Somalia ni failed state, kule hata watu wanauzwa. Somalia unafanya chochote unachojisikia, Hakuna serikali
Mkuu Somaliland wako vizuri sana na amani tele wanasafirisha kutoka Port ya Bossaso na Port ya Berbera na wanafanya biashara kuliko unavyofikiria
Kuna fursa nyingi sana huko
Kwa mtu ambae hajatembea na kuona vita ni ngumu sana kuelewa hili
Kuna fursa nyingi sana sehemu vita inapotokea
Mimi hapa nilikuwa na Lorry huko uarabuni miaka ya 80 baada ya vita kuanza baina ya Iraq na Iran ikabidi chakula kiwe kinashushwa kwenye Port za jirani kama Kuwait
Na hapo ndio nilipiga hela kubeba ngano kupeleka Iraq
Ila kama una roho ya uoga huwezi fanya hiyo biashara katikati ya vita
Angalia Congo kuna wanaume wanapeleka chakula huko na misaada ya UN
Kwa hiyo Hakuna cha failed state
Sisi miaka 60 ya Uhuru bado tunaringia Amani zaidi ya hapo ni zero state
Acha tupingane kwa hoja mimi nimefanya kazi kwenye nchi zenye vita na huwa nachekelea haswa kama aliesema waache wagombane Sisi tutawauzia chakula
Turudi kwenye hadithi yetu ya usafirishaji wa nyama sasa