Oliver N’goma: Mmoja kati ya wanamuziki bora zaidi wa kiume wa miondoko ya Zuku

Oliver N’goma: Mmoja kati ya wanamuziki bora zaidi wa kiume wa miondoko ya Zuku

“Nge’” maana yake You (wewe) kwenye hii nyimbo Inamhusu binti aliyechoshwa na hali ya kuwa mpango kando “side chick” anatamani naye kuwa na mpenzi wake mwenyewe hivyo anaomba Mungu amuonyeshe huyo mtu maana kachoshwa na aina ya mahusiano yake ya sasa. Oliver anamtia moyo kwa kumwambia yeye ni mzuri hivyo aombe na kusubiri.
RIP “NOLI” son from Mayumba
safi sana kaka kwa ufafanuzi ..hii nyimbo itaishi sana ..bnafsi naipenda mno ...."MOBI MOBI USANGULA MUMU"
 
Nilichompenda sio mziki Bali maisha yanahitaji ubunifu, jamaa kamaliza degree ya engineering kafa mwanamziki
 
hapana alisomea utangazaji kitu kama hicho na aliwahi kuwa mtangazaji na camera Man
Oliver hakutarajia Kama kuna siku atafanya muziki kama kazi yake kuu, aliwahi kusema mke wake ndo mtu aliyemsukuma aingie rasmi na kumtia moyo kuwa muziki anauweza. Aliamini kuwa mwanaume anahitaji support ya mwanamke ili afanikiwe na kufika mbali. Anaheshimu sana mwanamke alimuimba na kumsifia mwanamke ndo maana hata nyimbo zake za mapezi zina title ya majina ya kike. Ntakuja kukupa maana ya wimbo “Muetsi” ambao ni maarufu sana maharusini.
 
Hebu nipe hiyo title bwana masoud masoud
 
Hebu nipe hiyo title bwana masoud masoud

“Muetsi” maana yake ni Moonlight (mwangaza wa mwenzi). Oliver anamwelezea mwanamke ambaye ameangaza (kuimarisha) maisha ya mwenza wake kama mwezi unavotupa nuru wakati wa usiku. Hivyo kama wanaume ni Vizuri kufanya chaguo jema la wenza wetu ( wake) kwani ni muhimu kwa maendeleo yetu na familia kwa ujumla.
Ndo maana nyimbo hii hupigwa sana kwenye harusi hata hapa kwetu Tanzania [emoji1241].
Inapatikana katika album ya “Adia”

Kwako Masoud Masoud [emoji23][emoji23]
 
Wakuu mimi ni moja kati ya mashabiki zake kindaki ndaki Uzima ukiwepo ipo siku nitaenda kuhiji huko Mayumba na Lebreville Gabon japo nione hata kaburi lake huyu mfalme wa Zouk aisee
Oliver N'goma alikua na miondoko na vionjo adimu sana sana sijawahi experience mziki mtamu wenye mixing na beat amazing Kama za Huyu mwamba aisee vibao kama
Bane
Adia
Icole
Betty
Lusa
Alphonsine
Saga
Noli
Betty
Mayumba
Mukuili
Ngebe
Julie
Lili
Melia
Seva
Nge
Lina
Noli
Mayumba
Na nyingine nyiiingi hakika ni moja ya vibao bora sana ambavyo sijapata kuona toka nianze kuujua mziki
Niseme tu hongera mtoa mada kwa kutambua mchango wa burudani wa huyu nguli
Mimi now nipo around miaka kama 23 tu hivi ila najua mziki mzuri hua napenda sana kufuatilia old music yaani kuhusu vijana wenzangu hawa wakina nani hua siwaelewi kabisaaaaaa
Anyway R.I.P oliver N'goma a.k.a Noli
King of Zouk!😢😢
Hongera Sana Mkuu, Kwa Umri Wako na Kupenda Haya Madini, Itoshe Kusema Ukom Njema Hasa
 
Huyu ni mmoja ya kati ya wanamuziki bora zaidi wa kiume wa miondoko ya Zuku kuwahi kutokea katika hii dunia.
Embu tujikumbushe kidogo na hii ngoma yake Inaitwa Ng’e. Btw wale watoto wa bongo flavor sikilizeni hii ngoma alafu mlinganishe na muziki wa sasa wa wavaa suruali chini ya makalio.

Back
Top Bottom