TANZIA Olivia Hussey, Aliyewahi kuigiza kama Bikira Maria (Mama wa Yesu) afariki dunia

Ila RC kuna mambo mnazingua, huku sio kuabudu masanamu kweli,?
Inaonekana hujui maandiko kiundani sana,ulitakiwa upate ufafanuzi kutoka kwà watu walioisoma na wakaielewa.Hii itakuondolea misconception.
 
Mwigizaji Olivia Hussey maarufu kama Juliet , aliyepata umaarufu kupitia filamu ya Romeo and Juliet ya mwaka 1968, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73.

Mwigizaji huyo ambaye amewahi kuuvaa uhusika kama mama wa Yesu katika filamu ya 'Jesus Nazareth' ya mwaka 1977, amefariki siku ya Ijumaa akiwa amezungukwa na wapendwa wake.
Huyu ndiye wakatoliki wanamuabudu kama bikra Maria? Hizi imani hizi zinatupotosha sana aisee!
 
Mbona Biblia imekataza kabisa matumizi ya sanamu Kanisani ? Kumb 4:16, 1 wakorintho 6:9 Mungu hakuna kama kuna uelewa hafifu ?
Hekalu tu lilikuwa na sanamu pamoja na michoro kibao hapo utasemaje ?
 
Huyu ndiye wakatoliki wanamuabudu kama bikra Maria? Hizi imani hizi zinatupotosha sana aisee!
Wewe nadhani ndio unapotosha, kwanza Bikira Maria haabudiwi, pili wewe umeona kanisa gani wamemuweka huyo ?
 
Umenikumbusha hii novena wakati nipo seminari, Tulikuwa tuna isali sana.

Tukiamini kwamba mtakatifu Rita ni mtakatifu wa mambo yaliyo shindikana.

Basi baada ya kufunga na kusali kwelikweli kwa kutia nia kabisa, unabaki kusubiri miujiza itendeke, Lakini Holaaaa!! 😂

Unahamia tena kwenye novena nyingine ya mtakatifu Filomena, ikibuma unapiga novena ya mtakatifu Theresia, ikibuma unapiga novena ya Bikira Maria wa mlima wa Karmeli, ikibuma unapiga sala kwa Padri pio, ikibuma unapiga novena kwa watakatifu wote wa mbinguni, malaika, maserafi mpaka kwa makerubii....🤣🤣
Kumbe ulikuwa mseminari sasa imekuwaje umekuwa atheist
 
Wewe nadhani ndio unapotosha, kwanza Bikira Maria haabudiwi, pili wewe umeona kanisa gani wamemuweka huyo ?
Kila kanisa la katoliki lina picha ya huyo mama wamempamba na kumuita kuwa yeye ndiye bikra Maria.
 
Lucia Franciska na Yasinta walitokewa na Bikira Maria, namna walivyomuelezea na kumtambua sura yake ndivyo inavyotumika kuelezea na kutengeneza sanamu ya Bikira Maria, Pia amewahi kutokea mara nyingi kwa nyakati tofauti.
 
Kumbe ulikuwa mseminari sasa imekuwaje umekuwa atheist
Mkuu, kila mtu ni Atheist in nature mpaka pale unapokuwa indoctrinated and brainwashed with religious beliefs.

Baada ya kusoma Philosophy kwa kina ndipo niligundua dhana nzima ya "Mungu" ilitungwa na watu tu.

Hata mapadri husoma Philosophy, Lakini wao huendelea na Theology na huko hawaruhusiwi kuhoji chochote kama ilivyo kwenye philosophy.

Huambiwa waamini mafundisho hayo kwa imani tu. Theology sana sana ni Dogmatic teachings.

Yani unalazimishwa kuamini kitu, pasipo kuhoji chochote wala kuuliza maswali.

Hapo ndipo niligundua kwamba Religion requires you to have "faith" because it lacks evidences, logic, proofs, facts, critical thinking and reasoning.
 
Lucia Franciska na Yasinta walitokewa na Bikira Maria, namna walivyomuelezea na kumtambua sura yake ndivyo inavyotumika kuelezea na kutengeneza sanamu ya Bikira Maria, Pia amewahi kutokea mara nyingi kwa nyakati tofauti.
Walitokewa mwaka gani? Tarehe ngapi? Mwezi upi? Siku ipi? Na muda gani exactly wa tukio?

Leta uthibitisho hapa.
 
Kati ya Mei 13 na Oktoba 13, 1917, watoto watatu Lucia, Fransisco na Yasinta wachungaji wa Kireno kutoka Alhindrel, walitokewa na Bikira Maria huko Cova da Iria, karibu na Fátima, mji umbali wa maili 110 kaskazini mwa Lisbon. Wakati huo, Ulaya ilihusika katika vita ya umwagaji damu sana. Ureno yenyewe ilikuwa katika machafuko ya kisiasa, baada ya kupindua mfalme wake mnamo 1910.
 
Mkuu, kila mtu ni Atheist in nature mpaka pale unapokuwa indoctrinated and brainwashed with religious beliefs.

Baada ya kusoma Philosophy kwa kina ndipo niligundua dhana nzima ya "Mungu" ilitungwa na watu tu.

Hata mapadri husoma Philosophy, Lakini wao huendelea na Theology na huko hawaruhusiwi kuhoji chochote kama ilivyo kwenye philosophy.

Huambiwa waamini mafundisho hayo kwa imani tu. Theology sana sana ni Dogmatic teachings.

Yani unalazimishwa kuamini kitu, pasipo kuhoji chochote wala kuuliza maswali.

Hapo ndipo niligundua kwamba Religion requires you to have "faith" because it lacks evidences, logic, proofs, facts, critical thinking and reasoning.
Sawa Mkuu
 
Lucia Franciska na Yasinta walitokewa na Bikira Maria, namna walivyomuelezea na kumtambua sura yake ndivyo inavyotumika kuelezea na kutengeneza sanamu ya Bikira Maria, Pia amewahi kutokea mara nyingi kwa nyakati tofauti.
Bado anawatokea watu au ndio kamaliza ?
 
Back
Top Bottom