Oman: Rais Samia ataka kuwepo Maritime transport ya kusafirishia Wanyama wakiwa hai kutoka Tanzania kwenda Oman

Oman: Rais Samia ataka kuwepo Maritime transport ya kusafirishia Wanyama wakiwa hai kutoka Tanzania kwenda Oman

Oman ni ndugu zetu, wao kufaidi mbuzi,kondoo na ng'ombe wa Tanzania na hapo hapo mfugaji amepata soko la uhakika shida ipo wapi?
Mama kweli godsent for Tanzanians, mindset/rigidity ya jiwe tupilia mbali. Kazi iendelee
 
Ni lini mtauza finished products? Wakiuzwa ng'ombe walio hai viwanda vya nyama vitawauzia nani?

Msemo wa 'Customer is always the King' , hatuwezi kuwalazimisha wateja bali tunafuata vile wateja wanavyopenda. Yaani nyama za makopo zilizosindikwa hazina biashara kubwa zaidi ya nyama za buchani zilizotoka ktk machinjio ya jirani na kwao.

Tamaduni za wateja ziheshimiwe na biashara ilenge vile mteja anataka na tuifanye vizuri ndivyo tutakavyowashinda washindani wetu wa soko la wanyama hai .
 
Anachofanya "Mama" ni sawa tu na alichofanya JPM kuanzisha hifadhi ya Burigi-Chato na kupeleka wanyama kule.

Kwa wanzanzibar,Oman ni home away from home.

Kwahiyo na yeye anapeleka wanyama nyumbani kwao pia!

Pinda Chana hatastopisha hili.
Hata alipokua Marekani kwenye royal tour aliwaambia atawapa wanyama Kama Simba, twiga, faru n.k
Vipi Marekani napo nyumbani kwetu?
 
Wabongo tatizo letu wengi ni ushamba umetujaa sana hata hatuelewi kipi kina faida kwetu au hakina
Ni kubisha kila kitu na huo sio akili bali ni kujiweka nyuma kwa kila kitu

Hata hii biashara ya mifugo Somalia wanafanya miaka kibao kupeleka saudia , Emirates na hata Oman
Ila wanajua biashara na hawana ujanja ujanja

Sisi kweli tunaweza kupewa fursa ya kupeleka wanyama au matunda lakini je hivyo viwango nani atakagua?

Nasema hivyo kwa sababu huko nyuma tumepeleka Tumbaku Zimbabwe na matokeo yake hawataki hata kutusikia na waliandika kwenye blogs nyingi duniani
Kweli mnaweka Mapembe ya Ng’ombe na battery zilizokufa na matofali ili kuongeza mzigo uwe mzito

Na hao wakaguzi ndio wanapewa rushwa wavushe mzigo

Tatizo letu kila mahali wizi

Huu uzi muufukue siku zijazo kuhusu hawa domestic animals watapigwa marufuku kwa sababu mtapeleka mpaka wagonjwa na ndio mwisho wa dili la mama
Hakuna dili lolote hapo. Wao wanapaswa kuuziwa finished products Kama nyama. Viwanda hapa vipo Kama havipo serikali iweke mazingira viongezwe au hao waoman waje kujenga viwanda huku wasafirishe hizo nyama
 
Watu wanatakiwa kuchangamkia fursa na siyo kulialia tu.
Fursa ni wa oman wangetoa order ya nyama kiasi gani wanahitaji kwa mwaka. Watu waingie chimbo wazalishe huku viwandani.
Ni lini tutauza finished products? Bila kuwa na viwanda vya kutosha hapa na kuzalisha finished products hakutakua na fursa Bali tutakua Kama Somalia tu
 
View attachment 2259291
Salaam Wakuu,

Rais Samia katika Kongamano la Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania, amesema kuna umuhimu Mkubwa wa kuangalia Usafiri wa Majini akimanisha Meli yenye Uwezo wa kusafirisha Wanyama wakiwa hai kutoka Tanzania kwenda Oman.

Watu hapa wasifikilie Wanyama Pori tu, Bali ni Habari njema kwa Wafugaji wa Tanzania kwani sasa Wataanza Kusafirisha Ng'ombe, Sungura, Kitimoto, Mbuzi, Swala, Twiga nk hasa kwa wawindaji wenye Vitaru.

Pia kazungumzia kuhusu meli za Kuvua samaki Bahari Kuu.

Amewataka Oman waje kuwekeza Tanzania ardhi ipo ya kutosha.

Watanzania Kaeni Mkao wa kula.

............................................................................

Rais Samia akiwa kwenye kongamano Kiuchumi nchini Oman, amesema kuwepo kwa vyombo vya usafirishaji vya majini kusafirisha wanyama walio hai na bidhaa mbalimbali kwenda Oman kutaboresha biashara kati ya pande hizo mbili

Pia amegusia japokuwa tuna makubwa ya kuvua, kwa sasa hamna uvuvi wenye tija kwa taifa, amesema “kuna nchi zinakuja Tanzania kuvua na hatuwezi kuwafukuza kwa sababu hatuna vifaa, hivyo wanavua na kuondoka, hili ni eneo lingine ambalo tunaweza kushirikiana kwa pamoja”

Amesema kuwa kongamano la mwaka huu limekusudia kuangazia namna Tanzania itashirikiana na Oman katika sekta za utalii, kilimo, Uzalishaji (viwanda) mifugo na uvuvi na usafirishaji wa majini
Ok sawa ila Bwana yupo kazin ,tunashukuru Sana mh rais
 
Shida ni kuwa mama inaonekana anapokea ushauri kirahisi na kutekeleza na pia sioni kama yupo serious kwenye usimamizi wa rasilimali. Mfano hii mikopo inayokopwa kila kukicha kama hamna mipango madhubuti na usimamizi itakuja kwisha bila msaada wowote kwa nchi kuendelea
 
Changamkia fursa achana na kulialia
Hakuna fursa hapo bali ni majanga.
Ilipaswa tuwauzie nyama na sio ng'ombe .
Kama tunavyouza nje maparachichi ya mbeya na Njombe tuamue Sasa tuwauzie miti ya miparachichi.
Hakuna nchi inendelea na watu wake kuendelea bila kuzaisha finished products na kuuza nje.
 
Kuna wajinga humu wanaona mbuzi na twiga ni sawa, hawaoni kama hao waarabu watachangamkia kile ambacho hawakipati toka mataifa mengine.

Hao mbuzi na kondoo watawahitaji kwa kiasi kidogo kwasababu wanawapata toka nchi nyingine, lakini kwa twiga wetu, na wanyama wengine wa mwituni ndio watamalizwa, na utalii utahamia huko Arabuni.

Hizi fursa zinazofunguliwa na huyu mama ni janga kwa taifa letu na kwa vizazi vijavyo, madini wameyatoa sasa wanatoa na wanyama wetu. Oman wakianza kutangaza vivutio vyao vya utalii na Twiga wetu watakuwepo, sasa hao watalii watatoka wapi kuja kwetu?
 
Hata alipokua Marekani kwenye royal tour aliwaambia atawapa wanyama Kama Simba, twiga, faru n.k
Vipi Marekani napo nyumbani kwetu?
Huioni tofauti hapo wewe?

Oman inaenda kuwa serious business ya kusafirisha wanyama hai toka Tz siyo kuwapa wanyama watatu au kumi.
 
sasahv twiga wanapanda ndege bila hata ya passport.
 
Nchi kama Somali wanasafirisha Mbuzi na Kondoo huko Oman,Australia wanasafirisha Kondoo huko Oman,

Naona badala ya kuchangamkia fursa mmekimbili sijui Twiga mara Tembo!

Bila kubadili hizi fixed mind mentality mtu atajikuta yupo pale pale tu miaka na miaka.
Kuuza nyama na kuuza ng'ombe ipi ni fixed mentality?
Anayeuza nyama ndio amechangamkia fursa kwa kuwa anauza finished product. Na ataongeza thamani ya bidhaa yake kuliko kuuza ng'ombe
Matatizo unayoyaona Leo kwenye nchi zote za Africa ni sababu ya huo ujinga wa kuuza malighafi na sio finished products.
 
Hakuna dili lolote hapo. Wao wanapaswa kuuziwa finished products Kama nyama. Viwanda hapa vipo Kama havipo serikali iweke mazingira viongezwe au hao waoman waje kujenga viwanda huku wasafirishe hizo nyama

Mkuu Australians waliwapelekea wa Saudi na Kuwait nyama ya farasi na [emoji3075] kangaroos hata mimi nimekula sana kangaroo [emoji23][emoji23]huko
Ila walipogundua wakasema tunataka livestock tu
 
JPM Baba tunakulilia huku rudiii
Badala ushukuru Mungu kwa kutondolea ile kadhia wewe unatamani yule muuaji arudi tena. Kuwa siku watumwa walipewa uhuru wao lakini wengine wakakataa kuondoka na kuomba kubaki utumwani. Nadhani hata wewe ni aina ya watu wale.
 
Hawezi kuamka huyo, kwanza macho yake yamelegea utadhani amekula kungu! Anazidi kupotelea kwenye usingizi wa pono!
Wakiisha wanyama itabidi irudishwe biashara ya watumwa!
Seriously, badala ya kuanzisha viwanda ili tuuze processed animal products unawaza upuuzi wa kusafirisha wanyama ghafi astaghafurrulahi[emoji134]!
Mungu kwa nini ulimchukua Magu mapema?
Kweli JPM hatunae Tena! RIP JPM, our beloved president of the united Republic of Tanzania!
Bora mama kuliko Jiwe. Na kila mwenye akili timamu aombe na kusali tusije pata tena Rais dizaini yake
 
Mkuu Australians waliwapelekea wa Saudi na Kuwait nyama ya farasi na [emoji3075] kangaroos hata mimi nimekula sana kangaroo [emoji23][emoji23]huko
Ila walipogundua wakasema tunataka livestock tu
Acha utani
 
Mkuu Australians waliwapelekea wa Saudi na Kuwait nyama ya farasi na [emoji3075] kangaroos hata mimi nimekula sana kangaroo [emoji23][emoji23]huko
Ila walipogundua wakasema tunataka livestock tu

Ni kweli ndiyo maana Australia wanasafirisha wanyama hai baada ya Kulifahamu soko vizuri, na hii husaidia kuikamata fursa vizuri zaidi. Tunaweza kukazia mjadala huu kwa maneno matatu : Mteja Ni Mfalme.
 
Huioni tofauti hapo wewe?

Oman inaenda kuwa serious business ya kusafirisha wanyama hai toka Tz siyo kuwapa wanyama watatu au kumi.
Hoja yako ilikua ni kuhamisha wanyama na ukasema oman ni ndugu zetu, ndio nikakuuliza Marekani alisema pia atawapa nao ni ndugu zetu?
Serious business ya kuuza wanyama hai?
Nchi zote duniani zimeendelea kwa kuwa na viwanda vya kuzalisha finished products na kuuza nje. Kwa nn hao wa oman wasije kuwekeza viwanda vya nyama hapa?
 
Huyu Mama Si kitu kizito tu bali Cheney ncha kali. Watu wanapambana ku add value yeye Yuko busy na barter trade ya wanyama
 
Back
Top Bottom