DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Maombi ya dharura namba 24511 ya mwaka 2025 yaliyofunguliwa na Humphrey Polepole dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) na wenzake wanne (4) imesikilizwa leo, Alhamisi Oktoba 09.2025 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam chini ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Salma Maghimbi
Kesi hiyo ambayo imefunguliwa na Humphrey Polepole kupitia kwa Wakili wake Peter Kibatala, imekuja kufuatia kutoweka katika mazingira tatanishi kwa Balozi huyo wa zamani wa nchi za Malawi na Cuba, ambapo kufuatia kutoweka kwake ndugu wa karibu wamenunuliwa mitandaoni wakidai kuwa wametekwa
Pamoja na mambo mengine, katika wasilisho lake Mahakamani hapo leo, Wakili Peter Kibatala ameiomba Mahakama kutoa amria ya haraka ili wajibu maombi wamlete Mahakamani mleta maombi (Humphrey Polepole) leo hii wakati wanasubiri kusikiliza hoja za pande zote mbili (2)
Akijibu hoja hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi Faraja Nguka ameieleza Mahakama kuwa maombi hayo hayatekelezeki kwakuwa kiapo kilichowasilishwa Mahakamani hapo na Wakili wa mleta maombi (Peter Kibatala) hakijaonesha wazi ni nani hasa ambaye amemshikilia Humphrey Polepole, lakini pia ameendelea kusema kuwa kupitia kiapo hicho Wakili anakili kwamba mteja wake amechukuliwa na watu wasiojulikana, na kwamba hadi sasa haijulikani alipo
Sambamba na hilo Wakili wa Serikali Mwandamizi Faraja Nguka ameieleza Mahakama kuwa, kupitia kiapo cha hicho, Wakili Peter Kibatala amedai kuwa ana mashaka kwamba mleta maombi anashikiliwa na mjibu maombi namba tano (5) katika kesi hiyo ambaye ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZPC)
'Akipangua' hoja hizo Wakili Peter Kibatala amefafanua kuwa katika kiapo chake amebainisha wazi kwamba wajibu maombi wote ambao kwa ujumla wao wanawakilisha Jamhuri wanapaswa kumleta Humphrey Polepole Mahakamani, lakini amesema kuwa ombi hilo mahsusi linamuhusu mjibu maombi wa tano ambaye ni ZPC
Amesema amelazimika kuweka umahususi kwa mjibu maombi wa tano kufuatia taarifa za awali alizozipata kutoka kwa ndugu wa Humphrey Polepole, akiwemo Godfrey na Augusto Polepole ambao taarifa zao na madai yao yameene kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na vyombo vya habari.
Chanzo: Jambo Tv