Oman: Rais Samia ataka kuwepo Maritime transport ya kusafirishia Wanyama wakiwa hai kutoka Tanzania kwenda Oman

Oman ni ndugu zetu, wao kufaidi mbuzi,kondoo na ng'ombe wa Tanzania na hapo hapo mfugaji amepata soko la uhakika shida ipo wapi?
Mama kweli godsent for Tanzanians, mindset/rigidity ya jiwe tupilia mbali. Kazi iendelee
 
Ni lini mtauza finished products? Wakiuzwa ng'ombe walio hai viwanda vya nyama vitawauzia nani?

Msemo wa 'Customer is always the King' , hatuwezi kuwalazimisha wateja bali tunafuata vile wateja wanavyopenda. Yaani nyama za makopo zilizosindikwa hazina biashara kubwa zaidi ya nyama za buchani zilizotoka ktk machinjio ya jirani na kwao.

Tamaduni za wateja ziheshimiwe na biashara ilenge vile mteja anataka na tuifanye vizuri ndivyo tutakavyowashinda washindani wetu wa soko la wanyama hai .
 
Anachofanya "Mama" ni sawa tu na alichofanya JPM kuanzisha hifadhi ya Burigi-Chato na kupeleka wanyama kule.

Kwa wanzanzibar,Oman ni home away from home.

Kwahiyo na yeye anapeleka wanyama nyumbani kwao pia!

Pinda Chana hatastopisha hili.
Hata alipokua Marekani kwenye royal tour aliwaambia atawapa wanyama Kama Simba, twiga, faru n.k
Vipi Marekani napo nyumbani kwetu?
 
Hakuna dili lolote hapo. Wao wanapaswa kuuziwa finished products Kama nyama. Viwanda hapa vipo Kama havipo serikali iweke mazingira viongezwe au hao waoman waje kujenga viwanda huku wasafirishe hizo nyama
 
Watu wanatakiwa kuchangamkia fursa na siyo kulialia tu.
Fursa ni wa oman wangetoa order ya nyama kiasi gani wanahitaji kwa mwaka. Watu waingie chimbo wazalishe huku viwandani.
Ni lini tutauza finished products? Bila kuwa na viwanda vya kutosha hapa na kuzalisha finished products hakutakua na fursa Bali tutakua Kama Somalia tu
 
Ok sawa ila Bwana yupo kazin ,tunashukuru Sana mh rais
 
Shida ni kuwa mama inaonekana anapokea ushauri kirahisi na kutekeleza na pia sioni kama yupo serious kwenye usimamizi wa rasilimali. Mfano hii mikopo inayokopwa kila kukicha kama hamna mipango madhubuti na usimamizi itakuja kwisha bila msaada wowote kwa nchi kuendelea
 
Changamkia fursa achana na kulialia
Hakuna fursa hapo bali ni majanga.
Ilipaswa tuwauzie nyama na sio ng'ombe .
Kama tunavyouza nje maparachichi ya mbeya na Njombe tuamue Sasa tuwauzie miti ya miparachichi.
Hakuna nchi inendelea na watu wake kuendelea bila kuzaisha finished products na kuuza nje.
 
Kuna wajinga humu wanaona mbuzi na twiga ni sawa, hawaoni kama hao waarabu watachangamkia kile ambacho hawakipati toka mataifa mengine.

Hao mbuzi na kondoo watawahitaji kwa kiasi kidogo kwasababu wanawapata toka nchi nyingine, lakini kwa twiga wetu, na wanyama wengine wa mwituni ndio watamalizwa, na utalii utahamia huko Arabuni.

Hizi fursa zinazofunguliwa na huyu mama ni janga kwa taifa letu na kwa vizazi vijavyo, madini wameyatoa sasa wanatoa na wanyama wetu. Oman wakianza kutangaza vivutio vyao vya utalii na Twiga wetu watakuwepo, sasa hao watalii watatoka wapi kuja kwetu?
 
Hata alipokua Marekani kwenye royal tour aliwaambia atawapa wanyama Kama Simba, twiga, faru n.k
Vipi Marekani napo nyumbani kwetu?
Huioni tofauti hapo wewe?

Oman inaenda kuwa serious business ya kusafirisha wanyama hai toka Tz siyo kuwapa wanyama watatu au kumi.
 
sasahv twiga wanapanda ndege bila hata ya passport.
 
Kuuza nyama na kuuza ng'ombe ipi ni fixed mentality?
Anayeuza nyama ndio amechangamkia fursa kwa kuwa anauza finished product. Na ataongeza thamani ya bidhaa yake kuliko kuuza ng'ombe
Matatizo unayoyaona Leo kwenye nchi zote za Africa ni sababu ya huo ujinga wa kuuza malighafi na sio finished products.
 
Hakuna dili lolote hapo. Wao wanapaswa kuuziwa finished products Kama nyama. Viwanda hapa vipo Kama havipo serikali iweke mazingira viongezwe au hao waoman waje kujenga viwanda huku wasafirishe hizo nyama

Mkuu Australians waliwapelekea wa Saudi na Kuwait nyama ya farasi na [emoji3075] kangaroos hata mimi nimekula sana kangaroo [emoji23][emoji23]huko
Ila walipogundua wakasema tunataka livestock tu
 
JPM Baba tunakulilia huku rudiii
Badala ushukuru Mungu kwa kutondolea ile kadhia wewe unatamani yule muuaji arudi tena. Kuwa siku watumwa walipewa uhuru wao lakini wengine wakakataa kuondoka na kuomba kubaki utumwani. Nadhani hata wewe ni aina ya watu wale.
 
Bora mama kuliko Jiwe. Na kila mwenye akili timamu aombe na kusali tusije pata tena Rais dizaini yake
 
Mkuu Australians waliwapelekea wa Saudi na Kuwait nyama ya farasi na [emoji3075] kangaroos hata mimi nimekula sana kangaroo [emoji23][emoji23]huko
Ila walipogundua wakasema tunataka livestock tu
Acha utani
 
Mkuu Australians waliwapelekea wa Saudi na Kuwait nyama ya farasi na [emoji3075] kangaroos hata mimi nimekula sana kangaroo [emoji23][emoji23]huko
Ila walipogundua wakasema tunataka livestock tu

Ni kweli ndiyo maana Australia wanasafirisha wanyama hai baada ya Kulifahamu soko vizuri, na hii husaidia kuikamata fursa vizuri zaidi. Tunaweza kukazia mjadala huu kwa maneno matatu : Mteja Ni Mfalme.
 
Huioni tofauti hapo wewe?

Oman inaenda kuwa serious business ya kusafirisha wanyama hai toka Tz siyo kuwapa wanyama watatu au kumi.
Hoja yako ilikua ni kuhamisha wanyama na ukasema oman ni ndugu zetu, ndio nikakuuliza Marekani alisema pia atawapa nao ni ndugu zetu?
Serious business ya kuuza wanyama hai?
Nchi zote duniani zimeendelea kwa kuwa na viwanda vya kuzalisha finished products na kuuza nje. Kwa nn hao wa oman wasije kuwekeza viwanda vya nyama hapa?
 
Huyu Mama Si kitu kizito tu bali Cheney ncha kali. Watu wanapambana ku add value yeye Yuko busy na barter trade ya wanyama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…