Binadamu Mtakatifu
JF-Expert Member
- Oct 12, 2018
- 4,423
- 9,296
Habari wana-tech,
Leo nataka kuwashirikisha mradi wangu mmoja wa open-source unaitwa OllaBridge. Huu mchongo utawasaidia sana ma-developer wenzangu wanaotumia shared hosting (kama Hostinger, cPanel, n.k.) kutumia nguvu ya AI kwenye websites zao bila kulipia madola ya ChatGPT API wala kuhitaji VPS za gharama.
Ile kero tuliyokuwa nayo: Shared hosting nyingi hazikubali ku-install Python au kuendesha "heavy AI models." Na changamoto nyingine ni kwamba huku kwetu kupata Static IP kwenye local server au Pc ya nyumbani ni ishu, hivyo huwezi kuunganisha website yako na AI iliyo kwenye mashine yako moja kwa moja.
Suluhisho (OllaBridge): Hapa ndipo OllaBridge inapoingia kati. Hii ni programu ndogo (Worker) inayokaa kwenye Pcyako. Badala ya website yako kuitafuta Pc yako (kitu ambacho kingehitaji static IP), Pc yako ndiyo inayoiuliza website: "Oya, kuna mzigo wowote wa AI unatakiwa kuchakatwa?"
Website ikipata swali kutoka kwa user, Pc yako inaubeba, inauchakata kupitia Ollama, kisha inarudisha jibu kule kule kwenye website. Ni simple na haina complications za ma-firewall.
Maujanja yake:
Maoni yenu ni muhimu: Kama una project yoyote ya PHP au website unayotaka kuweka mambo ya AI (kama Llama 3, Qwen, n.k.) kishikaji na bure, jaribu hii OllaBridge. Kama kuna mahali utakwama au una wazo la kuiboresha, nistue hapa hapa chini kwenye comment.
Tupige kazi! 🚀

- Setup ni fasta: Ina wizard (ollabridge setup) inayokuongoza mwanzo mwisho.
- Hauzimiki: Inaji-install kama systemd service, yaani hata ukizima na kuwasha Pc, mchongo unajiwasha wenyewe fasta.
- Usalama: Kuna "Secret Key" ambayo unaitumia ili kuhakikisha ni website yako tu ndiyo inayoweza kuipa kazi local server yako.
- Standalone Binary: Kama hutaki mambo ya Python, nimeandaa file moja tu (binary) — unadownload na kuanza kazi.