Uchaguzi 2020 Omary Kumbilamoto atoboa siri za CHADEMA kuhujumu Miradi ya Awamu ya Tano

Uchaguzi 2020 Omary Kumbilamoto atoboa siri za CHADEMA kuhujumu Miradi ya Awamu ya Tano

Zamani nilikuwa nikisikia wazungu wanatuita manyani nilikuwa napata hasira sana, lakini baada ya kufuatilia vizuri nimegundua wako sahihi. Kila siku rais anasema anataka kuona siasa za kistaarabu za kuhubiri sera, kisha anatokea mtu anafanya igizo la kitoto la kusema alihujumu miradi, kwa akili hizo hizo za kinyani anasemehewa na nyani mwenzake badala ya kushitakiwa! Ajabu watu wanashangilia huo utoto!
Kauli ya mnafiki anayejifanya mfia Chadema.
 
Kumbilamoto anajipendekeza ili akishinda udiwani ccm wampitishe kuwa meya. Nilikuwa namkubali huyu jamaa kwasababu wakati cuf ina mgogoro, yeye alikuwa upande wa Maalim. Hivi Charles Kuyeko ambaye alikuwa ndio meya kabla yake yuko wapi hivi sasa? Sababu aliunga mkono juhudi kabla ya Kumbilamoto.
Kama ni kweli walihujumu miradi ya maendeleo kwanini TAKUKURU wasimkamate uhujumu uchumi na amekiri?
 
Mwendelezo wa siasa za ghiliba, uzushi na uzandiki ili kumfurahisha bwana yule mpenda sifa
 
Tundu anaenda kupata aibu ya dunia awamu hii.
 
Duh CCM imechokwa kweli kweli yaani wamefikia hatua ya kutumia siasa nyepesi kiasi hiki.
Nikikumbuka CCM ya Kinana,Gama,Kolimba na kuilinganisha na ya Bashiru,kuna tofauti kubwa sana kiuongozi na kipropaganda.
 
Leo eneo la Kinyerezi kwenye kampeni za Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi ambaye ndie Rais Mtarajiwa hilo halina ubishi, Kumbilamoto amemuomba msamaha Dkt. Magufuli kuwa walifanya makosa makubwa sana akiwa Meya wa Ilala kupitia CHADEMA kuhujumu miradi ya Serikali ili kuonesha Rais Magufuli hawezi kutatua matatizo ya wananchi, hivyo amesema CHADEMA ni Chama kinachozungukwa na watu wasiolitakia Taifa letu mema hasa sisi wanyonge.

===


Aliyekuwa Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala, ambaye pia alikuwa ni Diwani wa Vingunguti, Omar S. Kumbilamoto amumomba radhi Dkt. Magufuli leo katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kinyerezi

Kumbilamoto ameomba radhi kwa kuwa alikuwa Upinzani katika Umoja uliojulikana kama UKAWA katika Uchaguzi Mkuu wa 2015

Kwasababu hiyo ameomba radhi kwa Rais, CCM, wananchi na viongozi wa Ilala kwa mabaya waliowafanyia kipindi yuko upinzani

Ameyasema hayo alipopewa muda wa kuzungumza kwenye mkutano wa kampeni

Nukuu:
Kabla sijaongea, nichukue fursa hii kwanza kukuomba msamaha wewe binafsi, Chama cha Mapinduzi na wananchi kwa ujumla kwa mabaya tuliyowafanyia wakati tupo upinzani. Naomba sana unisamehe Mheshimiwa Mwenyekiti.

Mheshimiwa Rais, katika manispaa yetu uliingiza miradi ya Soko la Kisutu, Machinjio ya Vinginguti na Hospitali ya Kivule.

Ukaingiza bilioni 17.6 ujenzi wa daraja la Ulongoni, bilioni 4.3 ujenzi wa Daraja la Zimbili na uliingiza takribani bilioni 115 ya barabara za BMDP.

Nisikufiche Mheshimiwa Rais, miradi hii ilikwama kwa maelekezo kwamba tukifanya sisi kama ukawa tutakupa kiki wewe Rais Magufuli. Ilibidi na sisi tutii, tukakuhujumu. Kwahiyo naomba unisamehe sana.

Baada ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala sisi kurudi, miradi hii yote tukaikwamua na hivi sasa ipo kwenye maendelezo na mingine imeshakamilika.

Lakini kubwa zaidi Rais kilichotuuma sisi tukawa upinzani kulikuwa na mikopo ya Asilimia 10 ambapo mikopo hii ilikuwa haitoki na wala wananchi hawaijui – 2010 hadi 2015. Ulipoingia ukaagiza itoke hii mikopo takribani bilioni 10 na hapa nimpongeze Mkurugenzi , pesa hizi zimewafikia wananchi wa kawaida – mama lishe na bodaboda.
Ningependa afafanue yeye na wenzake walihujumu namna gani

ili akileta ushahidi kwa namna walivyofanya wachukuliwe hatua iwe fundisho kwa jamii
 
Hawa wachumia tumbo wenu mliowanunua kwenye hii awamu yenu ya tano waambieni hawatawasaidia chochote.
 
Thread yako haina mashiko ni takataka tu kwa sababu Kumbilamoto hajawahi kuwanChadema hata siku moja.

Umekurupuka.
 
Lissu jibu hoja hizo za chadema kuhujumu maendeleo. Nimesikia nikashangaa na zisipojibiwa zitakuwa ni kweli
Magufuli kadanganywa huyu mpuuzi alikuwa CUF kabla ya kununuliwa na Jiwe kaingia kichwa kichwa.
 
Zamani nilikuwa nikisikia wazungu wanatuita manyani nilikuwa napata hasira sana, lakini baada ya kufuatilia vizuri nimegundua wako sahihi. Kila siku rais anasema anataka kuona siasa za kistaarabu za kuhubiri sera, kisha anatokea mtu anafanya igizo la kitoto la kusema alihujumu miradi, kwa akili hizo hizo za kinyani anasemehewa na nyani mwenzake badala ya kushitakiwa! Ajabu watu wanashangilia huo utoto!
Masharti ya zile pesa walizopewa ni kutumika kama hivi, utakaloambiwa ukaliseme ni lazima utii.

Ukishakula pesa ya ccm umekwisha.
 
Masharti ya zile pesa walizopewa ni kutumika kama hivi, utakaloambiwa ukaliseme ni lazima utii.

Ukishakula pesa ya ccm umekwisha.

Ahaaa ahaaa, kweli pesa ya shetani ni hatari. Uzuri sisi wapiga kura wa upinzani wengi tunajitambua na maamuzi tayari tumeshafanya. Hakuna uwezekano wa kutubadili kwa propaganda nyepesi.
 
Nikikumbuka CCM ya Kinana,Gama,Kolimba na kuilinganisha na ya Bashiru,kuna tofauti kubwa sana kiuongozi na kipropaganda.
Usiisahau ccm ya Wilson Mkama walichoma wenyewe banda la kuku halafu wakawasingizia Chadema, ilikuwa uchaguzi mdogo Igunga.
 
Akamatwe kwa kuhujumu uchumi na asipewe dhamana kama sheria zinavyotamka!Tofauti na hapo ni porojo tu na propaganda kumfurahisha Magufuli!
Chama cha Mbowe, kinaweza kufanya zaidi ya hayo aliyoyasema huyo jamaa. Kama majitu mazima yanaambiwa kila mwezi yapeleke 1.5M kama michango ya chama kwa mwamaume mwenzao mwenyekiti na wanatii sembuse kuzuia utekelezaji miradi? Chama cha mapunguani kabisa hicho.
 
Back
Top Bottom