Tormenter
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 427
- 808
Yule uliemuua ili uchukue pesa zake pale benki..
Ndugu zake walimzika kwa vilio, na Dunia nzima ililaani kitendo kile..
Yule bondia mwenzio ulingoni, uliempiga mpaka akazimia..
Mkewe alipiga kelele akiwa nje, na kusema bado yupo pamoja na mumewe..
Yule rafiki yako mwanfunzi mburula, uliyembagua kwenye vikao na discussion na vipanga wenzio,
Wazazi wake walimpongeza kwa alama chache alizopata, na kumpa moyo asome kwa bidii..
Yule Mbeba zege uliempa kazi, kisha ukamcheleweshea hela yake makusudi..
Familia yake ililala njaa, lakini bado asubuhi, walimuombea tena dua mtafutaji wao..
Ile kesi aliesingiziwa yule maskini asiejiweza, ili waliotenda waendelee kubaki uraiani.
Ndugu zake walimsubiri hadi alipotoka jela, na kumwambia wapo pamoja nae, aanze upya maisha yake..
Kama nguvu na uwezo wako, havikupi kundi kubwa la watu, watakaokutetea ukiwa hujiwezi, badilika..
Unaweza kushinda ndani ya uwanja, wengine wakashinda nje kwenye MAISHA YA KWELI..
Mmonaga kundungu, kumeyo mwanja