Omary Mjenga: Gharama za Gulf Stream kwenda Rio de Janerio Brazil ni mara 7 ya Dreamliner ya ATC

Wananchi waelezwe gharama yote ya Mhe. Rais kwenda Brazil kwenda na kurudi ikijumuisha ujumbe wake wote. Pili tuelezwe ni faida gani itapatikana na safari ya Mhe. Rais kwenda Brazil?.
 
Wananchi waelezwe gharama yote ya Mhe. Rais kwenda Brazil kwenda na kurudi ikijumuisha ujumbe wake wote. Pili tuelezwe ni faida gani itapatikana na safari ya Mhe. Rais kwenda Brazil?.
Brazil shamba au hujui
 

Hii inanikumbusha siku moja kama miezi miwili iliyopita.
Tunatoka Kigamboni kuja huku Feri.
Kivuko kinakaribia kushusha kuna mtu akawapa ishara ya kusogea mbele yani pale pakushukia mbele kabisa vijana wawili binti na mvulana,
wao wakawa wa kwanza kabisa, lakini ng'ambo kabisa kuna Gari jeusi lenye namba za Jeshi V8 imetugeukia na kuna kamanda kasimama na kaifungua milango ya Gari hilo.

Wale vijana wakashusha kwenye Kivuko na moja kwa moja wakaingia kwenye Gari fasta.
Ilikuwa ni kitendo cha harakaharaka sana hata kutokuweza kujiuliza kuwa inaweza ikawa ni damu ya kiboba gani wa 'Nji' hii.
Watu wakawa wanabung'aabung'aa tu.

Ila kuna watu wanakula matunda ya Uhuru nyie.

Acheni ujinga,
Tafuteni madaraka Kenge nyie.
 
Mimi nilichoka siku alipoenda ziara nchi Fulani ,ktk hotuba yake akamtambulisha mwanae Abdul 🥴🥴😔
 
Ndio ukaji wao
 
$ 5000 kwa gharama zipi? Kula, kulala, kusafiri bure. Bado per diem 5000! Naomba utaalamu hapa
Rais anaishi bure, ni kula kulala na analipwa na anacholipwa haijulikani analipwa kwa kusudi gani ikiwa anapatiwa huduma zote bure hata anapostaafu.
 
Hii ni the same ingekuwa kuna mtoto wa kibabo flani yupo chini ya jengo pale Kkoo. Hadi helicopter za jeshi zingetumika.

Nadhani kuna shida mahali katika kuelewa dhamani ya ubinadam. Kinachoangaliwa zaidi ni dhamani ya vyeo mkuu.
 
Wewe ndiye unahitaji msaada kwa ujinga wako wa kutokuelewa.
 
Huu urais ulimuangukia tu kwa bahati, labda Magufuli asingefariki naye asingekuwa rais, lakini kwakuwa iliisha kuwa hivyo muacheni ale raha, kila siku mnamtishia uchaguzi, ambao ni mwakani tu apo.

Jiulizeni asipokula leo atakula lini? Na huo ndio urefu wa kamba mliyompa.

Jamani mnataka president apande bus kwenda Brazil? Au mlitaka apande KLM au Air Frence? Au mlitaka apande Sea Horse?

Kapanda ndege ya Tanzania na watanzania 100 mnalalamika?

Juzi hapa tulikuwa tunalalamika kawakilishwa, sasa kaamua kwenda mwenyewe mnalalamika. Hata akienda kusikiliza tu muacheni aende, tulitaka rais akakutane na wenzake huko, au mnataka afanyeje?
 
Mkuu, kwa namna ulivyo orodhesha hayo maswali hapo juu inaonekana umemuelwa vizuri.

Tulitamani uyajibu halafu ndio muulize kama ameyaelewa majibu yako.

Au kweli wewe ni mtoto wa shule??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…