Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
- Thread starter
- #41
Wanabodi,
Hili ni ombi maalum kwa watu maalum, hivyo hii thread sio thread ya watu wote bali ni thread ya kutuma ujumbe maalum kwa watu maalum.
Tanzania sio nchi ya watu fulani tuu au chama fulani tuu, Tanzania ni ya Watanzania wote, wa vyama vyote, wa dini zote, wa makabila yote, wa jamii zote, wa jinsia zote, wa rangi zote, wa hali zote, na circumstances zozote,
Hivyo tunapokwenda kwenye uchaguzi, naomba kutoa ombi maalum kwa Wahusika Wakuu wa Uchanguzi huu wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020, uendeshwe kwa kutumia kanuni ya Kilatini ya "Ceteris Peribus" na sio kutumia zile kanuni zetu za kawaida za "Mutatis Mutandis!"
Tukikubali kutumia ceteris paribus badala ya mutatis mutandis, Taifa la Tanzania litabarikiwa, viongozi wetu watabarikiwa, na sisi wananchi pia, tutabarikiwa, na nchi yetu kupata neema ya mafanikio na maendeleo kwa wote.
Tukiendelea kufanya chaguzi zetu kwa mutatis mutandis, taifa letu tutalaaniwa, viongozi wetu sio tuu watalaaniwa, bali baadhi ya viongozi wanaoendekeza mutatis mutandis, wataadhibiwa kupitia kitu kinacho itwa karma.
Mungu mbariki Rais Magufuli, na watendaji wake wapate uwezo kuona ubaya wa kuendesha uchaguzi kwa mutatis mutandis, na badala yake watumie "Ceteris Peribus" kwa vyama vyote.
Mungu ibariki Tanzania.
NB. Sijaweka ufafanuzi wa maneno "Ceteris Peribus" na "Mutatis Mutandis" sio kwa bahati vibaya, nimefanya hivi makusudi kwa sababu ujumbe huu ni ujumbe maalum na mahsus kwa watu maalum ambao mimi nawajua huwa wanatembelea sana jf, kwa vile watu hao, wanayajua maneno hayo, wengine hayawahusu, sikuyafafanua ili ujumbe huu uwafikie walengwa wahusika tuu!..
Hata Mungu alipataka kumfikishia ujumbe maalum mfalme fulani, alimtumia kiganja cha mkono kikaandika kwenye ukuta wake, "Mene Mene Tekeli na Peresi".
Nawatakia Weekend Njema,
Paskali.
Mkuu Drifter, kwanza asante kwa mchango wako, very objective, kiukweli tangu nimepandisha uzi huu, wewe ndio mtu wa kwanza kunielewa, kwasababu, kiukweli kabisa, hii jf ya sasa, tuna watu wachache sana, wenye kuweza kusoma bandiko na kisha kujiuliza what is the motive behind.Swali moja rahisi sana kwako Paskali. CHADEMA ikifa, Watanzania na taifa kwa ujumla tutapata hasara gani? Unaamini NI LAZIMA CHADEMA iendelee kuwepo (exist)?
Maelezo yote hayo marefu sana uliyotoa na ambayo umekuwa ukiyatoa zaidi ya mwaka kuhusu CHADEMA, yanadhihirisha kuwa kwa mazingira ya kisiasa tuliyo nayo Tanzania, HAIWEZEKANI tuwe na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini ambao ni BONA FIDE GENUINE.
Halafu, VERY CURIOUSLY, siioni juhudi yako ya dhati kuwaasa wenye dhamana ya kutengeneza mazingira sahihi ya demokrasia ya vyama vingi Tanzania ili kuwezesha vyama kama CHADEMA kuwepo na kufanya shughuli zake kwa ufanisi. Hapo ungeeleweka badala ya kupania kwa makala kadhaa zilizojaa jazba nyingi kutaka CHADEMA IWEPO na ikubaliane na dola tu hata katika mazingira hatarishi kiasi gani!
WHAT’S YOUR REAL MOTIVE?
Chama cha Mapinduzi ni chama cha ukweli na haki, kiliasisiwa na Mwalimu Nyerere, mpenda haki na mtenda haki. Baada ya Mwalimu, CCM ilipitia mageuzi na kuishiwa kuhodhiwa na wenye fedha, hivyo kuzalisha kada kubwa ya makada wa CCM ambao ni makada maslahi, na kwenye uchaguzi, wanakuwa wako tayari kutumia mbinu zozote kushinda uchaguzi. JPM alipoingia, amekuja kuibadili CCM kuirudisha ile CCM ya Nyerere. Sasa ndani ya makada wa CCM, kuna makada wa aina mbili, kuna "CCM Die Hard", wafia chama, hawa ndio wanaotaka kuhakikisha CCM inashinda kwa mbinu zozote ikiwemo kuhakikisha inaupondaponda upinzani na kushinda kwa asilimia 99.9% kwa kutumia mbinu zozote.
Tupo sisi makada "Modern CCM" ambao kutokana na good track record ya kazi nzuri ya JPM, CCM itashinda kwa mshindi mzuri kishindo safi na clear victory, kushinda kwa haki bila kufanya figisu figisu zozote!.
Kwa vile Bunge letu ni Bunge la vyama vingi, na CCM ndio chama tawala, kina wajibu wa kulea upinzani. Mimi naamini kuna baadhi ya wana CCM tuko very genuine, tunapenda kuona CCM inashinda chaguzi bila figisu na baadhi ya wapinzani wakishinda akiwemo mtu kama Zitto, Mbowe, JJ.Myika, Lissu, Sugu, Mbatia etc, lakini kutokana na wapinzani 'kukataliwa' na wananchi, ili Bunge lichangamke, zile kamati 2 za oversight committee, PAC na LAAC, lazima ziongozwe na wabunge wa upinzania ambao ni vichwa vya ukweli, kwenye hao wabunge wote sijaona watu wa kalibre hiyo ndio maana kila siku, tunamuomba Mwenyekiti wetu, JPM, katika zile nafasi zake 10, awateua wapinzani 4, Zitto, JJ Mnyika, Mbatia na kale kabinti Queen Sendiga.
Ili CCM itawale vizuri inahitaji Upinzani makini, ndio maana kila uchao, naibalasa Chadema humu na ACT Zanzibar, waache ujinga wa kususa. Ili kusasa kwa akili ni kususa kama kwa kususa huko utaachieve something, lakini kususa tuu for the sake of kususa, huku you won't achieve anything huu ni ujinga!.
Karibu tena.
P