Ole Sabaya hata kama alikuwa na hatia lakini sio ya unyag'anyi wa kutumia silaha. Hakimu aliyehukumu hana weledi

Team Jiwe kweli mmechanganyikiwa.
Hivi ulituatilia hatua zote za ushahidi mpaka hukumu inatoka?
 
Ok mzee wa legacy, nasikia kilio chako kimesikika na sasa atatumikia miaka kumi tu! Hongera san mzee legacy
 
Huyu jamaa bado atakubishia tu

Idugunde
 

Sabaya lilikuwa jambazi la kutisha lililopewa nguvu zote toka kwa marehemu Magufuli.

Jana nilikuwa Mwanza na afisa mmoja wa Polisi aliyeenda Mwanza kwaajili ya msiba, nikamwambia, 'mtu wenu amehukumiwa miaka 30 jela", akajibu kuwa lile ni jambazi lililoruhusiwa kufanya ujambazi na marehemu, kiasi cha polisi kulazimishwa kushirikiana na jambazi. Akasema, watu hawajui tu, sisi wenyewe tunafurahishwa sana na haya yanayoendelea sasa hivi. Hawa akina Kingai na wenzake, ni kundi hilo hilo la Sabaya. Hawa siyo polisi, ni majambazi yaliyoingizwa polisi halafu yakapewa mamlaka makubwa kuzidi polisi.
 
Sababya na wenzake walikwenda na magari ya serikali kufanya upekuzi juu ya magendo. .
Mkuu dhana ya upekuzi juu ya magendo inashindwa kuwa sahihi kutokana na hao 'wenzake' alioongozana nao. Hawakuwa watumishi wa serikali,hivyo wanakosa uhalali wa kufanya oparesheni za serikali.

Na moja kati yao ( Kati ya hao wenzake) aliiambia mahakama kuwa hakuwahi kuonana wala kufahamiana na mahakama na wamefahamiana baada ya kushitakiwa pamoja. Mahakama ikaja kujiridhisha kwamba walikuwa wanafahamiana na walishirikiana katika oparesheni hizo.

Mkuu,Sabaya hawezi kuchomoka. Kuna kesi ya uhujumu uchumi inayoendelea, kuna uwezekano mkubwa ile pia akatiwa hatiana. Akikata rufaa si jambo jepeai kushinda rufaa za kesi zote mbili na kwa makosa yote.



Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Askari mlinzi benki akiwa na silaha akakwambia ondoka, huwa unamwogopa yeye ama silaha? bona huwa haukatai kuondoka ila mtu akikwambia nipishe kwenye daladala unagoma?
 
Ni sahihi kabisa. Polisi wapo, ndio wenye mamlaka kisheria ya kumkamata mhalifu. Ndio wenye hakinkisheria kuwa na silaha wanapokwenda kumkamata mtuhumiwa, kama ni lazima. Yeye akawachukua majambazi wenzake, akawaacha polisi. Halafu wakapora pesa. Hawa waitwe nani zaidi ya kuwa majambazi?
 
Umekuwa bush lawyer au vipi? Naona unamkosoa hakimu na kusema hana weledi.
 
Tuwekeeni hukumu tuisone humu
 
Hoja hii bado Idugunde haioni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…