Uchaguzi 2020 Ole Sabaya anategemewa na CCM kumng'oa Mbowe jimbo la Hai

Uchaguzi 2020 Ole Sabaya anategemewa na CCM kumng'oa Mbowe jimbo la Hai

Ole sabaya ni gaidi limejificha CCM. Mmewafunga masheikh wa uamisho mkamuacha sabaya uraiani. sabaya vurugu zote zinazotokea pale zinaratibiwa na yeye
Acha uongo wa kijinga kama angekua gaidi wewe ungekuepo hapa hadi sahizi? Unaongopa kwa faida ya nani?
 
Sabaya ameharibu mashamba ya Mbowe, JPM amemvunjia billcanas na kufanya pawe parking, sasa Mbowe hata kutoa gari la wagonjwa CCM Hai wapo radhi wamama wafe nyumbani kuliko gari lipokelewe, na ikawa hivyo , na bado walionyweshwa mataptap wanashangilia hawajui ndugu zao ndio wanakufa, hii nchi ilishalogwa
Uongo na ukasuku
 
Hiyo ni ndoto yako, hat sie tuliemueka hapo tunajua, Ile sio size ya Mbowe, bali tuliamua kumuweka chakaramu Mmoja asiye na haya hapo hai, ili amsumbue na kumvunjia heshima Mbowe, na anatimiza kazi aliyotumwa.
Mbowe na wewe wote mnaakili sawa na watu wamewachoka
 
Hapo kwenye udhaifu wa Mbowe unaposema hakuna jambo kubwa ambalo amelifanya kwake ningependa uelezee ulitaka afanye jambo gani?

Nahisi umeshindwa kuelezea zaidi hiyo pointi kwasababu siamini kama mbunge anaweza peleka maendeleo jimboni yeye binafsi bila kuungwa mkono na serikali, tena serikali hii inayomchukia Mbowe bila sababu.

Nakusaidia kujua siasa za Kilimanjaro, Ni siasa za Chama na wananchi watapata nini. Kwa taarifa yako Mkoa wa Kilimanjaro ndio Mkoa ambao watu wenye umri zaidi ya miaka 45 , 80% wako CCM.

Hakuna mbunge wa ama CCM au upinzani anaeshinda kwa zaidi ya kura 65%. Kuna solid and patriots CCM members, na solid patriots Chadema. Wapenzi wa CCM kilimanjaro wana mapenzi ya kupitiliza, na Chadema pia.

Kwa hali ya kipesa patriots wa pande zote wanashindana lakini kwa leo hii Patriots wa CCM wana mizigo mikubwa. Idadi ya wazee inaendelea kupungua kila siku na vijana inaongezeka kila siku na ndio ushindi wa kura Chadema ( vijana ).

Neno msilo taka kusikia ni hili: Wenyeji na wakaazi wa kila siku Hai wa wanataka kuingia CCM , Ukweli wa pili: Uongozi wote wa Hai wa madiwani leo hii wapo CCM na karibu wote wameshinda kwa upande wa CCM.

Na uongozi wa mitaa yote leo hii Wilaya ya Hai upo CCM, na wengi wao 79% walikuwa viongozi Chadema. kwa hiyo CCM wanazo bunduki nyingi za mashambulizi kiuelekea kwa Mbowe.

Waliokuwa wakifanya kampeni ya kumuweka Mbowe madarakani leo wamehama. The grassroot mobilizers karibu wote, ama wako CCM au wako controlled na CCM. ( wakifanya kazi CCM wanalipwa, wakifanya kazi CHADEMA wanajitolea, na watani wangu kwa pesaaaaa, wamerogwa na hali huku imebana sana) huu ndio ukweli halisi.

Hii ndio hali halisi na kinyume chake nii kuwafurahisha wana JF.

Leo nipo hapa Machame napandisha watalii.

KWA KUJUA UKWELI UNATUFANYA SIASA ZETU TUNAENDESHA KWA UFAHAMU NA KWA MUONO WA ILIONYOOKA NA SAWA SAWA.
 
Mwaka huu mwanzoni kabisa niliwaambia kuwa Jimbo la Hai ni mojawapo ya Jimbo ambalo litavuta hisia za Siasa za Tanzania, hapa hakuna kulala, ni mwendo wa mahuburi, ngumi na jino kwa jino. Hii Ni kutokana na umuhimu wa Jimbo hili kwa Upinzani na kwa CCM. Kwa Upinzani ndipo anapotokea Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni. Yaani hawatokubali inyeshe mvua liwake jua kupoteza eneo hili kwani itakuwa aibu ya mwaka. Kwa CCM hapa wanataka kumpiga mchungaji na Kondoo watawanyike, wanajua kabisa ukitaka kumuua nyoka gonga kichwani....

NGUVU YA CCM.

Mipango ya Ushindi wa CCM unaanzia Kichwani kwa Ole Lengai Sabaya, yaani CCM kwa ujumla wanategemea Ole Sabaya awasaidie kumngoa Mbowe pale Hai. Sabaya ndiye DC anayeongoza eneo gumu kuliko yote kati ya maDC wote nchini yaani kupewa jukumu la kuongoza eneo ambalo anatokea Kiongozi mkuu wa Upinzani sio kazi ndogo.

Jukumu la pili alilopewa au alilojipa Ni la kuhakikisha Mbowe hashindi Hai jukumu ambalo Ni zito ambalo hata Bashiru Ally Kakurwa hawezi kulibeba.

Sabaya anapambana kweli matokeo yake anaweza kuumia au akaishinda hii vita, lazima impact itakuwa aidha aumie au ashinde. Niliwahi kusema Kama hatopata usaidizi huyu kwa Jasusi Mbowe ataonekana hafai hata U DC. Pale CCM nani anaweza kuja kuwaongoza watu wanaomuita Mbowe kaka na akaeleweka? Mbowe Hai sio Mbunge tu Bali Ni kaka yao Kama wanavyomuita.

Nguvu ya Pili ya CCM Ni kuwa Sabaya anajitahidi Sana kufanya Siasa na watu wa Tambarare. Siasa maendeleo, siku za karibuni tunaona barabara zikichongwa, hospital ikijengwa nk. Sabaya anajitoa sana kuhakikisha image ya Serikali na Chama inaelewaka Hai. Aidha kwa kutumia mbinu nzuri au mipango Michafu lakini anapambana sana.

UDHAIFU WA CCM

Udhaifu CCM ni kwamba imejisahau, wanamtegemea Mkuu wa Wilaya afanye Kila kitu. Haitawezekana peke yake awaletee Ushindi halafu pia Ni kinyume cha Sheria mkuu wa Wilaya kufanya Siasa za wazi. Ndio maana hata waosema ni yeye ametuma watu wamshambulie Lisu hawana ushahidi wa moja kwa moja.

Udhaifu wa pili Ni kwamba CCM Haina network ambayo Mbowe anayo. Nitaelezea hapa chini nitakapokuwa naelezea nguvu za Mbowe.

Udhaifu wa tatu ambao hauonekani Ni Kifo cha Mzee Mengi. At least Mengi alikuwa Ni mmojawapo ya watu ambao walikuwa wanaweza kuwaambia Viongozi wa Dini Jambo wakalisikia, au hata jamii yake (Wachaga) jambo na wakamsikia.

Udhaifu wa nne Mkoa wa Kilimanjaro Ni Mkoa ambao hauna Agenda ya kuombea kura. Yaani hakuna Jimbo ambalo utapata kura kwa kuahidi hospital, Au umeme, au maji au barabara. Hivi Ni vitu ambavyo vipo toka uhuru. CCM Mara nyingi imekuwa ikitumia agenda hizi kuombea kura kwenye majimbo ya Kilimanjaro hizi sio agenda.

NGUVU YA CHADEMA.

Mbowe karelax kabisa sidhani hata Kama anawaza Sana kuhusu Ushindi wake. Nguvu kubwa waliyoanayo Chadema Ni aina ya mgombea waliyenaye. Mbowe kwa Sasa ndiye mhimili wa Siasa za Upinzani nchini.

Uimara wa Pili wa Chadema Hai Ni network ambayo Mbowe anayo. Mbowe anaungwa mkono na taasisi za Kidini lipo chini ya capert na ndio wanaompa nguvu sana, Mbowe anaungwa mkono na wafanyabiashara wengi toka Hai, Mbowe anaungwa mkono na hata baadhi ya wanaccm waliopo Hai.

Uimara wa tatu ni desturi na Mila za Kabila la wachaga. Kabila hili likishamuamini mtu sio rahisi kuwabadili. Hawaogopi kujilipua kwa kitu wanachokipenda. Mbowe anapendwa Sana na jamii yake. Hawa ndio wanaomuitaga Kaka si rahisi kuwabadilisha mtizamo, watakuchekea usoni lakini kwenye Sanduku la kura watakuadhibu tu. Ndio maana Kabila hili linaongoza katika kuendesha Siasa za Upinzani. Ndio Kabila linalotoa Viongozi wengi wa vyama vya Upinzani nchini. Hii Ni hulka yao kwa maana hiyo ukitaka kuwawin lazima Kwanza wakupende na wakuamini.

Uimara wa nne wa Mbowe Ni kulitawala jukwaa kwa Hoja. Ukimruhusu huyu mtu akupige kwa Hoja atakuua kabisa.

UDHAIFU WA MBOWE.

Udhaifu mkubwa wa brother Mbowe hakuna Jambo kubwa ambalo amelifanya kwenye Jimbo lake.

Pili eneo analotokea si rafiki Sana kwa Siasa za sasa. Mbowe anatokea eneo la milimani, Kuna tetesi kuwa eneo la tambarare ambalo Lina watu wengi nao wameanza kuwaza kutoa mtu wao kuwa Mbunge. Hii Ni kwa sababu eneo hili halijaendelea kwa Sana Kama eneo la Milimani hivyo Wana hasira.

Udhaifu wa Tatu Mbowe amejikita zaidi kwenye siasa za kitaifa na kusahau watu wake. Huu ni udhaifu kwa wabunge wengi wa Upinzani.

Swali ninalojiuliza Sabaya atauweza huu Mbuyu ambao umeshindikana Miaka na Miaka?

Ukitaka kumshinda Mbowe kirahisi tenganisha urafiki wake na Kanisa, tenganisha urafiki wake na wafanyabiashara wa Hai. Mwisho kabisa CCM ndani ya Mkoa na nje ya Mkoa wakitaka kushinda Hai wamsaidie Sabaya, peke yake hatoweza.

Ole Mushi
0712702602.
Yaani huyu Ole Mavi Mushi naona akili yake imejaa uchafuu..

Strike 1: Sabaya=Bashite,angalia matokeo ya Kigamboni!Rejection votes!

Strike 2: Mbowe kwa Hai ni Mungu,goodluck beating that!

Strike 3: Mbowe ni Michael Jordan of politics,Sabaya is a toddler in diapers compared to him!

What Sabaya will use?

Stealing votes?

Good luck with that too,Kilimanjaro sio Simiyu.....Muulize Davis Mosha,atakueleza vizuri!
 
Asante...kwanza Mbowe hajatokea milimani, kwao ni Lambo jirani kabisa na Machine Tools(Njiapanda ya Machame)all in all hakuna Ccm itakuja kutawala Hai mpaka dunia inaisha..
Mkuu unazungumza ukiwa wapi, hali ya hapa Machame ni lazima ifanyike kampeni ya kufa mtu mwaka huu. Vinginevyo tegemea matokeo tofauti. If you are from Machame please coma and fight for Mbowe hali sivyo mnavyoaminishwa watu.
 
Mkuu unazungumza ukiwa wapi, hali ya hapa Machame ni lazima ifanyike kampeni ya kufa mtu mwaka huu. Vinginevyo tegemea matokeo tofauti. If you are from Machame please coma and fight for Mbowe hali sivyo mnavyoaminishwa watu.
Mbowe must go
 
Yaani huyu Ole Mavi Mushi naona akili yake imejaa uchafuu..

Strike 1: Sabaya=Bashite,angalia matokeo ya Kigamboni!Rejection votes!

Strike 2: Mbowe kwa Hai ni Mungu,goodluck beating that!

Strike 3: Mbowe ni Michael Jordan of politics,Sabaya is a toddler in diapers compared to him!

What Sabaya will use?

Stealing votes?

Good luck with that too,Kilimanjaro sio Simiyu.....Muulize Davis Mosha,atakueleza vizuri!
Maji utaita mma unazungumzia Mbowe wa 2010 katika siasa za 2020! Umechemka sana
 
Back
Top Bottom