Uchaguzi 2020 Omary Kumbilamoto atoboa siri za CHADEMA kuhujumu Miradi ya Awamu ya Tano

Kauli ya mnafiki anayejifanya mfia Chadema.
 
Hii awamu mbona imekuwa na watu wajinga wengi sn? Mzee kama huyu kukosa akili ni aibu.
 
Kama ni kweli walihujumu miradi ya maendeleo kwanini TAKUKURU wasimkamate uhujumu uchumi na amekiri?
 
Mwendelezo wa siasa za ghiliba, uzushi na uzandiki ili kumfurahisha bwana yule mpenda sifa
 
Tundu anaenda kupata aibu ya dunia awamu hii.
 
Duh CCM imechokwa kweli kweli yaani wamefikia hatua ya kutumia siasa nyepesi kiasi hiki.
Nikikumbuka CCM ya Kinana,Gama,Kolimba na kuilinganisha na ya Bashiru,kuna tofauti kubwa sana kiuongozi na kipropaganda.
 
Ningependa afafanue yeye na wenzake walihujumu namna gani

ili akileta ushahidi kwa namna walivyofanya wachukuliwe hatua iwe fundisho kwa jamii
 
Hawa wachumia tumbo wenu mliowanunua kwenye hii awamu yenu ya tano waambieni hawatawasaidia chochote.
 
Thread yako haina mashiko ni takataka tu kwa sababu Kumbilamoto hajawahi kuwanChadema hata siku moja.

Umekurupuka.
 
Lissu jibu hoja hizo za chadema kuhujumu maendeleo. Nimesikia nikashangaa na zisipojibiwa zitakuwa ni kweli
Magufuli kadanganywa huyu mpuuzi alikuwa CUF kabla ya kununuliwa na Jiwe kaingia kichwa kichwa.
 
Masharti ya zile pesa walizopewa ni kutumika kama hivi, utakaloambiwa ukaliseme ni lazima utii.

Ukishakula pesa ya ccm umekwisha.
 
Masharti ya zile pesa walizopewa ni kutumika kama hivi, utakaloambiwa ukaliseme ni lazima utii.

Ukishakula pesa ya ccm umekwisha.

Ahaaa ahaaa, kweli pesa ya shetani ni hatari. Uzuri sisi wapiga kura wa upinzani wengi tunajitambua na maamuzi tayari tumeshafanya. Hakuna uwezekano wa kutubadili kwa propaganda nyepesi.
 
Nikikumbuka CCM ya Kinana,Gama,Kolimba na kuilinganisha na ya Bashiru,kuna tofauti kubwa sana kiuongozi na kipropaganda.
Usiisahau ccm ya Wilson Mkama walichoma wenyewe banda la kuku halafu wakawasingizia Chadema, ilikuwa uchaguzi mdogo Igunga.
 
Akamatwe kwa kuhujumu uchumi na asipewe dhamana kama sheria zinavyotamka!Tofauti na hapo ni porojo tu na propaganda kumfurahisha Magufuli!
Chama cha Mbowe, kinaweza kufanya zaidi ya hayo aliyoyasema huyo jamaa. Kama majitu mazima yanaambiwa kila mwezi yapeleke 1.5M kama michango ya chama kwa mwamaume mwenzao mwenyekiti na wanatii sembuse kuzuia utekelezaji miradi? Chama cha mapunguani kabisa hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…