Ole Sendeka: Waziri Pindi Chana anataka Simanjiro, Ngorongoro na Longido kuwa Mapori ya akiba. Wamasai hatutakubali kamwe!

Ole Sendeka: Waziri Pindi Chana anataka Simanjiro, Ngorongoro na Longido kuwa Mapori ya akiba. Wamasai hatutakubali kamwe!

Tatizo lipo katika uwasilishaji wa hicho mbunge anachotumwa na kuwa na vielelezo vyote sahihi vya suala husika.
Mwalimu Tulia anajua baadhi ya sheria hufutwa kwa sheria mpya siyo vifungu

Ndio sababu alimuwahi Ole sendeka kabla hajamwaga mboga!

Angekuwa Zitto Kabwe angekomaa naye hadi mwisho kama Buzwagi
 
Alipewa muda wa kutosha na hata angepewa saa nzima bado asingeweza kujieleza vyema kwani vifungu vya sheria havikuwemo kati ya makaratasi yake.

Naibu waziri alijibu kwa hasira kwani alichukulia kama vile serikali inataka kuwaonea wamasai wakati eneo la hifadhi halina watu.

Kuna suala la kizalendo linafanywa na serikali tatizo la watanzania siku zote ni tafsiri potofu kuenezwa kwa haraka kuliko zile sahihi.

..kwa maoni yangu Spika Tulia akimkatisha-katisha kila mbunge anayechangia kama alivyofanya kwa Ole Sendeka hakuna mbunge ataweza kuchangia.

..Ole Sendeka alipaswa aachwe ajenge hoja yake vile alivyokuwa amejiandaa mpa ahitimishe mchango wake.

..baada ya hapo Naibu Waziri naye angepewa nafasi kuisafisha serikali kwa kupangua hoja na vifungu alivyowasilisha Ile Sendeka.

..pia nashauri suala la UZALENDO lisitumike ktk kupima hoja za wahusika ktk mgogoro huu. Kuna hatari ya kuharibu mjadala, au hata kuanza kuumizana kama ilivyotokea ktk awamu ya 5.
 
Alipewa muda wa kutosha na hata angepewa saa nzima bado asingeweza kujieleza vyema kwani vifungu vya sheria havikuwemo kati ya makaratasi yake.

Naibu waziri alijibu kwa hasira kwani alichukulia kama vile serikali inataka kuwaonea wamasai wakati eneo la hifadhi halina watu.

Kuna suala la kizalendo linafanywa na serikali tatizo la watanzania siku zote ni tafsiri potofu kuenezwa kwa haraka kuliko zile sahihi.
Hilo suala kizalendo linalofanywa na serikali lifafanue hapa. Tunayosikia ni kwamba:
1. Kuna mwekezaji wa kiarabu anatafutiwa nafasi ya KUJINAFASI yaani apewe kitalu kikubwa cha kuwinda!
2. Kuna suala la kuruhusu wanyama kusafirishwa wazima kwa meli maalumu.
Fafanua hayo mawili yanaingiaje kwenye uzalendo.

Lakini pia kuna hili suala linalozungumzwa la kuwabania wakenya, je wakenya wakilisha na waarabu wakichukua wanyama kuna unafuu wapi?

Ninachokiona hapa ni kwamba hata serikali haijawa wazi sana katika suala hili. Watufafanulie na kutupa mchanganuo unaoonesha Tanzania tutaingiza sh ngapi kwa mwaka kwa hatua hii tunayoifanya ili tuone kama usumbufu huu wa wananchi unastahili kukubalika!
 
Mwalimu Tulia anajua baadhi ya sheria hufutwa kwa sheria mpya siyo vifungu

Ndio sababu alimuwahi Ole sendeka kabla hajamwaga mboga!

Angekuwa Zitto Kabwe angekomaa naye hadi mwisho kama Buzwagi
Ardhi ipo Handeni na ni yenye rutuba na fidia wanalipwa na wanakutana na nyumba zilizojengwa tayari.

Wenye akili wameona kubishana na serikali hakuna maana yoyote.
 
Ardhi ipo Handeni na ni yenye rutuba na fidia wanalipwa na wanakutana na nyumba zilizojengwa tayari.

Wenye akili wameona kubishana na serikali hakuna maana yoyote.
Usichanganye madesa
Wanaokwenda Handeni ni Wamasai wa Ngorongoro
 
Back
Top Bottom