Ogopa sana aina ya watu wanaozungumza na kila mtu

Ogopa sana aina ya watu wanaozungumza na kila mtu

Ni kitabu kizuri ukiwa USA kwa huku kwetu manufaa yake ukutane na watu walio kama wewe
Kitabu kina mazuri na mapungufu yake. Hicho kitabu wanakitumia watu wote hasa hasa wafanya biashara wanasiasa watu wa usaili n.k

Inategemea na interest zako mkuu
 
Hayo mambo ya keep your friends close and your enemies closer. Ndo unafiki wenyewe! Na wengi hufanya for a purpose na si bure!

Unachanganya madesa Mkuu..
Usimuamini kila mtu, hii haimaanishi we ni mnafiki, hapana! Inamaanisha unaelewa namna akili za watu zinavyofanya kazi.. na unatambua kwamba hakuna alie sahihi 100% na wew ukiwemo..
Ila Wewe ndo unajua unataka nini kwa wakati gani na kwanini.. sasa hebu nambie kipi bora kushughulika na watu usiowajua ama kushughulika na nafsi yako unayoijua vizuri..??
Hakuna cha Bure dunia hii..
 
Huyo shetani kuna Time anasogoa na Mungu na wanapanga jinsi ya kukutesa itakua sisi binadamu 😹😹

Una wazimu wewe ishi maisha yako
 
Kikubwa Tu hapa duniani usikanyage njia za watu kupata HELA..hela ndo kitu utajichanganya ila sio maneno....ongea vzr na kila mtu ila usitake kuchunguza na kuchungulia wapi anapata mkate wake wa kila siku hapo mtavurugana..Siri ndo imelala hapo ila kuhusu maneno hamnaga Noma..hapa stori Tu kula kwenu
 
Hahahahahah na ndio waTanzania wengi walivyo.Ukimkuta na mhusika wanacheka hatari hadi wanagonga mikono akigeuka utaskia"Yule sio mtu kabisa" unabaki kushanga nyinyi si ni mlikuwa mnacheka wote hadi jino la mwisho linaonekana?
 
Muogope sana mtu anayetafuta kupendwa na kila mtu , mtu aina hiyo lazma atavaa vazi la unafiki ili aweze kuwaingia watu

Unakuta mtu ofisini /mtaani anazungumza na kila mtu , hata maadui wasiopatana yeye pande zote yupo .

Watu wa aina hiyo wabaya sana atabeba ya huku atapeleka kule na ya kule atayaleta huku vice versa
Sasa kama ofisini kiongozi asipoongea na kila mtu kazi zitafanyikaje?
 
Muogope sana mtu anayetafuta kupendwa na kila mtu , mtu aina hiyo lazma atavaa vazi la unafiki ili aweze kuwaingia watu

Unakuta mtu ofisini /mtaani anazungumza na kila mtu , hata maadui wasiopatana yeye pande zote yupo .

Watu wa aina hiyo wabaya sana atabeba ya huku atapeleka kule na ya kule atayaleta huku vice versa
Mimi ni mmoja wa hao watu...nadhani umekutana na mtu wa aina tofauti tu.

Nazungumza na kila mtu. Unaweza kukuta A anaugomvi na B lakini nitazungumza na B na A bila tatizo lolote.

Na ili pasiwepo na Umbea topics zangu ni aidha mpira, siasa, kusafiri, magari na biashara.

Lakini watu wa aina yenu mnaopenda kujadili watu ukiniona unadhani tunakusema wewe.

Siwezi kugombana na A kisa hana maelewanao mazuri na B. Hayo hayanihusu na ugomvi wao hauhusiani na mimi hata kidogo.
 
Back
Top Bottom