Ole Sabaya akamatwa pamoja na mabaunsa wake. Ahojiwa na Vyombo vya Dola

Ahojiwe hata mwaka mmoja akiwa hukohuko ndani asitoke nje akaharibu ushahidi
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza huyu TUJITEGEMEE ni nani? Kumbe na wewe umo! Pole sana na yanayokukumba baada ya mwendazake kuwaacha yatima. Jipige moyo ndugu yangu, Sabaya hakuwa peke yake...mko wengi. I feel your pain...!
Mkuu achana naye huyo mtu wa kitengo changanyikiwa.
Sisi tulalishukuru jeshi, JWTZ, kwa kuiletea nchi heshima kwa kutetea katiba na Mama kuingia madarakani.
Wangeendekezwa hawa kina TUJITENGEMEE, ingekuwa chaos nchini.
 
Kwahiyo 2045 atakayechaguliwa naye akiwa genge la akina Sabaya anaweka ndani akina Hamduna.
Tunaenda wapi?
Si " Imeandikwa"
Kisasi ni chake Bwana atalipa?
Kwani hamduni kamuonea nani umesikia?
 
Kumbe unalijua hilo kuwa mahakama ndiyo ina mamlaka ya haki kutoa hukumu, sasa imekuwaje tena kuita watu majambazi bila udhibitisho kisha kuamuru watu hao wafungwe!? Sasa kwa pamoja tujiulize umepanic bila kutumia akili ama umeelewa mwenzetu?!
Huyu anatakiwa afungwe jiwe kubwa la kusagia shingoni mwake akatupwe ferry hata mahakamani asipelekwe ushahidi wa cctv upo
 
Kamanda Hamduni leo ni siku ya sita(6) toka uthibitishe kumkamata Olesabya na wenzie kwa tuhuma zisizo julikana maana hazijawekwa wazi kabisa. Kwa tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa na watu mbali mbali dhidi ya Ole Sabaya tulitegemea hadi sasa ameshafikishwa mahakamani lakini si kukaa mahabusu...

Kwakuwa zimeshapita siku zaidi ya tatu ni wazi hakuna mlichonacho dhidi ya Sabaya na pengine watu wameshindwa kutoa ushahidi wa kilicho kuwa kinaongelewa na watu. Ni vyema akaachiwa huru msiogope kusema maana Mama kasema wazi msiogope kuachana na case ambazo hazina ushahidi.

Takukuru mnavyomchelewesha Ole Sabya kumfikisha mahakamani mnategeneza mianya ya kumbabikia case maana kwa tuhuma zilizokuwa zinatolewa dhidi ya Sabaya inakuwaje hadi sasa hamjamfikisha mahakamani na watu wanasema wana ushahidi?

Mnakwama wapi? basi muachieni huru.

Tamko la mkurugenzi wa Takukuru

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Kamishna wa Polisi Salum Hamduni AMETHIBITISHA kuwa wanamshikilia aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kwa maojiano tangu May 25 mwaka huu. Kamishna Hamduni amesema Sabaya hakukamatiwa Arusha kama vyombo mbalimbali vya habari vilivyoripoti, bali alikamatwa jijini Dar akiwa na watu wawili waliotambuliwa kuwa ni "mabaunsa" wake na wote wapo mahabusu kwa mahojiano. Amesema wanaendelea kuhojiwa na wakipatikana na kesi ya kujibu watafikishwa mahakamani!

Nitafurahi sana mkiwatetea na masheikh wa UAMSHO kama ambavyo mnavyowatetea wanasiasa n.k. Ndio kwanza hajafikisha hata wiki huyu ndugu yenu mmeanza kelele zenu, UAMSHO wana 8 years na ushee huko gerezani lakini mnajifanya kusilent.

Acha mahakama itende haki, si tu kwa sabaya bali kwa wote., japo kwa masheikh hawakuwatendea haki mpaka wa leo, Allah atawalipa kwa dhuluma wanayofanya.
 
Kamanda Hamduni leo ni siku ya sita(6) toka uthibitishe kumkamata Olesabya na wenzie kwa tuhuma zisizo julikana maana hazijawekwa wazi kabisa. Kwa tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa na watu mbali mbali dhidi ya Ole Sabaya tulitegemea hadi sasa ameshafikishwa mahakamani lakini si kukaa mahabusu...

Kwakuwa zimeshapita siku zaidi ya tatu ni wazi hakuna mlichonacho dhidi ya Sabaya na pengine watu wameshindwa kutoa ushahidi wa kilicho kuwa kinaongelewa na watu. Ni vyema akaachiwa huru msiogope kusema maana Mama kasema wazi msiogope kuachana na case ambazo hazina ushahidi.

Takukuru mnavyomchelewesha Ole Sabya kumfikisha mahakamani mnategeneza mianya ya kumbabikia case maana kwa tuhuma zilizokuwa zinatolewa dhidi ya Sabaya inakuwaje hadi sasa hamjamfikisha mahakamani na watu wanasema wana ushahidi?

Mnakwama wapi? basi muachieni huru.

Tamko la mkurugenzi wa Takukuru

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Kamishna wa Polisi Salum Hamduni AMETHIBITISHA kuwa wanamshikilia aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kwa maojiano tangu May 25 mwaka huu. Kamishna Hamduni amesema Sabaya hakukamatiwa Arusha kama vyombo mbalimbali vya habari vilivyoripoti, bali alikamatwa jijini Dar akiwa na watu wawili waliotambuliwa kuwa ni "mabaunsa" wake na wote wapo mahabusu kwa mahojiano. Amesema wanaendelea kuhojiwa na wakipatikana na kesi ya kujibu watafikishwa mahakamani!
MKUU WA WILAYA ANATEMBEA NA MABAUNSA?
YEYE NIMENEJA WA CASINO.
INAKUWAJE M/KITI WAKAMATI YA ULINZI WILAYA asipewe ulinzi polisi?tena anaagiza tu niletee polisi OCD.
Kwa mazingira hayo SABAYA NI MHUNI WA MITAANI HAKUSTAHILI KUWA DC.
 
Mwamwindi ilikuwa ni jeuri ya kihehe, ', Mgaya siida' kwa waliofanya kazi na mhehe akikutamkia maneno haya jua yupo tayari kwa lolote na hatojutia maamuzi yake kamwe .
.
Kitendo cha kutoka Isimani hadi iringa mjini wakati huo njia ni vumbi, huku akiwa ameubeba mwili wa kleruu kwenye buti ni level nyingine ya ukatili

Inasemekana mwl nyerere alijaribu mara kadhaa Kumtaka akiri kosa ili apunguziwe adhabu , mwamwindi alikataa kata kata
 
Mwamwindi aliyetembeza mapanga kwa rc...?
Gobore !
Ila pia inasemekana kulikuwa na ugonvi wa mapenzi baina ya wawili hao , kuna tetesi kuwa kleruu alikuwa mtu wa mademu , na katika pitapita zake huko iringa mjini aliwahi kupita na mke wa mwamwindi , na mwamwindi alikuwa anafahamu hilo , ni vile wakuu wa mikoa wana nguvu na mamlaka ya kisheria
 
Kamanda Hamduni leo ni siku ya sita(6) toka uthibitishe kumkamata Olesabya na wenzie kwa tuhuma zisizo julikana maana hazijawekwa wazi kabisa. Kwa tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa na watu mbali mbali dhidi ya Ole Sabaya tulitegemea hadi sasa ameshafikishwa mahakamani lakini si kukaa mahabusu...

Kwakuwa zimeshapita siku zaidi ya tatu ni wazi hakuna mlichonacho dhidi ya Sabaya na pengine watu wameshindwa kutoa ushahidi wa kilicho kuwa kinaongelewa na watu. Ni vyema akaachiwa huru msiogope kusema maana Mama kasema wazi msiogope kuachana na case ambazo hazina ushahidi.

Takukuru mnavyomchelewesha Ole Sabya kumfikisha mahakamani mnategeneza mianya ya kumbabikia case maana kwa tuhuma zilizokuwa zinatolewa dhidi ya Sabaya inakuwaje hadi sasa hamjamfikisha mahakamani na watu wanasema wana ushahidi?

Mnakwama wapi? basi muachieni huru.

Tamko la mkurugenzi wa Takukuru

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Kamishna wa Polisi Salum Hamduni AMETHIBITISHA kuwa wanamshikilia aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kwa maojiano tangu May 25 mwaka huu. Kamishna Hamduni amesema Sabaya hakukamatiwa Arusha kama vyombo mbalimbali vya habari vilivyoripoti, bali alikamatwa jijini Dar akiwa na watu wawili waliotambuliwa kuwa ni "mabaunsa" wake na wote wapo mahabusu kwa mahojiano. Amesema wanaendelea kuhojiwa na wakipatikana na kesi ya kujibu watafikishwa mahakamani!

😂 Yeye mbona alikuwa anaweka watu ndani bila makosa afundishwe adabu ili ajue inakuwaje huko ndani mateso yanamrudia
 
Mbinyeni huko huko mpaka awaonyeshe lile panga alilotumia kukata masikio #FREESABAYA 🤸🐒🤣
 
Mei 13, 2021 Rais Samia Suluhu alimsimamisha Lengai Ole Sabaya kuwa Mkuu wa Wilaya na kuamuru uchunguzi dhidi yake. Zaidi soma Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya

Baada ya kusimamishwa kazi, iliripotiwa kuwa Ole Sabaya anapanga kutoroka nchini. Zaidi soma Ole Sabaya apanga kutoroka nchini
View attachment 1800070
Picha: Raia Mwema​

Sabaya mbaroni

ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai ole Sabaya, amekamatwa jijini Dar es Salaam, Raia Mwema limeelezwa.

Taarifa kutoka mkoani Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam zinasema, Sabaya amekamatwa wilayani Kinondoni, mkoani Dar es Salaam, Jumanne iliyopita.

Kwa sasa, bado anahojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU), akituhumiwa kwa mambo mbalimbali, ikiwamo matumizi mabaya ya madaraka wakati akiwa mtumishi wa umma.

Kukamatwa kwa Sabaya, kumekuja takribani wiki mbili tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano, Samia Suluhu Hassani, kumsimamisha kazi Sabaya na kuelekeza kufanyika uchunguzi dhidi yake.

Sabaya anakabiliwa na tuhuma mbalimbali, ikiwamo uporaji wa fedha kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji; ukiukaji wa haki za binadamu, ukatili dhidi ya binadamu na matumizi mabaya ya madaraka.

Aidha, Sabaya anadaiwa kuwaandika barua baadhi ya wafanyabiashara, akitaka wachangie mamilioni ya shilingi, kinyume na sheria na misingi ya utawala bora.

Mtoa taarifa wa gazeti hili amesema, Sabaya alikamatwa na kikosi kazi (Task Force), kinachohusisha taasisi mbalimbali za ulinzi na usalama, kufuatilia kuwapo kwa tuhuma mbalimbali katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Tayari kikosi kazi hicho, kimefanya mahojiano na watu mbalimbali, katika mikoa hiyo na kwamba jana kilikuwa mkoani Kilimanjaro, ambako kilifanya mahojiano na watu kadhaa, wakiwamo wahanga wa uongozi wake.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kabla ya kwenda Kilimanjaro, kikosi kazi hicho, kilifanya kazi kama hiyo, mkoani Arusha, ambako kilipata nafasi ya kuzungumza na viongozi na watendaji, kwa lengo la kukusanya ushahidi wa kutosha dhidi ya Sabaya.

Anasema, wakati Sabaya anakamatwa alikuwa ameongozana na “vijana wake kadhaa,” baadhi yao wakiwa wanahusishwa na matukio mbalimbali ya uhalifu mkoani Arusha na Kilimanjaro.

“Huyu bwana alikuwa na watu kadhaa, wakati anakamatwa. Alikuwa na magari matatu, ambayo yalikuwa katika msafara wake, uliokuwa na vijana wake, wakiwamo mabaunsa wanaomlinda,” kimeeleza chanzo cha taarifa.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Salum Hamduni, amethibitisha Raia Mwema jana Alhamisi, kwamba taasisi yake, inamshikilia Sabaya kwa ajili ya mahojiano yanayotokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Amesema, "ni kweli kuwa Takukuru inamshikilia Sabaya, kwa mahojiano ya tuhuma mbalimbali za matumizi ya madaraka na rushwa, wakati akiwa mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.”

Hata hivyo, Hamduni hakutaka kueleza kuzungumzia kwa undani swala hilo, badala yake alisema, “mara baada kukamilisha upelelezi wetu, tutatoa taarifa rasmi kwa umma.”

Mbali na tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu, Sabaya anakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka, ikiwamo kukusanya mamilioni ya shilingi kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara kwa matumizi yake binafsi.

Katika kutekeleza mradi huo, Sabaya amekuwa akitumia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa fedha hizo zinakwenda kutumika kwa ajili ya shughuli za chama hicho tawala. Wengine waliochukuwa fedha zao, walielezwa kuwa zinatumika kwa ajili ya shughuli za serikali na maendeleo ya wilaya ya Hai.

Lakini taarifa ndani ya gazeti hili zinasema, hakuna hata shilingi iliyokusanywa ilitumika kwa ajili ya maendeleo ya Hai au CCM. Mamilioni yote ya fedha yaliyokusanywa yaliishia kwenye shughuli zake binafsi.

Katika kipindi cha takribani miaka mitatu ya uongozi wake, maisha ya Sabaya yalikuwa yakitawaliwa na anasa na ubabe usioelezeka. Baadhi ya wanaomfahamu wanasema, alikuwa akiishi maisha ya anasa kuliko baadhi ya viongozi wakuu wa serikali.

Sabaya alikuwa akitembea na kundi kubwa la mabaunsa, wanawake warembo na magari ya kifahari. Msafara wake ulikuwa wa magari matatu, moja anapanda yeye, nyingine mabaunsa wake, huku lingine likibeba wanawake warembo.

Pamoja na hayo, alilalamikiwa na baadhi ya watu, kwa uporaji na uvamizi wa maduka na biashara mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Sabaya alipokuwa akifika Arusha, alifikia kwenye hoteli za kitalii na kukodi vyumba viwili vya hadhi ya juu, kimoja akilala yeye, huku mabaunsa wakilala sebuleni kumlinda.

Kama huduma za hoteli hiyo na mandhari havikumfurahisha, alihamia hoteli nyingine, huku akigoma kulipa chochote kwenye hoteli alizokuwa akifikia yeye na watu wake.

“Alikuwa akiandika barua kwa mfanyabiashara au mwekezaji yeyote mwenye fedha, akimtaka achangie kati ya Sh. 15 milioni au Sh. 20 milioni. Akifanya hivi kwa wawekezaji 30, tayari anakusanya mamilioni kwa ajili ya matumizi yake,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Moja ya barua za aina hiyo ni pamoja na ya 18 Januari 2019, aliyomwandikia mmoja wa wawekezaji katika wilaya ya Hai.

Katika barua hiyo, Sabaya alimtaka mfanyabiashara huyo kuchangia Sh. 15 milioni kwa ajili ya hafla ya kutimiza miezi sita ya utumishi wake tangu alipoteuliwa kushika wadhifa wa mkuu wa wilaya na Rais John Magufuli.

Barua hiyo ambayo Raia Mwema imeiona nakala yake, imeeleza kuwa sherehe hiyo inafanyika tarehe 30 Januari 2019, siku ambayo anaitumia kusoma utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Ili kufanikisha shughuli hiyo, kupitia barua hiyo iliyoandikwa kwa Kiingereza, Sabaya anamtaka Mkurugenzi wa kampuni hiyo kuchangia Sh. 15 milioni kwa ajili ya bajeti ya shughuli hiyo.

Taarifa zinaeleza kuwa Sabaya alikuwa akifanya hivyo mara nyingi na mbinu hiyo pia, ilimfanya aishi maisha ya anasa pengine kuliko wafanyabiashara mabilionea nchini.

Mwekezaji Cuthbert Swai, Mkurugenzi wa hoteli ya kitalii ya Weruweru River Lodge, aliwahi kulalamika hadharani, kwamba Sabaya aliwahi kumtisha akitaka apewe mamilioni ya fedha.

Anadaiwa pia kutumia madaraka yake vibaya, kudai na kupokea rushwa ya Sh 10 milioni kutoka kwa mfanyabiashara huyo, ikiwa ni mwendelezo wa tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa na wawekezaji wengine wilayani Hai.

Swai alidai kuwa amekuwa akifanyiwa vitendo kadhaa na Sabaya, ikiwamo kuombwa rushwa ya kati ya Sh milioni mbili na milioni tano.

Pamoja na kutoa mamilioni hayo ya fedha, Swai aliamriwa ndani ya saa 48 kuhamisha akaunti za hoteli ya Weruweru River Lodge kutoka Moshi mjini kwenda Hai.

Swai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Ahsante Tours, alieleza mbele ya Naibu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Msafiri Mbibo, kwamba Sabaya amekuwa akitumia madaraka yake, kunyanyasa wafanyabiashara.

Tangu Sabaya asimamishwe kazi na Rais Samia Suluhu Hassan, amekuwa akiishi kwa kujificha huku vyombo vya dola vikiendelea na uchunguzi dhidi yake.

Alisimamishwa ukuu wa wilaya kwa tuhuma mbalimbali, ikiwamo matumizi mabaya ya madaraka, rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Taarifa zinasema Sabaya yuko Dar es Salaam, akiishi kwa kuhama hoteli moja baada ya nyingine.

Wiki iliyopita, Raia Mwema iliripoti kuwa Sabaya amejichimbia kwenye hoteli moja ya kisasa iliyoko Mbezi Beach, Dar es Salaam.

Juzi, Raia Mwema ilibaini ‘chimbo’ jipya la Sabaya kwenye hoteli isiyo maarufu sana, jirani na Mlimani City.

Aliingia hotelini hapo siku moja baada ya gazeti hili kufichua taarifa za kuwapo kwake kwenye eneo la Mbezi Beach, ambako alikuwa amejichimbia tangu alipotumbuliwa.

Taarifa kutoka hoteli hiyo, zilidai kuwa Sabaya alikuwa katika hoteli hiyo, akiwa amekodi vyumbo vitatu, kimoja kwa ajili yake na vingine viwili kwa matumizi ya mabaunsa wanaomlinda.

“Sabaya yuko hapa hotelini kwetu tangu mwishoni mwa wiki iliyopita, yuko chumba cha juu namba 323, walinzi wake wako chini…,” alisema mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hiyo ambayo jina tunalihifadhi.

Msafara wake, ulikuwa unatumia magari matatu, moja aina ya Harrier na Toyota Land Cruiser V8 zote nyeusi na nyingine ni Toyota Crown, yenye rangi nyeupe.

mwisho

Nani aliyekwambia kakoko kaachiwa wakati yupo ansnyea kopo....

Na sasa deals zao za mafuta zimeibuliwa...
Jiwe angeua hii nchi *****...
Fikiria miaka yote hiyo wameiba mafuta kiasi gani
 
Dah mwendazake alikuwa ni hatari
 
Rais wa sasa ni jinsia ya kike. Kama hizi tuhuma za ubakaji ni za kweli kuhusu wanawake basi Sabaya na marafiki zake are in for a big trouble.

Rais ndio mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, anachokijua ni cha uhakika zaidi.
Mkuu Kuna key witness Wa kuthibitisha haya??
 
Back
Top Bottom