Ogopa kufanya jambo ambalo Nyerere hakufanya

Ogopa kufanya jambo ambalo Nyerere hakufanya

1.alikuwa mbinafsi kwenye mamlaka ndio sababu ya kujitengenezea katiba ya kumfanya awe mungu mtu mdani ya nchi
2.kubinafsisha mali za taifa kuwa za chama na huku akijua fika zilipatikana kutokana na jasho la wananchi wote bila kujali itikadi za vyama
3.hii ya ziada , hakupenda kupingwa na kupokea challenge ndio maana aliwaweka kizuizini walio pinga sera zake za ujamaa na wengine aliwaua eg.karume

Yapo mengi sana
Ukitaka upewe ila hayo ni kwa uchache tu.
China walifanya hivyo hivyo sasa hivi wako wapi?
 
Ujamaa ndio mfumo bora wa uchumi wa mataifa yote yanayofanya kazi kwaajilinya watu.

Wakati nchi inaanza, tukianza na communism, though tu-kadeviate kwenda kwenye socialism. Na kwajuwa ndiontukikuwa tunaanza, hakukuwa na shida kuwa na TRIAL and ERROR.

Nyerere atabaki kuwaMARKING SCHEME kwasababu alijenga RELI ambayo ina manufaa kwa kila mtu.

Nchi zote zina MISINGI yake. Nyerere aliweka MSINGI.

Unapotaka kujenga msingi tofauti, hakikisha una kichwa na Maadili kuliko Nyerere, na hicho kichwa kwasasa hakipo.

View: https://youtu.be/KAJfYFvB-jk?is=5RpdfMV7ZR7aIITI
 
Baada ya miaka 5 huyo mchina utamkuta na kiwanda cha kusaga nafaka.

Sisi waafrika hatuna uvumilivu ni wazee wa shortcut ambayo kwenye maisha haipo.
Tunao mitaani karibu miaka 10 wanabangaiza hata bodaboda wanashindwa
 
Vipi lile bwawa tufukie?
Kwenye migodi n.k tufukuze wawekezaji wote mpaka tutakapoweza kuchimba wenyewe?
Kama baba yako hakujenga misingi imara ya familia, na wewe utaiga hivyohivyo?
Kwakua West wanaanza kutunanga Inapaswa tuanze mdogo mdogo kufufua viwanda vya ndani.

Bidhaa chache na muhimu ndio tuagize.

Tukifanya hivyo currency yetu itakuwa na nguvu.

Nchi inayojimudu kwa bidhaa za ndani inakuwa ngumu kuipelekesha.
 
Dunia haiongozwi na waliokufa. Hilo liweke kichwani.

Hayo mawazo sijui ya Nyerere, sijui Yesu, sijui Muhamad mara nyingi hutumiwa na watu wajanja kuwadhibiti watu wengi hasa waliotabaka la chini.

Wewe unafikiri watawala wanapofanya maamuzi yao wanakumbuka hata kulikuwa na Nyerere?
Nyerere utamsikia wakiwa majukwaani tuu.

Ukishakufa umekufa mkuu. Waliohai wanauhuru wa kuamua watumie mawazo yako au mawazo yao au mawazo yoyote.
Watu wenye akili siku zote tunarejea mantiki, hekima na busara zilizotolewa na watu walioishi zamani. Kwa mfano, ili kuielewa demokrasia na athari zake tunarejea maandishi ya kina Plato, Socrates n.k. Vivyo, katika masuala
mbalimbali ya maisha.

Be clear, waliokufa hawawezi kuongoza (in person). Lakini fikra zao zinaweza kuwa na uhai mkubwa sana kwa vile zinawakilisha ama facts, mantiki, logic na busara/hekima vitu ambavyo visipozingatiwa vinaweza kuleta athari mbaya. Huwezi kuzipuuza ukabaki salama.

Hivyo muulize mleta mada atueleze ni hoja ipi anayotuletea kuhusu umuhimu au ulazima wa kuzingatia mambo aliyofanya au ambayo hakufanya Nyerere. Great thinkers tutatumia critical thinking kuchambua kama hiyo hoja inasimama (ina mashiko) au ndio ule muendelezo wa fikra za kishirikina katika siasa za nchi hii. Manake kuna watu wengi nchini wanaoamini kuwa kuna viongozi fulani walio hai na waliofariki ni miungu au malaika.
 
China walifanya hivyo hivyo sasa hivi wako wapi?
Haya china ipo huko, tanzania iko wapi? Unadhani tanzania inahitaji siasa za kuuana ili mchi isonge mbele? TanzNia inahitaji viongozi makini wasio wabinafsi wenye maono na mipango kwa maslahi ya taifa na sio mipango ya kuziboresha familia zao kama ilivyo sasa, kikwete anapambana mwanae awe raisi na kama si mwanae basi timu yake ili amlindie ushenzi wake , samia anapambana kuweka wazanzibar wamlindie ushenzi wake, huku bado kina nchimbi ,kina makonda , kinamwigulu hao wote wanapambania uongozi wa nchi sio kwa maslahi ya nchi na wananchi wake ila ni kwa maslahi mapana ya kwao na jamaa zao, nchi ikija kupata kiongozi mwenye uzalendo wa dhati kabisa utaona itakavyo songa
 
Kwakua West wanaanza kutunanga Inapaswa tuanze mdogo mdogo kufufua viwanda vya ndani.

Bidhaa chache na muhimu ndio tuagize.

Tukifanya hivyo currency yetu itakuwa na nguvu.

Nchi inayojimudu kwa bidhaa za ndani inakuwa ngumu kuipelekesha.
Wakufufua viwanda nani? Na kwa usimamizi upi? kama wezi wa mali za uma wanalindwa kwa mtutu wa bunduki, shirika la ndege linatushinda, reli inatushinda ,bandari imetushinda hadi tumegawa kwa wajomba, unadhan kuna wa kuweza kuinua huo uchumi na viwanda? Atoke wapi? nchi hii bila kuweka misingi thabiti ya kuwajibishana kikatiba kuanzia kumuwajibisha Rais kisha watu wake wa chini nchi haitatoka hapa kabisa na itazidi kuzama, kila kiongozi akiingia ananyanyua mabega mana katiba inamlinda hivyo hata watu wake wa karibu wakiharibu wanajifichia kwake yaani kushughulika na wabadhirifu ni hadi rais aamue asipo amua yeye kwa kuwa ni watu wake basi hakuna mamlaka ya kumuwajibisha sasa nchi unataraji itasinga vipi kwa propaganda za kula siku, nchi kila mwaka ipo kwenye vita ya kupigania madaraka hayo maendeleo yatoke wapi.
 
1.alikuwa mbinafsi kwenye mamlaka ndio sababu ya kujitengenezea katiba ya kumfanya awe mungu mtu mdani ya nchi

Huwezi kusema mbinafsi, halafu hayo madaraka hayakuwa kwa manufaa yake.

Nchi changa yenye ukabila, udini, daktari mmoja, vita baridi.

Alitakiwa kufanyaje?

Toa altenative
2.kubinafsisha mali za taifa kuwa za chama na huku akijua fika zilipatikana kutokana na jasho la wananchi wote bila kujali itikadi za vyama
3.hii ya ziada , hakupenda kupingwa na kupokea challenge ndio maana aliwaweka kizuizini walio pinga sera zake za ujamaa na wengine aliwaua eg.karume
Hakuna mali za taifa zolizobinafsishwa kuwa za chama.

Huu mi uzamwamwa.

Malimza CCM.ni zile zilizokuwa za chama wakati wa chama kimoja.

Mali zilizobinafsishwa zilikua za taifa, siyo chama.

Taja hiyo mali moja iliyobinafsishwa ikawa ya chama.
Yapo mengi sana
Ukitaka upewe ila hayo ni kwa uchache tu.
Mengi yapi?
 
Nyerere mwanzilishi wa Taifa huru la Tanzania toka Tanganyika na Zanzibar.

Kama kuna jambo hakulifanya tukaja kulifanya sisi.

Tufikiri mara mbili.

Pamoja na kuwa mzaliwa wa Mkoa wa Mara, hakufikiri hata kujenga Airport Mbuga ya Serengeti.

Ila sasa sisi wajanja kumzidi tunataka kujenga.

Kitatulamba.
Tulioshuhudia mazishi yake kwa sinema za vijijini tumekupata
 
Nyerere mwanzilishi wa Taifa huru la Tanzania toka Tanganyika na Zanzibar.

Kama kuna jambo hakulifanya tukaja kulifanya sisi.

Tufikiri mara mbili.

Pamoja na kuwa mzaliwa wa Mkoa wa Mara, hakufikiri hata kujenga Airport Mbuga ya Serengeti.

Ila sasa sisi wajanja kumzidi tunataka kujenga.

Kitatulamba.
Huwa anatokea na kuwaeleza mapya ya kufanya.?
  • kwamba aliyosema yakiisha utakuwa mwisho wa kutenda?
  • anasubiriwa marehemu kutoa mwongozo?
 
Tumefika hapa kwasababu tunadhani tuna akili sana kuzidi Nyerere.

Alifuta Machief, sisi tuko busy na siasa na Machief.

Aliheshimu kura, sisi tunataka shortcut za kuengua watu.
Angeheshimu kura asingefuta UPINZANI baada ya Uhuru..
 
Mkuu ungeweka hapa hayo mambo ambayo Nyerere hakuyafanya ili na sisi tusiyafanye kama unavyo shauri,

Mfano Nyerere hakutumia WhatsApp na Instagram,kwahiyo na sisi tusitumie?
 
Back
Top Bottom