulikuwa pangoni.
 
Hilo halikuwa Katu ajenda ya Nyerere , ajenda ya Nyerere Kama unatafuta ukweli soma hapa:-..

Kwa hiyo leo unapata ushahidi kuwa sababu ya muungano ilikuwa ni uislamu wa Zanzibar!
Nyerere angewezaje kuuondoa uislam Zanzibar?

Mtu unayeamini hivi kuna njia yoyote kweli ya kukuondoa katika fikra za aina hii, kama siyo kupoteza muda tu!
 
Back
Top Bottom