Uchaguzi 2020 Ombi: Ratiba ijayo ya Mikutano ya Kampeni za Tundu Lissu iangazie Wilaya za Rungwe na Kyela

Uchaguzi 2020 Ombi: Ratiba ijayo ya Mikutano ya Kampeni za Tundu Lissu iangazie Wilaya za Rungwe na Kyela

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Nafahamu wazi kwamba muda hautoshi kwa Mh Tundu Lissu kuweza kupita kila mahali kuomba kura , lakini kuna maeneo ambayo umuhimu wa Tundu Lissu kupita ni mkubwa sana , hii ni kutokana na mvuto wake wa kisiasa na hamasa waliyonayo wananchi wa kule .

Kyela ndio njia panda ya Malawi , nchi ambayo juzi tu iliweka historia mpya kwa kusimamia demokrasia ambapo Jeshi la nchi hiyo lilihakikisha kwamba mshindi halali anatangazwa bila kupunja chochote , kimsingi ujasiri wa wananchi wa Malawi ndio ujasiri wa Wananchi wa Kyela, ambao kwa miaka mingi wamekubali mabadiliko bila kujali vitish , ndio maana tunaomba sana Mh Lissu kwenye ratiba hii ya lala salama alikumbuke eneo hili ambalo kuanzia udhamini wake na sasa kampeni hajawahi kufika , kabla ya kufika Kyela ni lazima upite Rungwe , hapo utakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja , huku kuna kura za uhakika na ambazo hazina mashaka yoyote , ni kiasi cha kufika na kuongeza ujasiri tu .

Mungu Ibariki Chadema

Subpost 1 - Bibi zetu ujumbe wenu kama VIJANA tumeuelewa sana.   Mkasema kama VI ( 640 X 640 ).jpg

Rungwe na Kyela ni maeneo nyeti naamini huko kuna nguvu ya mabadiliko, Lissu kupita huko itakuwa vizuri sana, hasa jimbo la Kyela lenye mgombea mpya wa CCM naamini Chadema wanaweza chukua hilo jimbo.
 
Rungwe na Kyela ni maeneo nyeti naamini huko kuna nguvu ya mabadiliko, Lissu kupita huko itakuwa vizuri sana, hasa jimbo la Kyela lenye mgombea mpya wa CCM naamini Chadema wanaweza chukua hilo jimbo.
Una jicho la Tai
 
Ni muhimu lakini siku zimebaki chache sana bado hajaenda DSm,Arusha,Tanga,Dodoma, mtwara,Lindi ,ruvuma ,Hai ,Tabora na singida
 
Ni muhimu lakini siku zimebaki chache sana bado hajaenda DSm,Arusha,Tanga,Dodoma, mtwara,Lindi ,ruvuma ,Hai ,Tabora na singida
Arusha pameshaeleweka.

Tanga, Lindi, Mtwara, DSM, Ruvuma, Singida, Mafia huko si pa kukosa

Asije akafanya kosa akadharau mikoa ya kusini, huko ndo kuna kura za hasira ya gesi na korosho!
 
Arusha pameshaeleweka.

Tanga, Lindi, Mtwara, DSM, Ruvuma, Singida, Mafia huko si pa kukosa

Asije akafanya kosa akadharau mikoa ya kusini, huko ndo kuna kura za hasira ya gesi na korosho!
Kule kusini ni pakufanya mkutano moja moja kila mkoa coz Salum mwalimu alishapita kule.
Ratiba yake inaonyesha siku tatu za mwisho atakuwa singida
 
Arusha pameshaeleweka.

Tanga, Lindi, Mtwara, DSM, Ruvuma, Singida, Mafia huko si pa kukosa

Asije akafanya kosa akadharau mikoa ya kusini, huko ndo kuna kura za hasira ya gesi na korosho!
Rais wa wanyonge bwana magufuli kasema msichague viongozi kwa jazba, la sivyo na yeye atawaongoza kwa jazba
 
mugah di mathew , Missile of the Nation , Erythrocyte , denooJ ,

..Mnaweza kufuatilia Ratiba ya Wagombea Uraisi ktk link niliyoiweka hapo chini.

Ratiba ya TUNDU LISSU inaonyesha ifuatavyo:

October 10 to 11 amepangiwa kuwa Chamwino, Mvumi, Ikungi, Manyoni, Mkalama, Singida .

October 12 amepangiwa kuwa Tabora [Igunga, Nzega] Shinyanga[ Kahama].

October 13 amepangiwa kuwa Geita [ Mbogwe, Bukombe, Chato].

October 14 amepangiwa kuwa Mwanza[ Ukerewe ], Mara [ Rorya ].

October 15 amepangiwa kuwa Simiyu [ Itilima, Meatu, Bariadi ].

October 16 amepangiwa kuwa Tabora [ Tabora, Urambo,Kaliua].

October 17 amepangiwa kuwa Singida[ Manyoni], Dodoma [ Bahi, Kongwa, Dodoma ].

Ratiba ya SALUM MWALIMU inaonyesha kati ya October 10 to 17th atakuwa maeneo ya Iringa, Mbeya, Songwe, Rukwa, Kigoma, na Kagera.

https://www.nec.go.tz/uploads/documents/sw/1601631440-RATIBA YA KAMPENI TOLEO LA TANO.pdf
 
Na mimi naombi langu ingawa nje ya mada.
Wagombea wote waliotumia uchawi na uganga kwenye uchaguzi huu, bila kujali chama wala nafasi wanayogombea, wote washindwe.
Nimeona mnaweka maombi, na mimi naweka langu.
 
Back
Top Bottom