Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Lazima muanze kujiandaa kisaikolojia mjue kbs mmepanga kufanya Nini endapo huyu mnayemuona Ni mtesi wenu hatafungwa..tatizo lenu Ni Moja tu hamuwajui watu wa Kanda ya kaskazini tabia zao...
itamuachia kama sheria inavyo ainisha. nothing less but till then acheni vyombo vya usalama na mahakama vifanye kazi yake
 
Naskia jana kagombaniwa balaa (hata kama amekonda ndani ya wiki tu, ila katackle bado kapo)
 
Wakati wengine wanaangalia uhalifu wa sabaya wewe unaangalia matumizi ya kiswahili.[emoji17]View attachment 1808370
Mkuu haya mashitaka nimeshindwa kuyaelewa, lugha iliyo tumika imeniacha mdomonwazi.....niwe mkweli sijaelewa kitu humo labda unitafsirie.
Tuliambiwa kuwa shughuli za kimahakama zote zitaendeshwa kwa lugha ya Taifa ya kiswahili, sasa sijui wamegoma au?
sidhani tena kama kitatumika.
 
Aliyekuwa mkuu DC wa Hai amesomea mashaka yake sita UHUJUMU UCHUMI UJAMBAZI KWA SILAHA KUTAKATISHA FEDHA NK AMEKWENDA RUMANDE MPAKA TAREHE 18/6/2021

View attachment 1808139
View attachment 1808140
View attachment 1808141

=======

Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kupokea rushwa.

Sabaya ambaye alisimamishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 13, 2021 kupisha uchunguzi alifikishwa mahakamani hapo akiwa amefungwa pingu na baada ya wote kushuka kwenye magari ya polisi, walitakiwa kuchuchumaa na kisha kupelekwa katika chumba maalum na baadaye kuingizwa mahakamani.

Waendesha mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka, Abdallah Chaula na Tresla Garvas mbele ya Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha wamesema Sabaya na wenzake walitenda makosa hayo Januari 20 na Februari 9, 2021.

Kweka amesema Sabaya na wenzake watano anatuhumiwa kwa makosa ya kuunda genge la uhalifu, uhujumu uchumi, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa na utakatishaji fedha ambapo Sabaya alijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mroso mkazi wa kwa Mromboo ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ukwepaji kodi ili amsaidie jambo ambalo ni makosa.

Pia, Sabaya na walinzi wake wawili, Sylivester Nyengu (26) maarufu kicheche na Daniel Mbura (38) wanakabiliwa na makosa mawili ya ujambazi wa kutumia silaha wakidaiwa kuyatenda Februari 9, 2021.

Wanadaiwa walimfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetin na kumuibia Sh390,000 na pia katika eneo la Bondeni jijini Arusha wakitumia silaha, Sabaya na walinzi hao wanatuhumiwa kumpiga, kumtishia silaha na kumpora Ramadhani Ayoub simu na Sh35,000.

Kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana watuhumiwa hao walipelekwa mahabusu Gereza Kuu la Kisongo na kesi hiyo kuahirishwa hadi Juni 18, 2021.
Hana hatia vipi na kuna mashahidi lukuki wa kumtia hatiani!
 
Neno Uzalendo lina maana nyingine labda.
Naomba tuambie we Mzalendo ki vipi?
hao type ya watu hao ambao wengi wameibuka awamu ya jpm. wana definition yao ya uzalendo.
moja ya sababu zao ni kuwa..kiongoz hata akitenda maovu kwa vile ni.mzalendo asiguswe wala kushtakiwa.

wana miss real concept ya uzalendo. uzalendo haumbatani na maovu
 
hao type ya watu hao ambao wengi wameibuka awamu ya jpm. wana definition yao ya uzalendo.
moja ya sababu zao ni kuwa..kiongoz hata akitenda maovu kwa vile ni.mzalendo asiguswe wala kushtakiwa.

wana miss real concept ya uzalendo. uzalendo haumbatani na maovu
Halafu wengi ni wajinga wajinga sana.
 
Mkuu haya mashitaka nimeshindwa kuyaelewa, lugha iliyo tumika imeniacha mdomonwazi.....niwe mkweli sijaelewa kitu humo labda unitafsirie.
Tuliambiwa kuwa shughuli za kimahakama zote zitaendeshwa kwa lugha ya Taifa ya kiswahili, sasa sijui wamegoma au?
sidhani tena kama kitatumika.
kama hujaelewa tafuta wana sheria wakueleweshe. wamejaa humu wengi tu.
tena wanaelewa english safi.

sasa kama ww shida yako ni lugha uko nyuma sana. watu wamefocus kwenye kesi
 
bordeaux city
Basi kama huishi hao..waache wana hai wenyewe.ni watu wazima wale sio wajinga mpaka wamsingizie sabaya. Kuna mabaa, hotels, migahawa, maduka mkubwa, bureau de change na vingine vingi watu wako eneo hili wameshuhudia maovu yake na wameathirirka.

kuna mpaka video za cctvs zinaonyesha jamaa navamia na kundi lake kashika mitutu ya bunduki,lakini aliona hizo video si kitu sababu jpm anamlinda.yani hata angewachukua wapinzani akawachinja mchana kweupe mbele ya jpm hakuna wa kumkamata.

So waache walio huko hai wenyewe yaliyowakuta wanayajua
 
Loh, hana dhamana...unyanganyi wa kutumia silaha!
Kweli kingereza cha mahakamani kigumu, nimetafuta kosa hili uliloeleza kwenye hati ya mashtaka sikuliona bali nimeona kosa moja lilotajwa kuhusika kukiuka sheria mbili.
===
Naomba tafsiri rahisi wa money laundering na mifano yake kama mitatu hivi.
 
Kweli kingereza cha mahakamani kigumu, nimetafuta kosa hili uliloeleza kwenye hati ya mashtaka sikuliona bali nimeona kosa moja lilotajwa kuhusika kukiuka sheria mbili.
===
Naomba tafsiri rahisi wa money laundering na mifano yake kama mitatu hivi.
kweli sisi watanzania wa daraja la chini bado tunasafari ndefu, maaana tuliaminishwa kuwa kiswahili sasa ndio kitakuwa lugha rasmi lkn wapi bwana, japo nasikia kuna sheria zimetungwa lkn sidhani kama zitatekelezwa.
sijui ni kwa masilahi ya nani haswa!
 
kama hujaelewa tafuta wana sheria wakueleweshe. wamejaa humu wengi tu.
tena wanaelewa english safi.

sasa kama ww shida yako ni lugha uko nyuma sana. watu wamefocus kwenye kesi
sasa mkuu, hayo mashitaka si ndio kesi yenyewe? sasa kama mashitaka yenyewe yameandikwa kwa kifaransa wakati mm ni mswahili wa kuzaliwa kweli hapo ni haki?
jamani tuache kubaguana, sisi sote ni watanzania na lugha yetu ni kiswahili sasa kwa nn tunajipendekeza kwenye lugha amabayo sio mali yetu?!
kiswahili ndio kinatuunganisha na sio lugha nyingine.
 
Inashangaza sana DC kujihusisha na matendo maovu kama haya. Hii ni dalili kuwa kwenye awamu ya 5 yalifanyika mambo mengi sana machafu ambayo mengine hayajaripotiwa.

Uongozi wa dhulma mwisho wake huwa mbaya sana
 
Inavyoelekea walikosa ushahidi Kwa tuhuma za hai, wakaona well tusipompeleka mahakamani itaonekana hatujafanya lolote, wakaja na hizo charges , kuteka na kuiba simu ya tekno.

Kuendesha genge la uhalifu, ujambazi wa kutumia silaha.

Aisee.

Rudisha hela ya kumsafisha Sabaya maana hasafishiki, hizo za Hai wanazificha kwani zilikuwa na baraka ya ccm ili washinde uchaguzi.
 
Kigogo anataka kuchomoa battery kwa Kidoti. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
FB_IMG_16228392163282566.jpg
 
Huyo Crimea Ni mfagiaji tu pale ofisi ndogo za lumumba hawezi kuwa na details za mambo yanayoendelea Kwenye chama wala serikalini.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] pedesheee ndama una nini wee lakini?
 
Back
Top Bottom